Ijue viettel mkombozi wa wanyonge

Ijue viettel mkombozi wa wanyonge

Ilisolokobwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
1,861
Reaction score
828
Kaka ulikuwa unawasikia hawa jamaa sasa leo nimeamini kweli watakuwa tishio ktk tasnia hii ya mawasiliano nchini Tanzania. Kwa muda mrefu akina voda wametuibia sana hadi wakafikia kufunga ndoa pamoja kwa kubana mb eti witandao yote wanatoa mb8 tu. Je ushindani iko wapi hapo?

NASEMA SHIKAMOO VIETEL
==========


Fahamu kwa Nini Mtandao Mpya wa Simu wa Viettel Unaogopeka! Wapewa Tuhuma za Kuhujumu Miundombinu ya Wengine

Kampuni mpya ya mtandao wa simu ambayo ata bado haijaanza kutoa huduma rasmi inazidi kuonekana tishio kwa wengine kwani haipiti muda bila kusikia habari kuhusu mtandao huu mpya. Leo tutakuambia kwa nini mtandao huu una uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa katika ushindani katika eneo la biashara na huduma ya mawasiliano ya simu Tanzania.

Kwanza tujikumbushe Viettel ni kina nani?

Tulishaandika kuhusu mtandao huu tokea taarifa za kuja kwao zilivyoanza kusikika rasmi, Viettel ni kampuni ya mtandao wa simu wenye makao makuu nchini Vietnam. Nchini Vietnam huu ni mtandao ndiyo namba moja nchini humo na unamilikiwa na serikali ya nchini humo kupitia Wizara ya Ulinzi wa nchi hiyo. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili tayari kampuni hiyo ishaingia kwenye nchi zingine zaidi ya 3 na hii ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mataifa yote iliyoingia.

Tuhuma za Kuhujumu Miundombinu ya Wengine…
Serikali kupitia Waziri Makame Mbarawa imepinga vikali tuhuma ya kwamba mtandao huu mpya unahujumu (haribu kwa kukusudia) mitambo ya wapinzani wake kwa sasa ambapo bado ipo katika utengenezaji wa mitambo yake nchini kote.
Waziri ametoa sifa kubwa kwa mtandao huu ya kwamba utawasaidia kwa kiasi kikubwa ata wale ambao wapo vijijini kutokana na kampuni hiyo kujikita kuhakikisha wanajenga minara yao maeneo mengi zaidi hii ikiwa ni mijini na vijijini. Hii ikiwa na baadhi ya maeneo ambayo hayajawahi kufikiwa na mitandao mingine ya simu.
Kuna mfuko wa kuchangia maendeleo ya mawasiliano vijijini unaolenga kupunguza mzigo wa gharama kwa makampuni ya simu pale wanapotaka kutengeneza miundombinu ya mawasiliano vijijini kwa kutambua ya kwamba huko kuna watumiaji wachache na hivyo kuchelewa kwa upatikanaji wa faida ya uwekezaji huo, inaonekana bado mitandao mingi ya simu haikutaka kutumia nafasi hii na sasa Viettel wanaitumia.

Je ni kweli mtandao wa Viettel unafaa kuogopeka?
Vyanzo vingi vinasema tayari mitandao mikubwa ya simu Tanzania, yaani Vodacom, Airtel na Tigo tayari wanakuna vichwa na kuhaha kuona ni jinsi gani kila mtu anajiweka katika mazingira mazuri ya kutoathirika na kuja kwa kampuni hii mpya ya simu.

Tuanzie nchini Vietnam…
Nchini humo mtandao wa Viettel unapatikana kwa takribani asilimia 98% ya maeneo yote yenye watu, hii ikimaanisha ni vigumu kwenda sehemu na ukapata shida ya network…wapo pande zote. Na karibia minara yao yote inarushwa signal za teknolojia ya haraka ya intaneti ya 3G (wana minara 32,000 ya 3G nchini humo).
Nchini East Timor….
Mwaka jana waliingia nchini East Timor na baada ya miezi sita wakawa tayari mtandao wao unawafikia zaidi ya asilimia 96 ya wananchi wa nchini humo. Na ndani ya mwaka mmoja wakawa wamefikisha zaidi ya watumiaji laki 5 kwa mtandao huo.

