Ijue MECCO ya Mbeya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,203
157,376
MECCO SPORTS CLUB MBEYA 1989. Uwanja wa Taifa Dar vs SSC : Matokeo SSC 1 - 1 MECCO.
Kuanzia Kulia kwenda kushoto.
Saidi Maeda (Team Manager), Saidi Jobe (Kocha Msaidizi), Gabriel Mwitika (Mlinzi kushoto), Rashidi Mandanje (mlinzi kulia), Goari Gama (mlinzi kulia),Betwel Africa (mshambuliaji/kati), John Moses Kanyiki (kiungo mshambuliaji),Ephraim Kayeta (mshambuliaji), Nasibu Abasi (winga kushoto), Jafari Nyoni (kiungo), Danford Ngesi ((kiungo/ mlinzi),George Mangula (Kipa),Nurdin Kasabalala (mlinzi/kulia), Venny Simon ( mlinzi/kati), Charles Makwaza ( mlinzi/kati), Mbaga Mwantiku (mlinzi)Juma Ahmed (Kipa) na Abeidi Kasabalala (winga/kulia.

16939604_1785067141518751_641148398596626718_n.jpg
 
Majimaji ilikuwa tamu ni ya miaka ya 80 katikati hiyo ya kina selestine (sikinde )mbunga kina Peter mhina ulikuwa mkoba huu nyanda isihaka majaliwa beki Abdul ntila na swamli ayubu (beki mstaarabu octovean mrope akina hamza maneno na dadi phares walikuja baadae
Kule tulikua na Ushirika, na CDA Dodoma.
 
Aisee kuna Mecco ya Nyakato Mwanza,sijui yenyewe vipi,wajuzi?
Mecco (ambayo ndio waliokuwa wamiliki wa team ya mecco) ilikuwa kampuni ya ujenzi ya serikali ambayo makao makuu yake yalikuwa mbeya.Miaka ya mwanzoni mwa themanini walikuwa wanajenga barabara za mwanza,kuanzia buzuruga stand hadi buzuruga shuleni, mpaka nyakato sokoni.Na kambi yao ilikuwa hapo nyakato (mecco) .Hivyo jina la mecco lilitokana na kambi ya hii kampuni ya ujenzi.
 
Usisahau Pamba ya Mwanza.
na Toto Africans,hahhaa Pamba imeshindwa kabisa
Pamba ya Mwanza ilitoka kushinda 12 na ile Timu ya shelisheli ilipoenda Mbeya na Mecco walifungwa 3 kwa moja mechi za mwisho mwisho wakina marsha kabla ya kwenda Simba..kipindi hicho kulikua na Mpira
nasikia kuna kipindi Pamba iliwahi kuwa kali kuliko Simba,au stori tu za wadau wa Pamba?
 
Nimesoma Nundu,nilikuwa napita hiyo barabara kila siku( hiyo barabara nimetembea KM nyingi kuliko zote duniani) lkn sikuwahi kujua the story behind,live long JF
 
na Toto Africans,hahhaa Pamba imeshindwa kabisa

nasikia kuna kipindi Pamba iliwahi kuwa kali kuliko Simba,au stori tu za wadau wa Pamba?
Pamba ilikuwa kiboko mkuu, walikuwepo watu kutoka morogoro Reli hiyo kiboko ya vigogo, bila kuisahau ushirika ya moshi, milambo ya tabora, timu za mashirika zilikufa na mashirika yake, RTC kigoma, RTC shinyanga, ujenzi rukwa, CDA Dodoma
 
Do Reli ya Morogoro niliisahau asante mkuu.
 
Pamba ya Mwanza ilitoka kushinda 12 na ile Timu ya shelisheli ilipoenda Mbeya na Mecco walifungwa 3 kwa moja mechi za mwisho mwisho wakina marsha kabla ya kwenda Simba..kipindi hicho kulikua na Mpira
Asante kwa kumbukumbu nzuri. TFF hawana records, poor them.
Nataka nitengeneza database archive ya soka LA Bongo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom