Ijue sheria ya makosa ya jinai

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
IJUE SHERIA

Imeandaliwa
Na. Jose

Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
Taratibu za mwenendo wa makosa ya jinai

TARATIBU ZA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI.

HATUA YA 1.
Nini maana ya Jinai? Jinai ni kosa au makosa yanayofanywa na mtu/watu/taasisi kupitia watendaji wake,kinyume cha sheria au taratibu zilizoainisha makosa mabalimbali. kwa mfano makosa yote yaliyoainishwa katika sheria ya kanuni za Adhabu Sura ya 16(Penal Code).

MATOKEO YA KUTENDA KOSA LA JINAI;
Mtu yeyote anayetuhumiwa/kushitakiwa kwa kosa la jinai inachukuliwa kuwa ameikosea au ametenda kosa dhidi ya Jamhuri. Maana yake ni kwamba mtenda kosa au mtuhumiwa huwa anachukuliwa kuwa ameikosea jamii ya watu waliokubali na kupitisha sheria au taratibu zilizowekwa.

Mara tu mtuhumiwa anapoonekana ametenda kosa la jinai, hatua zifuatazo zinapaswa kufuatwa:

KUKAMATWA
(kwa mujibu wa kifungu cha 11-33 kanuni za mwenendo wa makosa ya jinai).

Hii ni hatua ya kumtia mtuhumiwa nguvuni au chini ya ulinzi kabla ya kumfikisha katika vyombo vya dola. Vyombo vya dola ni pamoja na polisi au mlinzi wa amani.

a) WATU/VYOMBO VYENYE MAMLAKA YA KUKAMATA.
Ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anatiwa nguvuni vyombo vifuatavyo vimepewa mamlaka ya ukamataji:-
i)Polisi
ii)Afisa Usalama au askari kanzu
iii)Mkuu wa mkoa/wilaya
iv)waziri
v)Raia
vi)Hakimu
vii)Rais wa nchi

HATUA ZA UKAMATAJI
Ukamataji uko wa aina kuu mbili:-
i)Ukamataji wa kutumia hati(warrant of arrest)
ii)Ukamataji bila hati(without warrant of arrest).

HATUA YA 2.

UKAMATAJI WA KUTUMIA HATI(Warrant of arrest)
Kwa kawaida hati hii hutolewa na polisi kwa ajili ya kumkamata mtu anayetuhumiwa kwa kosa la jinai baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji.

Yaliyomo katika hati ya kukamatwa(kwa mujibu wa kifungu cha 120)Hati ya kukamata inapaswa iwe na vitu vifuatavyo:-

i)Iwe imetolewa na mkuu wa kituo cha polisi au hakimu
ii)Lazima iwe na mhuri wa polisi au mahakama
iii)Iwe imesainiwa;
iv)Lazima iwe na maelezo ya mtuhumiwa k.m. Jina, kabila, dini n.k
v)Lazima iseme kuwa mtuhumiwa akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

UKAMATAJI BILA KUWA NA HATI.
Watu watu/vyombo nilivyovitaja awali wanaweza kumkamata mtuhumiwa bila kuwa na hati ya ukamataji baada ya mtuhumiwa kuonekana ametenda kosa la jinai mbele yao.

DHAMANA
Dhamana ni ruhusa anayopewa mtuhumiwa au mshitakiwa wakati akisubiri shitaka lake kupelekwa au kusikilizwa mahakani au akisubiri hatma ya rufaa yake;

DHAMANA HUWEZA KUTOLEWA NA:-
i) Jaji au hakimu
ii)Mkuu wa kituo cha polisi;
Kwa hiyo mara mtuhumiwa anapofikishwa kituo cha polisi au mahakamani ana haki ya kuomba na kupewa dhamana isipokuwa kwa makosa ya mauaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uhaini.

MUDA WA KUFIKISHWA MBELE YA SHERIA.
Kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa anapokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi ni wajibu wa polisi kumfikisha au kupeleka shitaka lake mahakamani ndani ya masaa 48.

HATI YA MASHITAKA
Hii ni hati inayoelezea mambo yafuatayo:-
i)Jina, umri, dini, kabila au taifa na sehemu anayoishi mtuhumiwa.
ii)Kosa au makosa anayotuhumiwa;
iii)Kifungu au vifungu vya sheria alivyovivunja;
iv)Maelezo ya mazingira aliyotenda kosa.

NB: Mwendesha mashtaka anayo ruhusa ya kubadilisha hati ya mashtaka kabla ya kesi haijaanza kusikilizwa.

HATUA YA 3.

UPEKUZI NA UKAMATAJI MALI NA VITHIBITISHO AU VIELELEZO.

a)UPEKUZI.
Mtuhumiwa anapotiwa nguvuni na kufikishwa kituo cha polisi, polisi hulazimika kufanya upekuzi kwa mtuhumiwa ili kupata vielelezo au vithibitisho. Kazi hii hufanyika kwa mtuhumiwa mwenyewe mara tu anapofikishwa kituo cha polisi, hata hivyo, polisi wanaweza kulazimika kupata vielelezo zaidi kwenye maeneo mbalimbali yanayohisiwa kuwa mtuhumiwa anaweza kuwa amehifadhi vielelezo au vithibitisho. Polisi wana mamlaka ya kumpekua mtuhumiwa anapofikishwa kituo cha polisI bila kuwa na hati ya upekuzi(search warrant). Lakini polisi wanapolazimika kupata ushahidi maeneo mbalimbali yanayohisiwa kuwa na ushahidi wanawajibika kupata hati ya upekuzi. Hati hii hutolewa na mkuu wa kituo chochote cha polisi au hakimu.

b)MUDA WA KUFANYA UPEKUZI.
Kwa kawaida upekuzi unapaswa kufanywa siku yeyote isipokuwa siku ya Jumapili, na unaweza kufanyika masaa yeyote kuanzia jua linapochomoza na kabla ya jua kuzama.

Hata hivyo polisi wanaweza kuomba kibali kutoka mahakamani cha kufanya upekuzi muda wowote. Endapo imelazimika upekuzi kufanyika wakati wa usiku, afisa yeyote wa polisi aliyefanya upekuzi kwa mujibu wa hati ya upekuzi atalazimika kutoa sababu iliyomlazimu mbele ya hakimu.

c)UKAMATAJI WA MALI NA VIELELEZO AU VITHIBITISHO.

Wakati upekuzi unafanyika, polisi wakiona kitu chochote kinachoweza kuwa ushahidi au kusaidia kama kielelezo katika shitaka au kinachoshukiwa kuwa kimetumika au kingetumika kutenda kosa, basi polisi wanaweza kukikamata au kukichukua kwa ajili ya ushahidi.

Vielelezo au vithibitisho au mali inapokuwa imechukuliwa ni wajibu wa polisi kutoa stakabadhi ambayo itakuwa na saini ya mmiliki wa vielelezo au vithibitisho au mali iliyochukuliwa au vielelezo vitatumika kama ushahidi mahakamani.

HATUA YA 4.

UCHAGUZI WA KOSA.
Baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa hulazimika kufanya uchunguzi ili kupata ukweli au maelezo yatakayosaidia kupata ukweli wa jambo au mambo yatayosaidia kuendesha shitaka kihalali. Katika kufanya hivyo polisi hulazimika kufanya na kuzingatia mambo yafuatayo:-

a)KUMHOJI MTUHUMIWA;

Maofisa wa polisi wanauwezo wa kisheria, kumhoji mshitakiwa ili kupata taarifa zitakazo saidia uendeshaji wa shitaka na kwa upande wa pili, mtuhumiwa naye anayo nafasi ya kujibu mahojiano ya polisi.
Wakati wa mahojiano, polisi anapaswa kuyaweka katika maaandishi mahojiano yake na mtuhumiwa. Mahojiano haya yanapaswa kufanyika ndani ya masaa 4 tangu mtuhumiwa akamatwe.

a)WAJIBU WA POLISI WAKATI WA MAHOJIANO

Polisi anawajibu mbalimbali wa kufanya wakati wa mahojiano. Wajibu huu ni pamoja na:-
i)Kumtaarifu mtuhumiwa kuwa ana haki ya kukataa kutoa maelezo yoyote(kifungu(2)).
ii)Kumtaarifu mtuhumiwa jina lake,cheo chake,kosa la mtuhumiwa na kuwa na maelezo yake yatatumiwa kama ushahidi wakati wa kuendesha shtaka.
Iii) Anapaswa ampatie mtuhumiwa nakala ya maelezo ya mahojiano iliasome na kuyakubali kuwa ni maelezo sahihi aliyoyatoa.
iv)Anapaswa kumweleza mtuhumiwa kuwa ana haki ya kupata mwanasheria, na vilevile kuonana na familia yake.
v)Anapaswa kumweleza mtuhumiwa kuwa ana haki ya kupata matibabu kama mtuhumiwa atakuwa anaumwa au ana majeraha.
vi)Kama mtuhumiwa atakuwa ni mtoto wa umri chini ya miaka 18 basi mzazi au mlezi anapaswa kuwepo wakati wa kuuliza maswali.
vii)Anawajibu wa kutotumia nguvu na kutomlazimisha mtuhumiwa wakati wa mahojiano.

c)WAJIBU WA MTUHUMIWA WAKATI WA MAHOJIANO.

Mtuhumiwa ana wajibu ufuatao katika mahojiano:
i)Kusikiliza mahojiano dhidi yake na polisi nakisha kujibu au kunyamaza kimya.
ii)Ana haki ya kuuliza jina na cheo cha polisi anayeendesha mahojiano.
iii)Kusoma nakala ya mahojiano na kuikubali kuwa ni sahihi au la kisha kuweka saini kama ni sahihi kuidhinisha kukubali kwake, na ama kutotia saini ili kupinga utofauti wa maelezo yake sahihi na yale yaliyopo katika maandishi.

HATUA YA 5.

HATUA ZA KUMWITA MTUHUMIWA(kwa mujibu wa kifungu 100-109)

Baada ya shtaka kufikishwa mahakamani, mahakama hutoa waraka(samansi) wa kumuita mtuhumiwa mahakamani. Waraka huo unapaswa uwe:

Umetiwa saini na kugongwa mhuri wa mahakama. Samansi hupelekwa kwa mtuhumiwa na polisi, karani wa mahakama au mtumishi yeyote atakayepewa amri ya kufanya hivyo na mahakama.

Mtuhumiwa au mtu yeyote anayepokea nakala hiyo (samansi) anapaswa kusaini nyuma ya nakala hiyo kuthibitisha kuwa amepata habari ya wito.
Kama mtuhumiwa hakupatikana basi samansi atapewa mtu yeyote wa familia au mwajiri wake au mtu yeyote aliye karibu naye. Mtu huyu atalazimika kutia saini yake nyuma ya nakala. Kama mtuhumiwa ni afisa mkubwa wa serikali au shirika basi nakala hiyo itapelekwa kwa mkuu wa idara yake na mkuu wake atahakikisha mtuhumiwa anapata nakala ya samansi.

Kama mtuhumiwa ni shirika lenye nguvu ya kisheria basi samansi itapelekwa kwa viongozi au katibu. Kama mtuhumiwa aliye karibu naye hatapatikana, basi mahakama itatoa ruhusa ya kupeleka nakala hiyo mahali popote anapoweza kupatikana. Hivyo basi mtu aliyepeleka nakala hiyo hulazimika kutoa kiapo mbele ya mahakama kuwa amefikisha nakala hiyo. Baada ya hatua ya kumpelekea samansi kukamilika mahakama itamtegemea mtuhumiwa kuwepo mahakamani.

MATOKEO YA KUTOKUFIKA MAHAKAMANI:

Iwapo mtuhumiwa hatofika mahakamani na mahakama itakapofahamishwa kuwa mtuhumiwa alipelekewa samansi basi mahakama itatoa amri ya kukamatwa kwa mtuhumiwa(warrant of arrest).

UENDESHWAJI WA SHITAKA

Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani atasomewa shitaka na baada ya kusomewa shitaka mtuhumiwa ana haki zifuatazo:-

i)Kukubali kosa
ii)Kukana kosa
iii)Kunyamaza kimya
iv)Kuifahamisha mahakama kuwa alikwisha kutumikia kifungo.

KUKUBALI KOSA;

Kama mtuhumiwa atakubali kosa mahakama itajiridhisha kuwa mtuhumiwa amekubali kosa akiwa na akili timamu au la. Basi mahakama haina budi kumtia hatiani mtuhumiwa kwa sheria na kifungu kinachohusika.

KUKANA KOSA;

Iwapo mtuhumiwa atakana kosa, mahakama yaweza kuamua kusikiliza au kuahirisha na kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza.
Hata hivyo, kabla ya kuahirisha kesi mahakama itamweleza mtuhumiwa haki yake ya kupata dhamana endapo hakuwa na dhamana. Vilevile mahakama itaziomba pande zote mbili kuita mashahidi au kuleta mashahidi.

HATUA YA 6 NA YA MWISHO.

KUSIKILIZWA KWA SHITAKA.

Mahakama itaanza kusikiliza shitaka kwa kutoa nafasi ya kwanza upande wa mlalamikaji au walalamikaji kueleza shitaka na kutoa ushahidi. Katika hatua hii upande wa utetezi una haki ya kuhoji mashahidi upande wa pili ili kuthibitisha shitaka bila shaka yoyote.

Baada ya mahojiano kutoka upande wa utetezi mahakama hutoa nafasi ya mwisho kwa upande wa walalamikaji/mlalamikaji kufafanua hoja zilizokinzana wakati wa mahojiano na upande wa utetezi.

Upande wa utetetzi hupewa nafasi ya kutoa utetezi wake na kisha kuhojiwa na upande wa walalamikaji/mlalamikaji kama ilivyoainishwa hapo juu.

MUHIMU: Katika kusikiliza makosa ya jinai,mahakama ya mwanzo na mahakama kuu zinapaswa kuwa na wazee wa baraza.
HUKUMU.

Baada ya pande zote mbili kufunga ushahidi wake, mahakama huwajibika kutoa hukumu, amri na uamuzi. Matokeo ya uamuzi huashiria kifungo au kuachiliwa huru kwa mtuhumiwa.

ANGALIZO: Hukumu hutoa nafasi ya kukata rufaa. Rufaa yaweza kukatwa kutoka mahakama ya mwanzo kwenda mahakama ya wilaya, au kutoka mahakama ya wilaya kwenda mahakama kuu. Pia rufaa yaweza kukatwa toka mahakama kuu kwenda mahakama ya rufaa.

Baada ya hukumu kusomwa na kabla mshtakiwa kutamkiwa adhabu, mshitakiwa anayo haki yakuomba apunguziwe adhabu kwa kutoa sababu za msingi mfano mzee, ulemavu, kutegemewa na famila na tabia yake nzuri kwa jamii.

NAIMANI SASA HAMTAHUJUMIWA NA WANASIASA WALA POLISI MAANA UKWELI MMEUJUA, TUWEKE MASLAHI YA TAIFA MBELE KWANZA...

taratibu za mwenendo wa makosa ya jinai.

hatua ya 1.
nini maana ya jinai? Jinai ni kosa au makosa yanayofanywa na mtu/watu/taasisi kupitia watendaji wake,kinyume cha sheria au taratibu zilizoainisha makosa mabalimbali. Kwa mfano makosa yote yaliyoainishwa katika sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16(penal code).

matokeo ya kutenda kosa la jinai;
mtu yeyote anayetuhumiwa/kushitakiwa kwa kosa la jinai inachukuliwa kuwa ameikosea au ametenda kosa dhidi ya jamhuri. Maana yake ni kwamba mtenda kosa au mtuhumiwa huwa anachukuliwa kuwa ameikosea jamii ya watu waliokubali na kupitisha sheria au taratibu zilizowekwa.

kukamatwa

A) watu/vyombo vyenye mamlaka ya kukamata.
ili kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anatiwa nguvuni vyombo vifuatavyo vimepewa mamlaka ya ukamataji:-
i)polisi
ii)afisa usalama au askari kanzu
iii)mkuu wa mkoa/wilaya
iv)waziri
v)raia
vi)hakimu
vii)rais wa nchi

hatua za ukamataji
ukamataji uko wa aina kuu mbili:-
i)ukamataji wa kutumia hati(warrant of arrest)
ii)ukamataji bila hati(without warrant of arrest).

hatua ya 2.

ukamataji wa kutumia hati(warrant of arrest)
kwa kawaida hati hii hutolewa na polisi kwa ajili ya kumkamata mtu anayetuhumiwa kwa kosa la jinai baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji.
arrest warrant inatolewa na hakimu/jaji na kuelekezwa kwa mtu atakae affect hiyo arrest(polisi n.k) section 110 cpa, section 112 cpa and section 130 cpa

yaliyomo katika hati ya kukamatwa(kwa mujibu wa kifungu cha 120)

kifungu hiki (120) kinahusu arrest arrest outside of the local jurisdiction of the courtwhich issues the arrest warrant na si content ya arrest warrant kama ulvyosema hapo juu.
hati ya kukamata inapaswa iwe na vitu vifuatavyo:-

i)iwe imetolewa na mkuu wa kituo cha polisi au hakimu
ii)lazima iwe na mhuri wa polisi au mahakama
iii)iwe imesainiwa;
iv)lazima iwe na maelezo ya mtuhumiwa k.m. Jina, kabila, dini n.k
v)lazima iseme kuwa mtuhumiwa akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
haya yote ni kulingana na section 112 (2) na si kma ulivyosema sectin 120 hapo juu

ukamataji bila kuwa na hati.
watu watu/vyombo nilivyovitaja awali wanaweza kumkamata mtuhumiwa bila kuwa na hati ya ukamataji baada ya mtuhumiwa kuonekana ametenda kosa la jinai mbele yao.

dhamana
dhamana ni ruhusa anayopewa mtuhumiwa au mshitakiwa wakati akisubiri shitaka lake kupelekwa au kusikilizwa mahakani au akisubiri hatma ya rufaa yake;

dhamana huweza kutolewa na:-
i) jaji au hakimu
ii)mkuu wa kituo cha polisi;
kwa hiyo mara mtuhumiwa anapofikishwa kituo cha polisi au mahakamani ana haki ya kuomba na kupewa dhamana isipokuwa kwa makosa ya mauaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uhaini.

muda wa kufikishwa mbele ya sheria.
kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa anapokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi ni wajibu wa polisi kumfikisha au kupeleka shitaka lake mahakamani ndani ya masaa 48.

hati ya mashitaka
hii ni hati inayoelezea mambo yafuatayo:-
i)jina, umri, dini, kabila au taifa na sehemu anayoishi mtuhumiwa.
Ii)kosa au makosa anayotuhumiwa;
iii)kifungu au vifungu vya sheria alivyovivunja;
iv)maelezo ya mazingira aliyotenda kosa.

Nb: mwendesha mashtaka anayo ruhusa ya kubadilisha hati ya mashtaka kabla ya kesi haijaanza kusikilizwa.
as per section 234 of the cpa alteration of a charge inafanyika muda wowote kabla ya hukumu by either a)amendment of the charge b)substitute a new charge c)adition of a new charge. Nb. After alteration mtuhumiwa lazma aitwe kuapa upya over the altered charge and alteration itafanyika tu bila kusababisha injustice.

hatua ya 3.

upekuzi na ukamataji mali na vithibitisho au vielelezo.

A)upekuzi.
mtuhumiwa anapotiwa nguvuni na kufikishwa kituo cha polisi, polisi hulazimika kufanya upekuzi kwa mtuhumiwa ili kupata vielelezo au vithibitisho. kazi hii hufanyika kwa mtuhumiwa mwenyewe mara tu anapofikishwa kituo cha polisi,
search of persons hufanyika mara 2. A)mara tu baada ya kukamatwa b) baada ya kufikishwa kituo cha polisi as per sections 27 and 41 of the cpa cap 20 r.e 2002

hata hivyo, polisi wanaweza kulazimika kupata vielelezo zaidi kwenye maeneo mbalimbali yanayohisiwa kuwa mtuhumiwa anaweza kuwa amehifadhi vielelezo au vithibitisho. Polisi wana mamlaka ya kumpekua mtuhumiwa anapofikishwa kituo cha polisi bila kuwa na hati ya upekuzi(search warrant). Lakini polisi wanapolazimika kupata ushahidi maeneo mbalimbali yanayohisiwa kuwa na ushahidi wanawajibika kupata hati ya upekuzi. Hati hii hutolewa na mkuu wa kituo chochote cha polisi au hakimu.

b)muda wa kufanya upekuzi.
kwa kawaida upekuzi unapaswa kufanywa siku yeyote isipokuwa siku ya jumapili, na unaweza kufanyika masaa yeyote kuanzia jua linapochomoza na kabla ya jua kuzama.

hata hivyo polisi wanaweza kuomba kibali kutoka mahakamani cha kufanya upekuzi muda wowote. Endapo imelazimika upekuzi kufanyika wakati wa usiku, afisa yeyote wa polisi aliyefanya upekuzi kwa mujibu wa hati ya upekuzi atalazimika kutoa sababu iliyomlazimu mbele ya hakimu.

c)ukamataji wa mali na vielelezo au vithibitisho.

wakati upekuzi unafanyika, polisi wakiona kitu chochote kinachoweza kuwa ushahidi au kusaidia kama kielelezo katika shitaka au kinachoshukiwa kuwa kimetumika au kingetumika kutenda kosa, basi polisi wanaweza kukikamata au kukichukua kwa ajili ya ushahidi.

hatua ya 4.

uchaguzi wa kosa.
baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa hulazimika kufanya uchunguzi ili kupata ukweli au maelezo yatakayosaidia kupata ukweli wa jambo au mambo yatayosaidia kuendesha shitaka kihalali. Katika kufanya hivyo polisi hulazimika kufanya na kuzingatia mambo yafuatayo:-

a)kumhoji mtuhumiwa;

maofisa wa polisi wanauwezo wa kisheria, kumhoji mshitakiwa ili kupata taarifa zitakazo saidia uendeshaji wa shitaka na kwa upande wa pili, mtuhumiwa naye anayo nafasi ya kujibu mahojiano ya polisi.

a)wajibu wa polisi wakati wa mahojiano

polisi anawajibu mbalimbali wa kufanya wakati wa mahojiano. Wajibu huu ni pamoja na:-
i)kumtaarifu mtuhumiwa kuwa ana haki ya kukataa kutoa maelezo yoyote(kifungu(2)).
Ii)kumtaarifu mtuhumiwa jina lake,cheo chake,kosa la mtuhumiwa na kuwa na maelezo yake yatatumiwa kama ushahidi wakati wa kuendesha shtaka.
Iii) anapaswa ampatie mtuhumiwa nakala ya maelezo ya mahojiano iliasome na kuyakubali kuwa ni maelezo sahihi aliyoyatoa.
Iv)anapaswa kumweleza mtuhumiwa kuwa ana haki ya kupata mwanasheria, na vilevile kuonana na familia yake.
V)anapaswa kumweleza mtuhumiwa kuwa ana haki ya kupata matibabu kama mtuhumiwa atakuwa anaumwa au ana majeraha.
Vi)kama mtuhumiwa atakuwa ni mtoto wa umri chini ya miaka 18 basi mzazi au mlezi anapaswa kuwepo wakati wa kuuliza maswali.
Vii)anawajibu wa kutotumia nguvu na kutomlazimisha mtuhumiwa wakati wa mahojiano.

c)wajibu wa mtuhumiwa wakati wa mahojiano.

