Ijue Mitandao/Tovuti Jamii

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM

Miaka michache iliyopita kulikuwa na kitu kimoja ambacho vijana wengi sana walipenda kufanya nacho ni kutafuta marafiki kwa njia ya mtandao wengi wao wakiwa mbele ya komputa zao hata unapoenda kwenye migahawa ya mitandao wengi walikuwa wanatafuta marafiki na huduma zingine za kuwasiliana na dunia ya nje .

Wakati huo mitandao mbalimbali ilitengeneza pesa na kupata faida kubwa kwa ajili ya kukutanisha watu mbalimbali wengi walitakiwa kujiunga ili kuweza kupata fursa zingine kama kuona picha na zingine nyingi kwa kuangalia sifa za mtu anayemtaka yeye .

Hivi sasa mitandao hiyo iliyokuwa inaendesha huduma za kuunganisha watu marafiki na kupata huduma zingine karibu yote inaelekea ukingoni katika hatua za mwisho mwisho na hii imetokana na ukuaji wa kasi wa tovuti za jamii ambapo mtu anaweza kupata huduma hizi bure kwa kujiunga tu na kuanza kutafuta anachotaka yeye .

Tovuti au mitandao jamii ni ile mitandao inayomruhusu mtu kuwasiliana na mwenzake au wenzake kwa njia ya mtandao katika kubadilishana habari , kuongea na vitu vingine mbalimbali mitandao hii mingi ya jamii mingi iko kwa lugha ya kiingereza na inatumia sheria na miongozo ya nchi nyingi za ulaya haswa zile sehemu ambazo zinawateja wengi zaidi .

Baadhi ya mitandao hii kwa majina ni kama Blogger, LiveJournal, Open Diary, TypePad, WordPress, Vox, ExpressionEngine, Xanga,FMyLife, Jaiku, Plurk, Twitter, Tumblr, Posterous, Yammer, Qaiku,Facebook, Geni.com, Hi5, LinkedIn, MySpace, Ning, Orkut, Skyrock, Qzone, Vkontakte, RenRen, Kaixin, ASmallWorld, studivz, Xing, RunAlong.se, Bebo, BigTent, Elgg, Hyves, Flirtomatic,NutshellMail, FriendFeed,dillidost.com .

Kumbuka sio yote iko kwa ajili ya marafiki pekee kuna kazi mbalimbali za mitandao jamii lakini yote hii lengo lake ni katika kuhabarisha watu mbalimbali mengine inaendeshwa na mtu mmoja mmoja mengine ni kampuni na zingine ni vyama makundi yenye itikadi mbalimbali .


Mitandao hii haichagui kabila dini wala rangi ya mtu unachotakiwa ni kujua lugha iliyoandikwa kwenye kurasa za mitandao hiyo na kufuata sheria na miongozo mengine ambayo iko ndani ya mtandao hiyo ambayo iko sehemu nyingi za maisha ya mwanadamu .

Lakini unapaswa kukumbuka kwamba kuna ambayo pia inaendeshwa kwa misingi maalumu ambavyo mara nyingi ni ya siri kwa ajili ya maslahi ya baadhi ya jamii na nchi duniani mfano ukitembelea baadhi ya mitandao jamii ya uchina kuna baadhi ya vitu huwezi kuvikuta kwa uwazi kama ilivyo ile ya nchi za magharibi .

Kutokana na kukutanisha watu wa aina mbalimbali kwenye kubadilishana mawazo au hata wengine kuunda vikundi vyao ndani ya mitandao hiyo kwa sasa imeanza kutishia hali ya utulivu katika baadhi ya maeneo duniani ambapo tovuti na mitandao hiyo inaangaliwa .

Katika eneo moja nchini nigeria linalotawaliwa na sheria za kiisilamu viongozi wa eneo hilo liliamuru kampuni za utoaji wa huduma za mtandao kufungia baadhi ya mitandao ambayo ilikuwa na maneno ambayo hayaendani na utamaduni wao , hali kama hii ilitokea pia nchini Pakistani ambapo walifanya hivyo hivyo tofauti yake ni kwamba nchini Pakistani waliamua kufanya hivyo kutokana na shindano moja lililoendeshwa na kikundi Fulani ndani ya mtandao huo wa jamii unaoitwa facebook .

