Ijue historia ya Mji wa Tukuyu-Mbeya

LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,312
6,638
images (15).jpeg

Historia ya mji wa Tukuyu inaanzia enzi za Utawala wa Ujerumani nchini Tanganyika, Mji Mkuu wa utawala wa Ujerumani nchini Tanganyika ulikuwa ni Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani.

Ujerumani ili kujilinda na hatari ya kuvamiwa na Uingereza ambayo ilikuwa ikitawala Nyasaland, 'Malawi ya sasa' utawala wa Ujerumani uliamua kujiimarisha kando kando ya ziwa Nyasa katika eneo lililoitwa Langburg " Mwaya ya sasa" Lungburg maana yake ni Boma lefu au Ngome.

Mji wa Langburg ulikuwa ni eneo lote la Matema na Ipinda, boma la mji wa Mwaya au Langburg kwa sasa halipo tena limeshazama ndani ya ziwa Nyasa.

Baada ya Wajerumani kuamua kuuhama mji wa Mwaya au Langburg, ndipo walikuja kujenga Boma katika eneo la Tukuyu na ndio ukawa mwanzo wa mji wa Tukuyu ambao Wajerumani waliuita Neu Langburg, wakiwa na maana ya Langburg mpya.

Baada ya Wajerumani kujenga Boma katika Mji wa Tukuyu au Neu Langburg, pia walijenga Kambi ya Kijeshi katika kijiji cha Masoko kando kando ya Ziwa Kisiba, Masoko ukiwa njiani kueleka Mbambo, Bwibuka, Bujesi mpaka Lwangwa.

KIINI CHA ENEO LA BAGAMOYO MJINI TUKUYU

Wakati Wajerumani wanakuja Tukuyu walikuja na Askari pamoja na wapagazi kutoka Bagamoyo Pwani, ambao walikuwa ni masalia ya vizazi vya utumwa, makabila yaliyokuja na Wajerumani yalikuwa ni Wayao, Wamanyema, Wanyamwezi, Wamakonde, Wangoni, Wangindo n.k

Wengi ya wapagazi hao walikuwa ni Waislam kutokana na asili ya walikotoka yaani Bagamoyo ya Pwani ya Bahari ya Hindi, hivyo Wajerumani waliamua kuwapa watu waliokuja nao eneo la kuishi mwanzo mwa Mji wa Tukuyu, nao wakaamua kuliita eneo hilo Bagamoyo, ili kuenzi walikotoka.

Wapagazi wote waliokuja hawakuja na wake zao na walipata tabu sana kupata wake wa kuoa kutoka kabila la Wanyakyusa, kwani walitofautiana sana katika mila na desturi zao.

Baadae wapagazi hao walipata wasaidizi kutoka katika kabila la Wakinga kutoka Lupila, mkinga wa kwanza kuja kuishi Bagamoyo alikuwa ni Sadiki Mkakile, na alikubali kusilimu na kuwa Muislam.

Sadiki Mkakile ndiye anasadikiwa kuwa aliyerudi tena Ukinga na kuwachukua wakinga wengine na kuja nao Tukuyu-Bagamoyo kwa sharti la kusilimu na kuwa Waislam, aliwaleta huku akijifanya ni ndugu zake.

Mzee Mohamed Mpangule Kyando ndio Mkinga pekee ambaye alikuja Bagamoyo akiwa ni Muislamu tayari kwa kuwa yeye hakuja akitokea Ukinga bali alitokea Tanga na kuja Bagamoyo moja kwa moja,
inasemekana baada ya wapagazi na Wakinga walipokaa pamoja na kuelewana vizuri, wapagazi waliwashawishi wakinga kurudi ukinga kwenda kuwatafutia Wanawake wa kuoa.

Wapagazi hao walipoona umri wao umekuwa mkubwa waliamua kuwarithisha mali zao Wakinga na ndipo sehemu kubwa ya Bagamoyo ya Tukuyu kuwa na Wakinga ambao ni Waislamu.

