Nabi aanze na muunganiko upi hapa?

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Nabi Nesreddine kupangua safu yake ya kiungo na ushambuliaji kwa ujio wa Chicco Ushindi wa Kubanza?

Chicco ni winga mwenye uwezo wa kucheza wings zote kwa uwezo mzuri tu ma ndio maana alikuwa tegemeo TP Mazembe na timu ya taifa lake, DR Congo.

Ana uwezo mzuri kutumia miguu yote miwili hali inayomfanya kutumika wings zote kwenye attacking patterns.

Kiasilia alianza kucheza kama mlinzi wa kushoto kabla ya kupanda juu na kucheza kama kiungo mshambuliaji wa pembeni.

Eneo la kiungo la Yanga, lina wachezaji wengi kwa sasa wasioachana sana kwa ubora wao na kila mmoja ana kitu chake cha kipekee kwenye note book ya Nabi Nasreddine kocha mkuu Yanga SC.

Saido Ntibansonkiza mchezaji mkongwe kabisa ndani ya kikosi cha Nabi. Ana uwezo wa kucheza kama winga wa kushoto au playmaker eneo la kati. Ana technical ability kubwa na uzoefu kuliko mchezaji yoyote kwenye kikosi cha Yanga . Ana jicho la kipekee kubadili mfumo wa kushambulia pale plan A inapofeli na mara nyingi ndio key player wa mwalimu Nabi ndani ya uwanja kusoma pattern za mpinzani katika kushambulia na kujilinda. Mainly kwa Saido unapata ; Technical ability, Vision ya kuusoma mchezo kama playmaker, second attacker invisibly kwenye attacking zone . Key master wa set pieces. Si mzuri kwenye kusaidia kukaba , ila anaficha udhaifu wake huo kutokana na uwezo wa kumiliki mpira na kutunza tempo ya game kwenye sets za kushambulia.

Jesus Moloko: Huyu ni winga wa kulia ambaye ana uwezo mzuri kusaidia cut-backs kwenye offensive patterns . Ana kasi na nguvu kutunza tempo ya mchezo kwenye kushambulia. Bado ana changamoto ya kutunza perfomance yake hususani kwenye viwanja vyenye pitch mbovu. Faida kubwa ya Moloko kwenye note book ya Nabi, ni uwezo wa kuingia na kutoka eneo la kati kwenye deception plan ya kuunda shambulizi la upande linaloingia na kutoa kwenye midfield zone ( prompt-flank attack )

Farid Mussa: winga mwenye uwezo wa kucheza pande zote . Sifa yake kubwa ni kasi kwenye dribbling na krosi zenye macho chini na juu. Ana changamoto kubwa kutunza ubora wake hali inayomfanya kuwa chaguo namba mbili kwa Nabi.

Denis Nkane: huyu ni mpya kwenye kikosi cha Yanga akitoke Biashara United. Kijana mdogo mwenye kiu ya maendeleo. Nkane ana kasi sana kwenye wing na uwezo wa kufunga . Kasi yake ni faida kwenye mpango wa kuirudisha nyuma safu ya ulinzi ya mpinzani kuua mtego wa kuotea na kufanya merging ya kiungo na walinzi wa kati ili kuwatoa kwenye uwezo wa kwenda mbele wakiwa kwenye umbo zuri. Umbo lake ni changamoto sana. Ni mdogo na bado stamina si kubwa hali inayomfanya kuchezewa rafu nyingi. Si msaada sana kwenye kuingia na kutoka eneo la kati . Anahitaji space kufunga au kuchezesha timu.

Balama Mapinduzi: Ametoka majeruhi ya muda mrefu na amerudi uwanjani na ubora wake . Huyu ana uwezo wa kucheza pembeni kama winga na kiungo wa juu kama mchezeshaji pia second striker. Ana uwezo mzuri wa passing, dribbling , holding na ku-open-up tight marking zone za wapinzani kutokana agility yake kimbinu.

Feisal Salum: Key player kwenye central midfield na attacking zone . Anacheza kama kiungo mkabaji na mshambuliaji, second striker na playmaker kwenye attacking zone. Kwenye high pressing, Feisal ndio key player akitengeneza pattern na viungo wa chini na safu ya ushambuliaji. Ana uwezo kusimamia mfumo wa kujilinda unaoanzia kwenye eneo la mpinzani pia kutunza direct pay kwenye lane ya kati. Typical box to box midfielder mwenye uwezo pia kusimama kama attacking mid. Akichoka huitoa timu kwenye direct play kwa kupiga sana square passes.

Khalid Aucho: Ndio kiranja mkuu kwenye eneo la kiungo la Yanga SC . Nabi humtumia kama kiungo mwenye jukumu la kutunza mfumo wake wa kushambulia. Timu inapocheza 4-2-3-1, yeye ndio mwenye jukumu kuhakikisha safu ya juu ya kiungo inahakikisha timu inaingia kwenye box la mpinzani ikiwa na umbo zuri la kushambulia. Lakini pia ndio mchezaji aliyepo eneo la kati kufanya disrupting na blocking kuwakataa wapinzani kufanya build up ya shambulizi kupitia kati. Unaweza jiuliza tofauti yake na Feisal ni nini? Huyu ndio huhakikisha waliopo juu akiwepo Feisal wanakwenda vyema mipango yao lakini husogea juu endapo puncturing ya defence itafanyika kwenye direct play.

Zawadi Mauya: Typical deep lying holding midfielder. Hakuwa vyema hapo mwanzo hususani kwenye passing na 1v1 duelling. Hivi sasa ameimarika vyema kiasi cha kutengeneza muunganiko mzuri kiuchezaji na Aucho. Bado ana tatizo la piercing kwenye solid defence hali inayomfanya kupiga back passes nyingi . Akiweza kuwa na uwezo mkubwa wa kupenya katikati ya msitu wa wapinzani, anaweza kuwa bora zaidi.

Mukoko Tonombe: Kabla ya ujio wa Aucho huyu ndio alikuwa key player kwenye safu ya kiungo cha chini na juu. Mukoko ni mzuri kwenye kukaba, kusaidia kushambulia kutokana na uwezo wake wa pasi ndefu pia hufunga . Amegeuka chaguo namba tatu kwa Nabi kwakuwa ameshindwa kuingia kwa haraka kwenye approach ya Nabi. Nabi anatumia sana mid and standard blocking approach inayomtaka mchezaji kuwa na uwezo mzuri wa kukaa na mpira, kutoa pasi za mbele zenye macho , kutobutu kama bado timu haijaingiza watu wengi kwenye box la mpinzani. Tonombe si calm kwenye patterns hizo. Mwepesi kuachia pasi au shuti kabla timu haijatengeneza numerical superiority. Kitu hicho kinamfanya Nabi kumweka chaguo namba tatu .

Salum Aboubacary : Wenyewe wanapenda kumwita Sure Boy. Ingizo jipya kutoka Azam FC . Ukimuondoa Saido na Aucho , huyu anafuata kwa ubora wa kucheza timu eneo la kati . Ana passing accuracy nzuri sana . Ni kiungo mzuri kwenye mifumo yote mipana ambayo inaundwa na TRIANGULAR MIDFIELD . Yaani unakuwa na na viungo wakabaji wawili kwenye box na juu yao amasimama kiungo mchezaji mwenye uwezo wa kucheza timu deep kama huyu . Nabi amepata mtu wa kumtumia aidha kwenye 4-2-3-1 , 4-2-4 au 4-3-3 . Ana tatizo la kuchoka haraka akikosa back nzuri kwenye marking.

Yanick Bangala : Huyu ni kiraka ambaye Nabi humtumia kama mlinzi wa kati na kiungo wa chini. Naweza sema ndio injini ya Nabi kwenye mbinu zake za ulinzi . Ana akili kubwa sana kunusa hatari na kuiondoa pia kutunza umbo la timu kwenye marking . True definition of versatile player in high and mid blocking approach .

Deus Kaseke: Chaguo la nne kwenye eneo la midfield kwa sasa. Ana uwezo wa kucheza kama winga kulia au kushoto na inside 10 kwenye box la juu. Ana uwezo mzuri wa kukaba na kupiga pasi ndefu ingawa hivi sasa quality yake imeshuka kwenye uwezo wa kufunga na utulivu wa kucheza kama playmaker .

Crispin Ngushi: Unaweza kumtumia kama mshambuliaji wa kati au kiungo mshambuliaji wa pembeni. Mchezaji mpya kutoka Mbeya kwanza. Ana nguvu na uwezo mzuri kushambulia kutokea kati na pembeni . Analeta challenge kwa Fiston Mayele na Makambo eneo la kati lakini pia kwa viungo wa pembeni hususani akipangwa wingi ya kulia.

Nimechambua Samue Samuel , sasa nyinyi msaidieni Nabi kupata mseto mzuri wa kikosi cha kwanza hususani eneo hili la kiungo.

NB: “ changamoto zako za maisha zisikufanye utukuze mafanikio ya wengine. Kila jasho livujalo kwa haki na malengo, Mungu huweka baraka ya mafanikio “ - Ken Saro-Wiwa, mmoja wa waandishi maarufu waliowahi kutokea Nigeria na Afrika kwa ujumla. RIP
 
Kama ningekuwa Nabi ningetumia 3-5-2.

Back 3 yangu ingekuwa Mwamnyeto,Job na Bacca.

Shabaan Djuma na Yassin wangekua 'wing back'

Khalid Aucho deep lying mid.

Holding Mid angecheza Yanick Bangala.

Ntibazokiza CAM.

Fei Toto angecheza nyuma ya FKM.

Hapo vipi.
 
Sisi Utopolo tunavyowaza Tunajijua Wenyewe.....! Hapa Bado Jivuno Letu ni Lile lile....Mabingwa Wa Historia...!
 
Kama ningekuwa Nabi ningetumia 3-5-2.

Back 3 yangu ingekuwa Mwamnyeto,Job na Bacca.

Shabaan Djuma na Yassin wangekua 'wing back'

Khalid Aucho deep lying mid.

Holding Mid angecheza Yanick Bangala.

Ntibazokiza CAM.

Fei Toto angecheza nyuma ya FKM.

Hapo vipi.
Hii naiunga mkono.
 
Uzi mreeeeeful!! Mnatumia muda mwingi kukaa humu jf kuandika matope huku mnasahau kuwa msimu wa mvua umeanza.. badala muende pale kilingeni kwenu mkatengeneze matuta ya kukinga maji yasiingie mjengoni nyie mnaendelea kudanganyana humu..
 
Hii Yanga itakutwanga nyingi tu usipokuwa makini
Dah! Hii Yanga inaogopesha aisee!!! Yaani viungo wote ni wa level ya Kimataifa! Yaani viungo wote wanachezea/wameshawahi kuchezea timu za Mataifa yao!😬

Ukija kwenye upande wa magolikipa na walinzi, mambo ni yale yale! Ukienda kwa washambuliaji, ndiyo kabisaa unakutana na kinara wa ufungaji kwa sasa! Papaa Mayele! 😬
 
Kama ningekuwa Nabi ningetumia 3-5-2.

Back 3 yangu ingekuwa Mwamnyeto,Job na Bacca.

Shabaan Djuma na Yassin wangekua 'wing back'

Khalid Aucho deep lying mid.

Holding Mid angecheza Yanick Bangala.

Ntibazokiza CAM.

Fei Toto angecheza nyuma ya FKM.

Hapo vipi.
Ni nzuri ila kwa Yassin angeanza David bryson, Yassin sio mzuri going forward(technically), not calm with the ball, has a tendency of forcing direct passes & going long, by which 're not good traits for a settled possession side.
 
Ambundo anajua sana, ningependa kila game Ambundo aanze instead of Ducapele.
 
Back
Top Bottom