Kuna matukio mengine mfano kuna kijana mmoja huko nchini uingereza alimwagiwa tindikali baada ya kubainika kutembea na mke wa mtu ambaye alikutana nae kwenye mtandao mmoja wa jamii , kuna kijana mwingine mwenye asili ya Tanzania nchini uingereza nae alichomwa na kisu akapoteza maisha yake baada ya kutokea mabishano kati yake na mwingine kwenye mtandao jamii .

Bila kusahau matapeli wa mtandao nao wamegeukia sana kwenye mitandao jamii sikuhizi kwa kutumia majina bandia na mengine ya jinsia tofauti kwa ajili ya kutafuta marafiki na wetu wengine ambao wanaweza kuwalaghai kwa njia mbalimbali , kutokana na hili baadhi ya mitandao jamii imewahi kufunga baadhi ya anuani za watumiaji wa mitandao hiyo kwenye baadhi ya majimbo nchini Nigeria manake walikuwa wanasumbua sana baadhi ya watu

Pamoja na kasheshe hizo ambazo kukumba baadhi ya maeneo na watu bado mitandao hii imefanikiwa kufanya dunia ya mawasiliano kuwa endelevu na kupata maendeleo kwa baadhi ya watu na vikundi vyao kwenye mitandao hiyo duniani kote .

Kampuni nyingi kubwa duniani sasa hivi zinakurasa zake kwenye mitandao hii jamii kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wao na wapenzi wengine wa bidhaa zao maana yake kampuni hizi zinaweza kuwa karibu zaidi na wateja wao kuliko wakati mwingine wowote katika maisha ya wanadamu .

Sio hayo ya kampuni kubwa tu hata baadhi ya watu maarufu au hata wale wasio maarufu wamegeukia zaidi kwenye mitandao jamii katika kuwasiliana na watu wao wa karibu au kutafuta marafiki na aina nyingine za ushirikiano na watu mbalimbali duniani ambao wanafanya mambo ambayo yanafanana nao na mengi kama hayo .

Mfano raisi wa sasa wa marekani alitumia mtandao kama facebook sana kwenye kampuni zake za uraisi kuwasiliana na wananchi wake kwa urahisi zaidi na kwa siku za karibu viongozi wengi duniani nao wamefungua kurasa kwenye mitandao hii jamii kwa ajili ya kuwasiliana na wananchi wao kupata maoni na kutoa aina nyingi za maoni yao binafsi au kuwakilisha wananchi wao .

Hali hii ya kuwasiliana na wananchi kama raisi wa marekani aliavyofanya imekuwa tofauti sana kwa baadhi ya jamii haswa zile zinazoendelea kama afrika na maeneo mengine ambayo wananchi wake wengi hawana uwezo wa kuwa hata na simu ya mkono , hawajaunganishwa na mitandao na hata elimu ya masuala mengi ya mitandao kwao ni ndogo kwahiyo imekuwa pigo kwa upande mmoja kwa nchi hizi za kiafrika na jamii zake .

Lakini kumekuwa na tuhuma mbalimbali kwamba mitandao hii inawezekana inaendeshwa na baadhi ya mashirika ya ujasusi duniani kwa ajili ya kutafuta watuhumiwa na taarifa zingine za watu mbalimbali mbali duniani haswa walio nje ya mipaka ya nchi hiyo .

Hii ni kutokana na kwamba sasa mashirika hayo ya ujasusi au kampuni zingine kubwa zinaweza kupata taarifa za watu ambao wameamua kuziweka huko kwa hiari yao wenyewe bila kulazimishwa na inakuwa rahisi kutafuta taarifa zingine za watu kwenye mtandao hiyo kama anawasiliana na nani , rafiki zake na mawazo yake mengine anayoyatoa kwenye mada na majadiliano mengine yanayoendelea kwenye mitandao hiyo .