HISTORIA YA ELIMU KWENYE MJI WA TUKUYU

Wakati wa ukoloni wa Mwingereza na mwanzoni mwa Uhuru wa Tanganyika, sera ya elimu ilikuwa ni Darasa la Kwanza mpaka Darasa la Nne na baadae Mwanafunzi akifaulu anaendelea Darasa la Tano mpaka la Mjie.

Kabla ya mwaka 1964 Mji wa Tukuyu ulikuwa na Shule za Darasa la Kwanza mpaka la Nne zifuatazo.

1. Tukuyu boys, sasa inaitwa Tukuyu Day Sekondari
2. Tukuyu Girls, sasa inaitwa Bulyaga Shule ya Msingi
3. Tukuyu Mixed, sasa inaitwa Tukuyu Polisi Shule ya Msingi
4. TAPA, sasa inaitwa Madaraka Shule ya Msingi.
5. Katumba One
6. Katumba Two
7. Aghakhan, sasa inaitwa Bagamoyo Shule ya Msingi
8. Kyimbila

Shule hizi zote zilikuwa zinategemea Wanafunzi wao wanaofaulu kuendelea Darasa la Tano kwenda katika Shule zifuatazo.
1. Ndembela Boys
2. Mpuguso Boys
3. Lutengano Girls

Hizo ndizo Shule pekee zilizokuwa zinategemewa kuchukua Wanafunzi wanaofaulu, si kwa Shule za Tukuyu tu, bali kwa Rungwe nzima. Hali hiyo iliwalazimu Viongozi wa Wilaya kuumiza vichwa na kutafuta jinsi ya kupata Shule nyingine ya Darasa la Tano mpaka Nane.

Ndipo mwaka 1964 ilipoamuliwa kuwa Eneo na majengo yaliyokuwa yakitumiwa kuwaandaa watu kwenda kufanya kazi za migodini katika nchi za Afrika kusini, Zambia na Zimbabwe. Lichukuliwe na kugeuzwa shule, na shule hiyo ikaitwa Tukuyu Model, sasa inaitwa Magereza Shule ya Msingi.

Mwalimu Mkuu wa wa kwanza wa Shule ya Tukuyu Model alikuwa Marehemu Mwalimu George Mwakyembe, baba yake Dkt. Harrison George Mwakyembe aliyekuwa Mbunge wa Kyela.

Pia kwa wakati mmoja huo huo Mwalimu George Mwakyembe alikuwa Mkuu wa Shule zifuatazo Tukuyu Boys, Tukuyu Mixed na Tukuyu Model.

Miongoni mwa Wanafunzi
wa kwanza wa Shule ya Tukuyu Model ilipoanzishwa mwaka 1964 walikuwa Joseph Kasyupa na Habibu Saidi Mohamed. Mwalimu wa Darasa wa Kwanza shuleni hapo alikuwa Mwalimu Ulindula Mwamakombe.

KIINI CHA SHULE YA MSINGI MAGEREZA

Muingereza wakati akitawala Tanganyika pia alikuwa akitawala Afrika Kusini, Zambia, Malawi na Zimbabwe kwa Nchi za Kusini mwa Afrika, katika Nchi za Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini kulikuwa na migodi ya madini mbali mbali, hivyo ilimuhitaji Muingereza kuhitaji watu wa kwenda kufanya kazi migodini.

Baada ya kuumiza kichwa Muingereza akagundua kuwa Wanyakyusa hawakuwa waoga kufanya kazi za migodini na walizipenda kazi hizo, ndipo alipoamua kuanzisha kambi ya kukusanya na kufundisha watu wa kwenda kufanya kazi migodini.