Nchini Cameroon….
Nguvu kubwa wameziweka katika kuhakikisha hawashuki chini zaidi ya teknolojia ya 3G… na hili linaonekana linawasaidia sana. Nchini humo wanatumia jina tofauti.
Wameingia nchini Cameroon mwezi wa kumi na mbili mwaka jana na ndani ya miezi minne tuu walifanikiwa kupata watumiaji zaidi ya milioni moja kwa mtandao wao na wakisifika sana katika huduma ya intaneti ya 3G kila kona.

Msumbiji (Mozambique) je?
Walipata leseni rasmi mwezi wa kwanza mwaka 2011, na kuanza kazi rasmi kufikia kati kati ya mwaka 2012…mwaka mmoja baadae tayari mtandao huo ukawa unapatikana kwa zaidi ya asilimia 85 kwa watu wote nchini humo…na network yao ikiwa imefunika nchi nzima kwa asilimia 80% na kuhakikisha takribani watu 600,000 wakipata network za mtandao wa simu katika maeneo yao kwa mara ya kwanza katika maisha yao. Nchini humo wanatumia jina la Movitel na tayari wanashikilia nafsi namba moja kwa mtandao wenye watumiaji wengi zaidi nchini humo, wana wateja zaidi ya milioni 5.

Burundi…
Wanatumia jina la Lumitel nchini Burundi na sasa na ndani ya mwezi mmoja toka kuanza kutoa huduma walifanikiwa kuandikisha wateja 600,000…NDANI YA MWEZI MMOJA kumbuka!

Na sasa Tanzania…

Kwa kiasi kikubwa kuna uwezekano mkubwa sana wa wao kufanya vizuri sana. Kwani kwa sasa ingawa ni miezi imepita tokea tuanze kuwasikia hawajaanza kutoa huduma ila wanajiweka sawa kwa kujenga miundombinu nchi nzima wakiwa na lengo la kuanza huduma wakiwa tayari unaweza kupata huduma zao nchini kote. Na hapa ndio tunaona wamefanya cha maana sana.

Na pia nguvu yao nyingine itakuwa katika huduma ya intaneti ambapo wao wanakuja na huduma ya 3G moja kwa moja, hii ina maanisha hautakuwa na wasiwasi wa kupata huduma ya 2G ukiwa mikoani…ndani ndani hivi.Tusubiri tuone, ila na uhakika kuna mabadiliko makubwa katika ushindani yatatokea miezi michache baada ya Viettel kuanza kutoa huduma zake rasmi.

Mitandao ya simu iliyopo inatakiwa kuendelea kukuna kichwa na kuhakikisha inaboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kabla jamaa hawajaanza kutoa huduma rasmi…na hapa muda ndio huu unaisha kwani ndani miezi miwili mitatu ijayo huduma za hawa jamaa zinaweza anza rasmi. Kizazi cha sasa hivi kubadirisha laini haichukui muda sana hasa kama kufanya hivyo kutahakikisha unapata huduma bora zaidi.

CHANZO: Teknokona
 
kuna mahusiano gani kati ya kumkomboa mnyonge na kusambaza network nchi nzima? unless walete vifurushi vya bei rahisi zaidi ya hivi vilivyokuepo.

mtandao wa smart upo nchi nzima tena kwa 3g, nimejaribu maeneo mengi ambapo voda/tigo/airtel hawapo ila wao wapo, je wamemkomboa nani? wana kitu kinachomvutia mtu?

mitandao ya simu ina operate kama oligopoly hata wao wakija wataendelea na mb8 za vifurushi vya kupiga sababu hayo ni makubaliano waliyokaa wenyewe na tcra, tulitakiwa sisi tuwaulize maswali hao tcra watupe majibu kuna hekima gani nyuma ya hizo mb8
 
Kwa kuwa mimi sio mnyonge,huo mtandao haunihusu kabisa
 
kuna mahusiano gani kati ya kumkomboa mnyonge na kusambaza network nchi nzima? unless walete vifurushi vya bei rahisi zaidi ya hivi vilivyokuepo.

mtandao wa smart upo nchi nzima tena kwa 3g, nimejaribu maeneo mengi ambapo voda/tigo/airtel hawapo ila wao wapo, je wamemkomboa nani? wana kitu kinachomvutia mtu?

mitandao ya simu ina operate kama oligopoly hata wao wakija wataendelea na mb8 za vifurushi vya kupiga sababu hayo ni makubaliano waliyokaa wenyewe na tcra, tulitakiwa sisi tuwaulize maswali hao tcra watupe majibu kuna hekima gani nyuma ya hizo mb8
chiefmkwawa ngoja waje tuwajaribu nao ili tuone watakuja na kipi kipya ila binafsi nafurahishwa na ujio wao.unajua hawa akina tigo na wenzake ni wezi sana mfano unaweza ukawa ktk eneo lenye 3g lakini bado mtandao unakuwa slow.
Kutokana sa sifa wanazomiminiwa hawa viettel hakika lazima niwakubali lakini hata hivyo wakija itakuwa ni changamoto kwa makampuni yaliyopo
 
Last edited by a moderator:
Huo ni mwanzo tu wa daganya toto akisha kaa mwaka tu lazima nae ataiga sera za wenzie
 
chiefmkwawa ngoja waje tuwajaribu nao ili tuone watakuja na kipi kipya ila binafsi nafurahishwa na ujio wao.unajua hawa akina tigo na wenzake ni wezi sana mfano unaweza ukawa ktk eneo lenye 3g lakini bado mtandao unakuwa slow.
Kutokana sa sifa wanazomiminiwa hawa viettel hakika lazima niwakubali lakini hata hivyo wakija itakuwa ni changamoto kwa makampuni yaliyopo

Kaka case za mitandao kuwa slow na matatizo mengi zipo dunia nzima, mobile data kazi yake si kushusha vitu vikubwa toka net Ni kwa ajili ya vitu vidogo kama Whatsapp na fb

Tz tunahitaji mbadala WA mo mobile data kama vile internet za waya. Kuwe na isp anaetoa unlimited data kwa bei nafuu asambaze majumbani kama nchi zilizoendelea.
 
Last edited by a moderator:
chiefmkwawa ngoja waje tuwajaribu nao ili tuone watakuja na kipi kipya ila binafsi nafurahishwa na ujio wao.unajua hawa akina tigo na wenzake ni wezi sana mfano unaweza ukawa ktk eneo lenye 3g lakini bado mtandao unakuwa slow.
Kutokana sa sifa wanazomiminiwa hawa viettel hakika lazima niwakubali lakini hata hivyo wakija itakuwa ni changamoto kwa makampuni yaliyopo

inajulikana wakija watatumia " market penetration" kama mitandao mengine itatoa MB 8 basi wao wataziongeza perhaps ziwe MB 10" lol. then baada ya hapo kitaeleweka..watashuka hadi MB 8
 
Last edited by a moderator:
Naona waizi wanaongezeka nyie wanyonge ndio mtanyongwa mpaka mfe..Mitandao yote nchini wanafwata kanuni za TCRA sasa nini kipya hapo au wataleta 2Gb 100 Minute 10000 Sms Per day(24 hrs)...
 
kwanza hakuna pride yoyote kwa shirika la simu la nchi nyingine kuja kuweka mtandao wake apa.... hii kazi ilitakiwa ifanywe na TTCL sidhan kama utaenda kwa jiran zetu kama kenya watakuruhusu uweke mtandao mwingine wao kila kitu ni through safaricom tujifunzxe kukuza vya kwetu na tuachane kutukuza upuuz wa makampun ya nje hamna uwekezaj wowote ulio beneficial kwa host country ni kiini macho tu!!!
 
whereish!(hic) titishiel(hic when y'need it?(hic)where izh it? eh (hic)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom