Nazikumbuka Tukuyu star na MECCO za Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nazikumbuka Tukuyu star na MECCO za Mbeya

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Sep 19, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hizi ni timu ambazo sitaweza kuuzisahau kamwe katika maisha Yanga kutoka na style yake ya uchezaji na aina ya wachezaji waliokua wakiziwakilisha.Naizungumzia tukuyu star ilipanda daraja mwaka 1986 na kwenda straight kuchukua ubingwa wa tanzania bara wakiziacha simba na yanga zikishangaa shangaa na pia MECCO iliyopanda daraja mwanzoni mwa miaka ya 90 na kuleta changamoto kubwa kwenye mpira wa tanzania kiasi cha kuzitia hofu simba na yanga na mashabiki wao kudhani kwamba timu hiyo wachezaji wake hawakua wa kawaida bali wanatumia madawa ya kuongeza nguvu kutokana na kuwa na stamina ya kutosha hata dakika 180 bila kuchoka.

  Hii ndiyo Tukuyu Star ya mwaka 1986 ambayo ilitwa uchampioni tanzania bara mwaka huo huo iliyopanda daraja:

  1:Mbwana Makatta

  2:Ally Kimwaga

  3:Michael Kidulu

  4:Godwin Aswile

  5:Selemani Mathew

  6:Aston Pardon

  7:Justine Mtekele

  8:Karabi Mrisho

  9:Richard Lumumba

  10:peter Mwakibibi

  11:Kelvin Haule

  Benchi:

  Fadhili Emba-goal keeper

  John Alex

  Yusuf kamba


  MECCO 1990'S

  1:George Mangula

  2:Rashid Mandaje

  3:Gabriel Mwitika

  4:Mbaga Mwintinku

  5:Charles Makwaza

  6:Danford Ngessi

  7:Abed Kasabalala

  8:John Moses Kanyiki

  9:Betwel Afrika

  10:Ephraim Kayetta

  11:Nassib Abbas

  Reserve:

  Juma Ahmadi-Goal Keeper

  Nurdin Kasabalala

  Jaffar Nyoni

  Idd Mzomwe

  Augustino Sanga  Vipi vikosi vingine unavyovikumbuka wewe enzi hizi za 1985-1990's,najua wapo watu wa Dodoma humu hapo kulikua na CDA,SONGEA kulikua na majimaji,Arusha kulikua na NDOVU ya huko,MOSHI-USHIRIKA MOSHI,DAR ukiacha SIMBA na YANGA kulikua na PILSNER na SIGARA,MWANZA kulikua na PAMBA na BIASHARA MWANZA,SHINYANGA kulikua na BIASHARA SHINYANGA,KAGERA na KIGOMA zilikuwepo RTC za Huko,Tanga COASTAL UNION na Baadae AFRICAN SPORTS n.k. kama una kumbu kumbu mwaga vikosi vya timu hizo.Hii ni maalum kwa watu wa mpira wenye umri wa miaka 35 na kuendelea...yani karibu kila mkoa kulikua na timu na ligi ilikua ndefu mno kama ya Uingereza,ilichezwa almost mwaka mzima
   
 2. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee asante kwa kutukumbusha mambo ya zamani ,lile lilikua soka haswa ,wale wachezaji walikua wanakipiga haswa.Haya enzi zetu zimepita sasa tuwaone watoto na wajukuu wetu wanalofanya.
   
 3. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Duh mkuu safi sana, umenikumbusha mbali sana. Hizi zilikuwa timu bana, nakumbuka jamaa kuna wakati walikuwa wanaachwa Uyole then kocha anawaambia wakutane Sokoine uwanjani na players wanatoka baruti na wakifika pale sokoine wanapigishwa ngazi- juu chini uwanja mzima !! Wakati mwingine baada ya mazoezi wanaambiwa tukutane tena Uyole !!

  Wamevuruga sana milimani kwa matizi ya panda -shuka !!

  Pumzi hasa ya Mecco ilikuwa balaa, dk ya 1 hadi 90 wanakimbia kama wehu wakati timu nyingine hoi !! Waulize Simba na Yanga hata pale taifa ilikuwa shughuli..!!
   
 4. R

  RON PAUL Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mkuu kim kama hukua mchezaji wa moja ya hizi timu ntashangaa sana..lol unakumbukumbu za ajabu sana aisee,mimi nawakumbuka baadhi tu ya wachezaji kaka african sports kulikua na kina kulwa shaban mchezaji mrefu kupita wote kupata kutoakea bongo,juma burhani,victor mkanwa alikua anafunga sana,Abas mchemba huyu alikua anawafunga simba tu sijui kwa nini,ukija mwanza pamba nawakumbuka kina kitwana seleman,hamza mponda,Hussein marsha,George masatu,Fumo Felician,Nyota nyekundu sitamsahau kamwe mchezaji mkorofi cheupe ROSTA NDUNGURU,Frank Kasanga Bwalya "chapombe",Faustin Kibingwa,Mohammed Mgalike n.k.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah mimi LIPULI NA RELI WADAU,NAZIMISS SANA
   
 6. R

  RON PAUL Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  zama hizo zilizotajwa na mleta mada lipuli ilikua hata haijulikani,labda reli ya kina Duncun Butinini,Gasper Lupindo,Fikiri Magoso n.k. hiyo ndio Reli kiboko ya vigogo,simba na yanga walikua hawatoki morogoro na lazima vurugu zitokee
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Mabingwa wa ligi kuu ta Tanzania Bara(siku hizi vodacom) 1986
   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  tukuyu stars a.k.a. banyambala
   
 9. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unakumbuka bandari ya mtwara ? Marehemu chuma ? Na yule bulji vipi?hebu tujulisheni
   
 10. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu hakika wewe una kumbukumbu kali sana. Ila nakumbuka tukuyu walikuwa na mshambuliaji wao hatari aliyekuwa mrefu mithili ya Rashid Yekin wa Nigeria alikuwa anaitwa Jimmy Moredi. Au huyu alikuwa bado kipindi hicho?
   
 11. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyo Godwin Aswile akikukamia ujue siku hiyo hufurukuti maana alikuwa anahakikisha kuwa wewe hupewi pasi wala yeye haombi mpira hivyo wote hamsikiki siku hiyo.
   
 12. g

  gutierez JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  rtc kigoma,rtc/biashara shinyanga,katavi mpanda,ujenzi rukwa,zimanimoto walikuwa wanacheza mechi zao songea tu,away hawaendi uhaba wa nauli,waziri mkuu dodoma,ushirika moshi,ndovu arusha,coastal union na african sport tanga na zingine nyingi tu ntamalizia kesho nawahi ndondo muda huu mbagala kiburugwa kwahereni
   
 13. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Dah, umenikumbusha mbali sana,kuna mchezaji Mecco alikua bench anaitwa Jordan Namajojo,kila Mecco wakienda mpirani lazima anitafute nikaingie uwanjani na timu bure.
  Baada ya mdau kumtaja Fikiri Magoso, nimemkumbuka Costa Magoroso, walikua wananichanganya majina.
  Namkumbuka pia Athanas Michael.Ila funga kazi ilikua mechi ya simba na nyota nyekundu,walikua wakikutana Rosta Ndunguru na Twaha Hamidu, palikua panachimbika.Enzi hizo mpira ni kusikiliza redioni tu.Redio Tanzania Dar es salaam Idhaa ya Taifa.
  Watangazaji, Omay Jongo,Ahmed Jongo,Charles Hilary ...n.k.
   
 14. M

  MAFUNZO Member

  #14
  Nov 16, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 13
  Enzi hizo Fumo alikuwa anachezea Biashara Mwanza.....baba yake wlikuwa shabiki mkubwa wa Yanga. Kila yanga wakija kanda ya ziwa alikuwa anawafadhili sana. Sasa machungu yake yalikuwa ni kwa mwanaye Fumo...kwani kila mechi alikuwa lazima awalambe Yanga. Kafanya hivyo biashara na hata alipoamia Pamba.
  Mwishowe ili kuleta amani na mzee wake aliamua kusajiliwa na Yanga. Mwanza ........ilikuwa kiboko ya Yanga na simba. Manake Wazenji walituzimia umeme ligi ya Muungano...zikiwa zimesalia dakika chache Pamba kuwa bingwa........
   
 15. t

  testa JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2014
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu hii kumbukumbu imenikosha sana,ubarikiwe
   
 16. abbaczo

  abbaczo JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2014
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,557
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Dah hu uzi umenipa raha katika timu ya mecco hapo ktk reserve mmojawapo is my late father jaffar nyoni. R.i.p father, we still remember you
   
 17. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2016
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  kumbukizi mujaarab
   
 18. D

  Danny greeny JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2016
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 3,722
  Likes Received: 913
  Trophy Points: 280
  Umesahau kukamilisha historia mkuu. Tukuyu stars ndio timu pekee iliyoweka historia ya kipekee na kichekesho tangu soka lianze enzi za Tanganyika. Ni timu pekee iliyopanda daraja na kuchukua ubingwa na msimu uliofuatia kuonyesha wao ndio wababe wa soka wakashuka daraja na kuweka historia ya bingwa mtetezi kushuka daraja
   
 19. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2016
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  NIKUMBUSHENI JINA LA UTANI LA MECCO
   
 20. K

  Kataa Rushwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2016
  Joined: May 15, 2015
  Messages: 563
  Likes Received: 447
  Trophy Points: 80
  Rosta Ndungur mashine kutoka Mbinga hii Ana mtoto wake anapiga Sana mpira Yuko Songea anaitwa Candy kwa sasa sijui kama anachezea timu gani au anaendelea kupiga debe
   
Loading...