Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Mahusiano kati ya mshale mwanamke na cancer mwanaume huwa vipi
 
Habari mkuu!!

Naomba kujua

Mwanaume Simba na Mwanamke ni Ng'é
Simba ni moto na Ng'e ni maji ya moto hawa ni watu wanaotamaniana haraka sana kingono lakini Simba hujikuta kwenye wakati mkuu wa tabia za ng'e kwa wivu na anavyojiweka Ng'e ni mtu wa kununa kirahisi sana na Simba ni mwenye kiburi sana, simba humuona ng'e ni mgumu kuelewa na siyo muelewa nae ng'e humuona Simba ni mwenye kujifanya anajua au anaweza na mtu ws kujionyesha, pia ng'e humuona simba ni mtu wa kupenda sana sifa na kutamani watu wa nje zaidi. Ng'e huona ni bora afanye kabisa kuliko kutamani na hiyo humuharibia kabisa hali yake Simba. Na ngono si kila kitu kwake. Hivyo couple hizi huwa sio na pia kuchanganya nyota yoyote ya maji na moto ni hatari kwa maana ipo siku ya kuumizana tu

Rakims
 
Mkuu ikitokea mwanaume mwenye nyota ya Ng'e ndo mke wake ni Mapacha ni nini kitatokea?
Ng'e huvutika sana na urembo wa mapacha siku zote na pia muonekano wa kingono wa ng'e humvutia sana mapacha, kwa kipindi fulani mapacha huvutika sana na tamaa za ng'e katika kufanya ngono, mara nyingi mapacha hupenda sana kuwa huru katika maisha yake sasa ng'e yeye hupenda kubana sana wapenzi wake na kuwahisia mabaya siku zote hili humfanya mapacha mpenda lawana kushindwa kumuelewa ng'e hawa huwa hawachelewi kila mmoja kushika njia yake,

Rakims
 
Mahusiano kati ya mshale mwanamke na cancer mwanaume huwa vipi
Ama kama kuna watu huwa wanajutia maamuzi ya ndoa au mapenzi basi huwa ni baina ya kaa na mshale hawa ukiwafikiria sana unaweza ukahisi ndio walioanzisha ule usemi wa "adui yako ni yule unalala nae kitanda kimoja" au "kosea vyote usikosee kuoa au kuolewa" au "ndoa ndoana" hapa ni sawa na kuchanganya chumvi na sukari mkuu,
Au kuchanganya malaika na shetani, au malaya na muumini,
Ukiitwa hata kusuluhisha kesi ya hawa watu utajuta, sishauri mkuu kujaribu sumu kwa kuilamba, kama huwa unasikia mwanaume anakimbizwa na boksa au mwanamke anakuwa punching bag basi changanya hawa uone, mwanzo kama malaika

Rakims

Rakims
 
mkuu vipi ndoa ya mwanaume mizani na mwanamke kaa?
 

Mkuu nakuelewa sana sana.....mkuu kwa hiyo ng’e anashauriwa aoe mke wa nyota gani?
 
Habari yako mkuu, nimevutiwa sana na maelezo yako (elimu) uliyoitoa Allah akuzidishie palipopungua inshallah. Mimi jina langu linaanzia na herufi ‘A’ nimezaliwa tar 08/08/88 katika maelezo yako upande wa tabia naona baadhi nnazo za nyota ya simba na baadhi nyota ya punda nashindwa kuelewa nifuate nyota ipi? Mfano kwenye magonjwa nasumbuliwa sana na misuli ya kichwa na kuumwa kipanda kwa maelezo yako hii ni nyota ya punda na pia nikifanya kazi ama kutembea sana huwa naumwa sana mgongo na juu ya uti wa mgongo na mabegani. Hebu nifafanulie uzuri nifuate nyota ipi ‘Simba’ au ‘Punda’?
 
Na mara nyingi nikifanya ibada nakuwa na amani ya moyo na huwa mtu mwenye matumaini sana na pia nikifululiza swala na ibada huwa sitamani kufanya tendo la ndoa kabisa, Pia nikisikiliza quran mwili wangu husisimka na huwa kama natambaliwa na mdudu ama kitu katika mwili wangu. Hebu nipe mwongozo nna nini kinanisibu? Na je kama nilivyokwambia hapo awali herufi ya kwanza ya jina langu ni ‘A’ nimezaliwa 08/08/88 mke wangu nyota yake ni ‘Mizani’ je tunaendana? Ahsante
 
Asante mkuu, hapo unatakiwa kuelewa kwamba Nyota yako ji Simba haijageuka ila ina tabia za Punda sasa ukifuatilia ambalo ni gonjwa serious au ni sehemu yako kati ya simba na punda unapata ni simba kwa maana habadiriki huyo yupo thabiti hana nyuso mbili au kigeugeu, hili nitaliongezea hapo juu kwenye thread kuelezea tabia hizo 3 za nyota ukikaa kwenye nyota yako ya Simba ukatulia hapo basi hutaziona dalili za kuwa Punda

Rakims
 
mkuu vipi ndoa ya mwanaume mizani na mwanamke kaa?
Hiyo ni bora na wanaweza kujenga familia kwa maana maji hutembea kwa upepo na upepo huanzia kwenye maji, kaa ni maji ya bahari,
Mizani ni pepo za juu

Rakims
 
Simba ni moto wa mkaa na mizani ni upepo wa juu, mke wako ni bora kwako kwa maana anakutakasa na kukusafisha na kukung'arishia rizqi wewe ni kati ya wale watakao faulu katika ile kauli ya "oeni mpate kuzidisha kipato" ndoa yenu ni nzuri mkitulia mtafika mbali kwa maana mizani ni ndugu na ng'ombe wanaishi nyumba moja ya Zuhura(sayari ya mapenzi)

Kuhusu kutembelewa na wadudu ukisoma Qur.an kwa imani mara nyingi huwa ni mashetani wanaokuzengea kwenye mwili wanaumia ndio hukimbia hivyo.

Rakims
 
Maalim samahani kwa usumbufu maana sisi wengine ndio tunachota elmu na Allah anasema “mbora wenu ni yule mwenye kujifundisha na akafundisha elmu” Mfano mimi binafsi nishaijua nyota yangu sifa zake na tabia yake, sasa nataka ‘niing’arishe’ kama wengine wanavyosema nitumie njia gani au nifuate taratibu zipi pasipo kwenda kwa mtaalamu ‘mnajimu’ yaani mimi binafsi nifanye vitu gani ili nyota yangu ing’ae? Nawasilisha.
 
Ok.
 
Mkuu Rakims, je nyota ya Ng'ombe(mwanaume) na kaa(mwanamke mkubwa kidogo)
Je hawa watu wanaweza kua pamoja na wakakaa vizuri,naomba ufafanuzi maana bado sijapata majibu sahihi huko juu.
Vipi mkuu amekujibu private nini.
Kama kakujibu nipe mrejesho maana hii kama umenilenga yani
Rakims pita hapa tafadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…