Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,392
- 7,863
Aliingia mfanyakazi wa kawaida katika duka dogo la dawa, uso wake umechoka na mikono yake imepasuka kwa sababu ya kazi nyingi.
Akamuuliza mfamasia kwa sauti ya utulivu:
“Je, mna marhamu ya saruji(ni dawa ya kupaka juu ya ngozi kwa ajili ya kulainisha ngozi iliyokauka au kupasuka)?”
Mfamasia alicheka kwa dharau, na kwa sauti ya kejeli akasema:
“Tunayo marhamu ya saruji, na ya mawe pia! Je, unapendelea ya ndani au ya kutoka nchi za nje?”
Mfanyakazi alijibu kwa utulivu uleule, bila kuguswa na kejeli:
“Ya kutoka nje, tafadhali.”
Mfamasia akamjibu kwa dhihaka:
“Ni ghali sana, nakutahadharisha mapema!” Kisha akacheka kwa kujivuna.
📌Hapo mfanyakazi akainua mikono yake juu, na kusema maneno yaliyotikisa mioyo na kusimamisha kicheko:
“Mimi ni mfanyakazi wa saruji, mikono yangu ni migumu kiasi kwamba siwezi kugusa shavu la binti yangu mdogo…
Kila jioni hukimbilia kwangu, akiomba kumkumbatia…
Lakini naogopa kumuosha kwa mabaki ya saruji na mikono yangu migumu iliyopasuka…
Kama unayo marhamu inayoweza kunifanya nimkumbatie bila hofu…
Basi nipe ile ya bei ghali zaidi, nitailipia tu kwa ajili ya mwanangu nimkumbatie akiwa salama.”
❄️Ghafla… kicheko cha mfamasia kilisitishwa palepale,
Akaona nafsi yake ndogo, dhaifu mbele ya ukubwa wa moyo wa mtu huyu…
Akatambua kuwa yeye pia ni baba, lakini amewasahau watoto wake kwa muda mrefu sana
Hajawahi kuwakumbatia, wala kuhisi joto la upendo wao…
💔Kweli, umasikini wa kweli si ukosefu wa pesa…
Bali ni umasikini ni ule wa moyo uliosahau huruma kwa familia.
Umasikini… ni umasikini wa maadili.
Pamoja na hali yako ngumu ya kimaisha usiache kuipenda, kuihurumia, kuijali na kuithamini familia yako, Familia yako ndo kila kitu maishani mwako