Kuna watu kwa maelfu na mamia wanasafiri ulimwenguni kila siku watu hawa taarifa zao na picha zao zingine hupenda kuziweka kwenye mitandao jamii kwa ajili ya watu kuangalia wale wanaowasiliana nao au kama wako kwenye miradi basi watatengeneza kurasa ya mitadi wao kwenye kurasa za mitandao hii

Kumbuka mitandao mingi duniani inauwezo wa kuangaliwa kwa njia ya simu ya mkono na vyombo vingine vidogo vya mawasiliano pamoja na kuangaliwa pia unaweza kuhamisha picha na kufanya mazungumzo na watu wengine mbalimbali toka kwenye simu yako ya mkono .

Hii ina maanisha kampuni zinazotangaza bidhaa zao Fulani zinauwezo wa kutangaza kwa lugha mbalimbali kutumia mitandao hiyo kutokana na mtu anapotoka au anapoangalilia mtandao huo mpaka kwenye simu zao za mikono na vifaa vingine vya mawasiliano vyenye uwezo wa kufungua kurasa za mitandao hii .

Kwa jinsi binadamu wanavyozidi kuwa karibu zaidi kwa njia ya mtandao na ndio tekinologia mbalimbali za kurahisisha mawasiliano kati ya watu na wa maeneo mengine dunia zinavyozidi kukuwa zaidi ingawa kuna matatizo kidogo ambayo yamewahi kutokea kati ya jamii zingine kwenye mitandao hiyo .

Baadhi ya matatizo haya moja ni kuhusu kutoa habari na taarifa zingine nyeti kwa haraka zaidi ambapo hazihitaji kuhaririwa na ni bure tofauti na magazeti na majarida mengine ya habari duniani .

Baadhi ya mitandao inaendeshwa kwa kufuata sheria na kanuni za nchi ambazo zinapingana na nyingine katika mambo Fulani Fulani haswa ya uhuru wa habari kama nilivyoelezea huko juu kuhusu uchina na nchi kama irani na sehemu zingine duniani .

Mitandao mingi ya jamii haina huduma za kutafsiri lugha hii inawapa shida baadhi ya watu katika kujiunga na mitandao hiyo au hata kuweza kuelewa baadhi ya kanuni na sheria za mitandao hiyo haswa kwa watoto wadogo ambayo ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa mambo mabaya yanayoendelea kwenye mitandao hii jamii .

Pia kampuni zinazoendesha au kumiliki mitandao hii haijawa wazi zaidi kwa watumiaji wa mitandao hii kuhusu taarifa zao ambazo ziko kwenye mitandao hiyo jinsi vinavyotumika na watu wengine au vyombo vingine duniani .

Hayo niliyoandika hapo juu na mengine mengi zaidi tutakuja kujadili jumapili hii kuanzia saa 3 kamili asubuhi kwenye kipindi cha ULIMWENGU WA TEKNOHAMA katika MORNING STAR FM 105.3 ya Jijini Dar es salaam , Karibu kwa mazungumzo ya moja kwa moja , maswali . maoni na fursa zingine za kujifunza masuala mbalimbali ya kiteknohama .

SOMA ZAIDI
· Benkler, Yochai (2006). The Wealth of Networks. New Haven: Yale University Press
· Gentle, Anne (2009). [ISBN 978-0-9822191-1-9 Conversation and Community: The Social Web for Documentation]. Fort Collins: XML Press. ISBN 978-0-9822191-1-9.
· Johnson, Steven (2005). Everything Bad is Good for You: How Today’s Popular Culture Is Actually Making Us Smarter. New York: Riverhead Books
· Surowiecki, James (2005). The Wisdom of Crowds. New York: Anchor Books
· Kaplan Andreas M., Haenlein Michael, (2010)., Users of the world, unite! The challenges and opportunities of social media, Business Horizons, Vol. 53, Issue 1, p. 59-68.
· Golder, Scott; Huberman, Bernardo A. (2006). "Usage Patterns of Collaborative Tagging Systems". Journal of Information Science 32 (2): 198–208.

YONA FARES MARO
DAR ES SALAAM
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
 
Back
Top Bottom