Kambi hiyo ilianzishwa eneo la jirani na Gereza la Tukuyu, na ilikuwa na majengo yafuatayo:

1. Ofisi za Kambi, sasa hivi ni Ofisi ya kazi ya Wilaya ya Rungwe.
2. Nyumba za Wafanyakazi, kwa sasa wanakaa Wafanyakazi wa ofisi ya Kazi
3. Mabweni na Bwalo la chakula, kwa sasa ni Madarasa mlManne ya Shule ya Msingi Magereza yanayotazamana na Gereza la Tukuyu
4. Nyumba ya Meneja, kwa sasa ni nyumba aliyopewa Amon Nsekela.

(Andiko hili limeandaliwa kwa msaada wa simulizi za watu wa zamanizamani na pia taarifa mbalimbali zilizomo kwenye mitandao)

Ndagha Fujho Bhanyakyusa!
 
mimi natafuta nyumba ya kununurra Tukuyu kama kuna mtu ana taarifa nyumba inauzwa
 
Hiyo ni historia ya Tukuyu kipindi cha wakoloni, lete historia ya Tukuyu yenyewe, maana katika maelezo yako yanaonyesha wajerumani waliikuta tukuyu ipo
 
Nimefika Tukuyu,pana hali nzuri sana ya hewa.
Umeandika historia nzuri sana kwa mji wa Tukuyu.
Mwaka 1993 Nilikunywa "Power Na.1" pale stand,kulikuwa na baa inaitwa "Three in one".Nitarudi tena Tukuyu
 
Hujatoa asili ya neno Tukuyu....inasemekana kandokando wa barabara inayoelekea bomani...zilipo ofisi za mkuu wa wilaya kulikuwa na mti mkuyu "unkuju" hivyo raia wa mji huo walikuwa wakitamka "pankuju" wakimaanisha kwenye mkuyu jina ambalo wajerumani walishindwa kulitamka kiufasaha na kujikuta neno Tukuyu linazalishwa....neno ambalo watu wanachanganya kunawanaofikiri kuwa Tukuyu ni wilaya....Tukuyu ni mjii mkuu wa wilaya ya Rungwe.
Usisahau matajiri wa enzi hizo, pesambili, Baba Lea watoto, mwakyambiki nk.
 
Historia ya mji wa Tukuyu inaanzia enzi za Utawala wa Ujerumani nchini Tanganyika, mji mkuu wa utawala wa Ujerumani nchini Tanganyika ulikuwa ni Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

Ujerumani ili kujilinda na hatari ya kuvamiwa na Uingereza ambayo ilikuwa ikitawala Nyasaland, 'Malawi ya sasa' utawala wa Ujerumani uliamua kujiimalisha kando kando ya ziwa Nyasa katika eneo lililoitwa Langburg " Mwaya ya sasa"
Lungburg maana yake ni Boma lefu au Ngome.

Mji wa Langburg ulikuwa ni eneo lote la Matema na Ipinda, boma la mji wa Mwaya au Langburg kwa sasa halipo tena kwani limeshazama ndani ya ziwa Nyasa.

Baada ya Wajerumani kuamua kuuhama mji wa Mwaya au Langburg, ndipo walikuja kujenga Boma katika eneo la Tukuyu na ndio ukawa mwanzo wa mji wa Tukuyu ambao Wajerumani waliuita Neu Langburg, wakiwa na maana ya Langburg mpya.

Baada ya Wajerumani kujenga boma katika mji wa Tukuyu au Neu Langburg, pia walijenga kambi ya kijeshi katika kijiji cha Masoko kando kando ya ziwa Kisiba, Masoko ukiwa njiani kueleka Mbambo, Bwibuka, Bujesi mpaka Lwangwa.

KIINI CHA ENEO LA BAGAMOYO MJINI TUKUYU:
Wakati Wajerumani wanakuja Tukuyu walikuja na askari pamoja na wapagazi kutoka Bagamoyo Pwani, ambao walikuwa ni masalia ya vizazi vya utumwa, makabila yaliyokuja na Wajerumani yalikuwa ni Wayao, Wamanyema, Wanyamwezi, Wamakonde, Wangoni, Wangindo n.k

Wengi ya wapagazi hao walikuwa ni Waislam kutokana na asili ya walikotoka yaani Bagamoyo ya Pwani ya bahari ya Hindi, Hivyo Wajerumani waliamua kuwapa watu waliokuja nao eneo la kuishi mwanzo mwa mji wa Tukuyu, nao wakaamua kuliita eneo hilo Bagamoyo, ili kuenzi walikotoka.

Wapagazi wote waliokuja hawakuja na wake zao na walipata tabu sana kupata wake wa kuoa kutoka kabila la Wanyakyusa, kwani walitofautiana sana katika mila na desturi zao.

Baadae wapagazi hao walipata wasaidizi kutoka katika kabila la Wakinga kutoka Lupila, mkinga wa kwanza kuja kuishi Bagamoyo alikuwa ni Sadiki Mkakile, na alikubali kusilimu na kuwa Muislam.

Sadiki Mkakile ndiye anasadikiwa kuwa aliyerudi tena Ukinga na kuwachukua wakinga wengine na kuja nao Tukuyu Bagamoyo kwa sharti la kusilimu na kuwa Waislam, aliwaleta huku akijifanya ni ndugu zake.

Mzee Mohamed Mpangule Kyando ndio Mkinga pekee ambaye alikuja Bagamoyo akiwa ni muislamu tayari, kwa kuwa yeye hakuja akitokea ukinga bali alitokea Tanga na kuja Bagamoyo moja kwa moja,
Inasemekana baada ya wapagazi na wakinga walipokaa pamoja na kuelewana vizuri, wapagazi waliwashawishi wakinga kurudi ukinga kwenda kuwatafutia wanawake wa kuoa

Wapagazi hao walipoona umri wao umekuwa mkubwa waliamua kuwarithisha mali zao Wakinga na ndipo sehemu kubwa ya Bagamoyo ya Tukuyu kuwa na Wakinga ambao ni Waislamu.

HISTORIA YA ELIMU KWENYE MJI WA TUKUYU:
Wakati wa ukoloni wa Mwingereza na mwanzoni mwa uhuru wa Tanganyika, sera ya elimu ilikuwa ni darasa la kwanza mpaka darasa la nne na baadae mwanafunzi akifaulu anaendelea darasa la tano mpaka la nane.

Kabla ya mwaka 1964 mji wa Tukuyu ulikuwa na shule za darasa la kwanza mpaka la nne zifuatazo.
1. Tukuyu boys, sasa inaitwa Tukuyu day Sekondari
2. Tukuyu girls, sasa inaitwa Bulyaga Shule ya Msingi
3. Tukuyu mixed, sasa inaitwa Tukuyu Polisi Shule ya Msingi
4. TAPA, sasa inaitwa Madaraka Shule ya Msingi.
5. Katumba one
6. Katumba two
7. Aghakhan, sasa inaitwa Bagamoyo Shule ya Msingi
8. Kyimbila

Shule hizi zote zilikuwa zinategemea wanafunzi wao wanaofaulu kuendelea darasa la tano kwenda katika shule zifuatazo.
1. Ndembela boys
2. Mpuguso boys
3. Lutengano girls

Hizo ndizo shule pekee zilizokuwa zinategemewa kuchukua wanafunzi wanaofaulu, si kwa shule za Tukuyu tu, bali kwa Rungwe nzima. Hali hiyo iliwalazimu viongozi wa wilaya kuumiza vichwa na kutafuta jinsi ya kupata shule nyingine ya darasa la tano mpaka nane.

