Ijue Menopause ya wanaume: (chanzo na suluhisho).

Ijue Menopause ya wanaume: (chanzo na suluhisho).

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,140
Reaction score
10,857
Menopause ya wanaume ama kama inavyoitwa kitaalam, ANDROPAUSE inatokana na mabadiliko ya viwango vya homoni kunakotokana na mabadiliko ya umri wa mwanaume. Hii hupelekea kushuka kwa uzalishaji wa homoni ya testosterone katika makende haswa kwa wanaume wenye miaka 50 na zaidi.

Menopause ya wanaume inaweza kusababisha matatizo ya kimwili, tendo la ndoa na kisaikolojia kadiri mwanaume anavyokua. Kwa mfano:

- Upungufu wa nguvu za mwili.

- Msongo wa mawazo au kuwa na sura ya huzuni

- Kukosa bashasha

- Kutojiamini

- Kukosa umakini wa kazi

- Kukosa usingizi vizuri (insomnia)

- Kuongezeka mafuta mwilini

- Kuongezeka ukubwa wa matiti
Mifupa kupungua ukubwa

- Kushindwa kusimamisha uume vizuri/Uume legelege

- Hamu ya ngono kupungua (nyege)

- Kushindwa kumzalisha mwanamke.

- Kupungua ukubwa wa mapumbu. Kunyonyoka nywele

TIBA:

KULA MLO KAMILI.
Haswa vyakula vyenye mchanganyiko wa mbegumbegu (maboga, karanga na ufuta), Matunda (tikiti, machungwa,straw berry na ndizi mbivu na parachichi), Mbogamboga (Karoti, saladi, spinachi), Yogurt. Mafuta ya zeituni, Vyakula vyenye madini ya zinc na magnesium.

FANYA MAZOEZI YA KIASI MARA KWA MARA.

PATA USINGIZI KWA KUTOSHA.

EPUKA MSONGO WA MAWAZO.

KUNYWA KIASI KIDOGO CHA POMBE HASWA REDI WINE (kama wewe ni mnywaji).

PATA USHAURI WA DAKTARI
(tiba za kitaalam itakapobidi.)

Hata hivyo elewa, kadri unavyokua kiumri, hutarudi kuwa kama kijana mdogo, this is the hard fact.
 
Mada murua hasa kwa wazee.
Umesahau kidogo; madhara mengine ni tezi dume kutokana na kupungua elasticity ya prostate gland pouch .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom