Ijue historia ya Simba Achikongo kutokea Tunduru

Mdau1000

Member
Joined
Aug 21, 2024
Posts
16
Reaction score
11
Tunduru ni moja ya wilaya ambayo inapatikana katika mkoa wa Ruvuma kusini mwa Tanzania, asili ya wakazi wa Tunduru ni Wayao ambao wanasadikika wanatokea Msumbuji, katikati ya miaka ya 80 kulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa anafahamika Mzee ACHIMBALI, Mzee huyo alikua anaishi katika kijiji cha Marombe km zipatazo 10 kutoka Tunduru mjini ambayi kwa wakati huo ikikua na mapori kwa asilimia kubwa

ACHIMBALI alikuwa ni mtaalamu wa mitishamba pamoja na masuala ya uganga wa jadi, moja kati ya kazi zake ambazo zilikuwa maarufu ni kuzusha simba

Mzee ACHIMBALI alitengeneza simba kupitia mtu ambaye alikua na ulemavu katika moja ya mkono au mguu wake hasa katika kiganja, simba huyo alijulikana kwa jina la Achikongo kutokana na ulemavu huo.

SIMBA achikongo alihusika kwa kiasi kikubwa kutekeleza mauaji ya wakazi wa Tunduru, alikua anaua kwa kupitanisha kama leo anaua wa kike basi kesho ataua wa kiume lakini pia kama leo ataua marombe basi kesho ataua Misyaje hali hii ili pelekea apewe jina la (Simba makaratasi)

KIHOJA CHA KUSTAAJABISHA
mkuu wa kitengo cha maliasili (Gemu) ambaye alipangiwa majukumu yake Tunduru wakati anaripoti kuna kauli ambazo sio rafiki alizitoa kwa wenyeji wake akiwasanifu juu ya hofu iliyojijenga kutokana na simba huyo, basi jioni ya siku hiyo Wakati anarudi kumsindikiza mwanamke ambaye inasemekana alikua mchepuko wake katika eneo la Frankwestoni alikumbana ma Simba achikongo, simba alimtafuna karibia mwili mzima akabakisha kichwa na mkono ambao ulikua na saa.

Ama hakika simba achikonga alikua kisanga, alitikisa mitaa yote ya mlingoti, extended, majengo, Nakayaya, Mkapunda, Kadewele, NAKAPANYA, Semeni, Namwinyu mpaka njenga.

Kuuwawa kwa simba Achikongo

Ndugu msomaji chukua kikombe cha maji jimwagie kichwani kupoza Swaumu huku tukikuletea mkasa kamili wa namna alivyo uwawa mpaka Mheshiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo Mzee ALLY HASANI MWINYI kutua na helikopta kuhutubia umati wa wana Makombe na jioni yake simba kulipa kisasi.. Usikae mbali uzi bado unaendelea.
 
Muendelezo uko wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom