Ijue Malware ya iliyokuwa preinstalled kwenye simu za android zaidi ya milioni tano Duniani

rootadmin

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
349
242
Watafiti wa kiusalama (Security Researchers) Wamegundua malware inayo semekana inaendelea kukua kwa kasi sana ambayo tayari imesha ambukiza vifaa vya mikononi (mobile devices) zaidi ya milioni 5 Dunia nzima.

Vifaa vyote vilivyoathiriwa vilitumwa kupitia Tian Pai, Hangzhou(Kampuni inayo jihusisha na usambazaji wa simu), Lakini watafiti hao hawana uhakika kuwa Kampuni hii inahusika moja kwa moja na Malware hio.

Kwa mujibu wa Timu hiyo ya usalama wa simu ambayo imegundua suala hili inasema kuwa programu ya Android iitwayo RottenSys sio programu halali inayo toa Huduma za wifi kwani imekua ikidai Ruhusa (Permissions) nyeti kama Camera,microfone,message etc ili iweze kuisaidia kufanya shughuri zake za kudukua vizuri bila kujulikana.

pia watafiti hao waliongezea kwa kusema kuwa kwa kulingana na matokeo yao malware hiyo ya RottenSys ilianza kuenea mwezi septemba 2016 hadi mwezi machi 2018, ambapo vifaa zaidi ya vifaa 4,964,460 viliambukizwa na malware hii ya RottenSys.

Ili kuepuka kugunduliwa, programu ya huduma ya Wi-Fi(RottenSys) ya mfumo wa bandia inakuja mwanzoni bila sehemu ya uharibifu na haijaanza shughuli yoyote mbaya

Badala yake, RottenSys imetengenezwa kuwasiliana na Server zake za command-and-control servers ili kupata orodha ya vipengele vinavyohitajika, ambavyo vina Codes halisi zenye viashiria vya malicious.

RottenSys itaanza kudownload programs au Applications za simu na kuinstall bila wewe kujua.
Je ulishawahi kujiuliza kwanini unakuta baadhi ya apps kweny simu yako zimejidownload bila wewe kudownload na kuinstall .? bila shaka na ww pia ni mmoja wa Muathirika wa Malware hiyo.

Dhumuni ya Malware hii ni kuinstall kitu kinaitwa Adware.. Adware ni programu ambayo inakuwa inadisplay ads kwa mfumo wa pop up .. watu wengi wamekuwa ni waathirika wa tatizo hili la kupopup ads kwa simu yako wengine hutumia popupblocker kama njia mbadala ya kuzuia Tatizo hili.

Mwaka jana, Makampuni ya simu za smartphone kama Samsung, LG, Xiaomi, Asus, Nexus, Oppo, na Lenovo, ziliambukizwa na baadhi ya programu zisizo za awali (Malware ) kama (Loki Trojan na SLocker mobile ransomware)zilizo tengenezwa kwajili ya kupeleleza watumiaji wa simu hizo.

Nitajuaje kuwa simu yangu imeathiriwa na Malware hii.?
Kuangalia kuwa simu yako imathiriwa na Malware hii itabidi ufanye hivi
nenda Settings > App Manager > all apps
kisha angalia package zenye majina kama haya.

  • com.android.yellowcalendarz (每日黄历)
  • com.changmi.launcher (畅米桌面)
  • com.android.services.securewifi (系统WIFI服务)
  • com.system.service.zdsgt
kama ukizikuta Rahisi sana unistall it. kisha zima simu yako na uwashe.
 
Nikwel aisee,hata mim nasumbuliwa sana na hili tatzo,shukran sana mkuu,..yaan kuna adds skuhiz zinafosi uziangalie,na kutoka hazitak had ziishe *****
 
Nikwel aisee,hata mim nasumbuliwa sana na hili tatzo,shukran sana mkuu,..yaan kuna adds skuhiz zinafosi uziangalie,na kutoka hazitak had ziishe *****
pole sana mkuu,...
katika simu yako fungua settings > app manager >all au simu zingine zimeandikwa system apps
kisha tafuta majina haya
  • com.android.yellowcalendarz (每日黄历)
  • com.changmi.launcher (畅米桌面)
  • com.android.services.securewifi (系统WIFI服务)
  • com.system.service.zdsgt
kila utakapo kuta jina kama hili wewe unistall tuu.. baada ya kumaliza ku unistall zote sasa zima simu yako then iwashe tena itakua good...
 
com.android hii hata nikiunistall nikizima simu nikiiwasha naikuta imerudi tena,naitoaje hii chief
 
com.android hii hata nikiunistall nikizima simu nikiiwasha naikuta imerudi tena,naitoaje hii chief
sio com.android malizia package nzima com.android.yellowcalendarz hapo hilo jina lenye yellowcalendarz ndo lina matter zaidi sio hio com.android
 
Vzr kwa taarifa lkn kwa sasa simu nyingi haswa samsung zinaingia na security iitwayo DEVICE MAINTENANCE .. inascan virus..
 
Vzr kwa taarifa lkn kwa sasa simu nyingi haswa samsung zinaingia na security iitwayo DEVICE MAINTENANCE .. inascan virus..
Tambua kuwa hyo malware ni built in yani since simu inatengezwa wakati wa kuweka os ndipo walipo weka na hzo malware
 
Back
Top Bottom