Ndipo mwaka 1964 ilipoamuliwa kuwa Eneo na majengo yaliyokuwa yakitumiwa kuwaandaa watu kwenda kufanya kazi za migodini katika nchi za Afrika kusini, Zambia na Zimbabwe. Lichukuliwe na kugeuzwa shule, na shule hiyo ikaitwa Tukuyu Model, sasa inaitwa Magereza Shule ya Msingi.

Mwalimu Mkuu wa wa kwanza wa shule ya Tukuyu Model alikuwa Marehemu Mwalimu George Mwakyembe, baba yake Mhe. Harrison George Mwakyembe Mbunge wa Kyela.

Pia kwa wakati mmoja huo huo Mwalimu George Mwakyembe alikuwa Mkuu wa Shule zifuatazo Tukuyu boys, Tukuyu Mixed na Tukuyu Model. Miongoni mwa wanafunzi
wa kwanza wa shule ya Tukuyu Model ilipoanzishwa mwaka 1964 walikuwa Joseph Kasyupa na Habibu Saidi Mohamed. Mwalimu wa darasa wa kwanza shuleni hapo alikuwa Mwalimu Ulindula Mwamakombe.

KIINI CHA SHULE YA MSINGI MAGEREZA;
Muingereza wakati akitawala Tanganyika pia alikuwa akitawala Afrika Kusini, Zambia, Malawi na Zimbabwe kwa nchi za kusini mwa Afrika, katika nchi za Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini kulikuwa na migodi ya madini mbali mbali, hivyo ilimuhitaji Muingereza kuhitaji watu wa kwenda kufanya kazi migodini.

Baada ya kuumiza kichwa Muingereza akagundua kuwa Wanyakyusa hawakuwa waoga kufanya kazi za migodini na walizipenda kazi hizo, ndipo alipoamua kuanzisha kambi ya kukusanya na kufundisha watu wa kwenda kufanya kazi migodini.

Kambi hiyo ilianzishwa eneo la jirani na Gereza la Tukuyu, na ilikuwa na majengo yafuatayo:

1. Ofisi za kambi, sasa hivi ni Ofisi ya kazi ya wilaya ya Rungwe.
2. Nyumba za wafanyakazi, kwa sasa wanakaa wafanyakazi wa ofisi ya kazi
3. Mabweni na bwalo la chakula, kwa sasa ni madarasa manne ya Shule ya Msingi Magereza yanayotazamana na Gereza la Tukuyu
4. Nyumba ya Meneja, kwa sasa ni nyumba aliyopewa Amon Nsekela.

(Andiko hili limeandaliwa kwa msaada wa simulizi za watu wa zamanizamani na pia taarifa mbalimbali zilizomo kwenye mitandao)

#Ndaga_fijo.....Bhanyakyusa!!!!!!!!!!
Mkuu sahihisha jina la kijerumani la Tukuyu.
Ni Neu Langenburg na si Neu Langburg.
 
Mkuu asante kwa historia, lakini ni historia ya juzi sana na inaacha mapengo mengi.
Nakubaliana na uasili wa kijerumani kwa mji wa Tukuyu, lakini jina lilikuwa ni Neu Langenburg.

Katika shule maarufu hata kabla ya uhuru, shule kama za Kyimbila na Lutengano toka enzi za mwalimu wa kikoloni Mary Hancock huwezi kuwakwepa kihistoria(miaka ya 1940~1950s).
Je unawafahamu waalimu maarufu kama Mwambapa(mwanawe alikuwa Gen Owen Mwambapa), Esili Mwakyambiki(alikuja kuwa mbunge wa Rungwe na naibu Waziri Ulinzi), mwl. Mwaijande, mwal. Mwabalakata,mwl Ngwala(yuko hai pale Kiwira)

Hao wote walimu wa tokea 1950s.
Najua wako wengine wengii hebu tuwaenzi.
 
Mnyaki wa kwanza kupeleka dini ya kikristo Tukuyu anaitwa Sindano Kyusa....all in all mleta mada umeandika vitu safi sana
 
Back
Top Bottom