I)kusikiliza mahojiano dhidi yake na polisi nakisha kujibu au kunyamaza kimya.
Ii)ana haki ya kuuliza jina na cheo cha polisi anayeendesha mahojiano.
Iii)kusoma nakala ya mahojiano na kuikubali kuwa ni sahihi au la kisha kuweka saini kama ni sahihi kuidhinisha kukubali kwake, na ama kutotia saini ili kupinga utofauti wa maelezo yake sahihi na yale yaliyopo katika maandishi.

hatua ya 5.

hatua za kumwita mtuhumiwa(kwa mujibu wa kifungu 100-109)

baada ya shtaka kufikishwa mahakamani, mahakama hutoa waraka(samansi) wa kumuita mtuhumiwa mahakamani. Waraka huo unapaswa uwe:

arrest ni alternative ya summons: Mtu akikaidi summons ndipo arrest hutumika though kwa baadhi ya makosa ambayo ni capital ofences au hatari kwa jamii moja kwa moja au makosa ya papo kwa papo(kutenda kosa mbele ya police au mtu yeyote) hayahitaji summons

matokeo ya kutokufika mahakamani:

iwapo mtuhumiwa hatofika mahakamani na mahakama itakapofahamishwa kuwa mtuhumiwa alipelekewa samansi basi mahakama itatoa amri ya kukamatwa kwa mtuhumiwa(warrant of arrest).

uendeshwaji wa shitaka

baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani atasomewa shitaka na baada ya kusomewa shitaka mtuhumiwa ana haki zifuatazo:-

i)kukubali kosa
ii)kukana kosa
iii)kunyamaza kimya
iv)kuifahamisha mahakama kuwa alikwisha kutumikia kifungo.

kukubali kosa;

kama mtuhumiwa atakubali kosa mahakama itajiridhisha kuwa mtuhumiwa amekubali kosa akiwa na akili timamu au la. Basi mahakama haina budi kumtia hatiani mtuhumiwa kwa sheria na kifungu kinachohusika.

kukana kosa;

iwapo mtuhumiwa atakana kosa, mahakama yaweza kuamua kusikiliza au kuahirisha na kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza.

hatua ya 6 na ya mwisho.

kusikilizwa kwa shitaka.

mahakama itaanza kusikiliza shitaka kwa kutoa nafasi ya kwanza upande wa mlalamikaji au walalamikaji kueleza shitaka na kutoa ushahidi. katika hatua hii upande wa utetezi una haki ya kuhoji mashahidi upande wa pili ili kuthibitisha shitaka bila shaka yoyote.

muhimu: katika kusikiliza makosa ya jinai,mahakama ya mwanzo na mahakama kuu zinapaswa kuwa na wazee wa baraza.
Hukumu.

angalizo: hukumu hutoa nafasi ya kukata rufaa. Rufaa yaweza kukatwa kutoka mahakama ya mwanzo kwenda mahakama ya wilaya, au kutoka mahakama ya wilaya kwenda mahakama kuu. Pia rufaa yaweza kukatwa toka mahakama kuu kwenda mahakama ya rufaa.

naimani sasa hamtahujumiwa na wanasiasa wala polisi maana ukweli mmeujua, tuweke maslahi ya taifa mbele kwanza UTII WA KUJUA SHERIA NI BORA KULIKO KITU CHOCHOTE..

By J
 
Je mwendesha mashitaka anaweza kuondoa mashitaka yako baada ya kuyasoma mahakamani, au anaweza kuondoa shauri lako likiaa limesomwa au kabla ya kusomwa mahakamani na kuachana na wewe?
 
Je kabla ya hukumu kutolewa na ikathibitika kuna vielelezo au ushahidi zaidi ukasadikika kuwepo mahali fulani hakimu anaweza kutoa amri vikaletwa hivyo vielelezo. Na je mlalamikaji ana haki ya kudai vielelezo au ushahidi uletwe mahakamani?
 
Ahsante kwaelim zuri, mzidi kutuongezea mambo hata tusiye wanataaluma ya Shelia tuijue kupitia mitandao yakijamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna ukiukaji mkubwa sana wa haki za ki binadamu kutoka polisi, wengi hawachukulii maanani
 
Back
Top Bottom