Igunga Special Photos

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,345
WanaJF nitakuwa nawekea picha za mikutano ya CDM katika kipindi hiki cha lala salama, kwa kuanzia jionee hali halisi ambapo Mh. Freemani Mbowe alitua na chopa na kutema cheche.

nkinga 1.jpg
nkinga 2.jpg
Nkinga 3.jpg
Nkinga 4.jpg
nkinga.jpg
Karibuni,
 
Shukrani mkuu. vijana hawa woteeeee..... hawana imani na CCM bali matarajio na matategemeo yao yote yako kwa CHADEMA.
 
WOTE HAWA hawapewa wali, kwasababu wanajua wataharisha baada ya siku mbili na kuwa na njaa tena! Hawajapewa tshirts kwakuwa wanajua ni aibu kuvaa kuvaa vitu hivyo wakati wezi wa nchi wanavaa suti kali na kutembelea vx. Waangalie vyema. Wote wako tiyari kupigania haki zao. Wamenuna kama msoja. Wanandita zinazoonesha uelewa wa hali ya juu.
 
WOTE HAWA hawapewa wali, kwasababu wanajua wataharisha baada ya siku mbili na kuwa na njaa tena! Hawajapewa tshirts kwakuwa wanajua ni aibu kuvaa kuvaa vitu hivyo wakati wezi wa nchi wanavaa suti kali na kutembelea vx. Waangalie vyema. Wote wako tiyari kupigania haki zao. Wamenuna kama msoja. Wanandita zinazoonesha uelewa wa hali ya juu.

Mkuu kwa kweli inatia moyo. Ufanyike uhamasishaji wa mkubwa kuhakikisha kuwa umati huu unajitokeza kupiga kura. Isiishie tu kwenye kuishangaa chopa.
 
Dah! Hii ndio nguvu ya UMMA bwana! nawatakia kila kheri makamanda wote walioko mstari wa mbele huko igunga, Nasali sana wezi wote wa kura huko igunga wapigwe upofu. Ameeen!
 
leo tumefanya mikutano sita kwenye kata sita na chopa,pamoja na chopa tumeendelea na mikutano ya ndani,kimsingi tunashambulia kote kote
Mkuu shaka yangu si watu kujitokeza katika mikutano au kushambulia ila ni watu kujitokeza siku ya mwisho na kufanya maamuzi sahihi. Tuombe Mungu mambo yaende kama yalivyopangwa.
 
Mkuu kwa kweli inatia moyo. Ufanyike uhamasishaji wa mkubwa kuhakikisha kuwa umati huu unajitokeza kupiga kura. Isiishie tu kwenye kuishangaa chopa.
Hilo ndiyo neno nililotaka kulisema, uzoefu unaonyesha kuna mwitikio mzuri katika mikutano lakini siku ya kura wananchi hawaoni umuhimu wa kura zao na kupuuzia jambo ambalo ni hatari. Naomba hili lisitokee ili uchaguzi huu ili uvunje rekodi ya watu waliopiga kura.
 
Tuombe tu Amani itawale mpaka siku ya uchaguzi na hata wakati wa kutangaza matokeo. Nina wasi wasi kwamba hizi picha zitawachochea wale jamaa waanze kuzungusha vifaru huko Igunga. Kama walianza kuonyesha Bastola kule mwanzo kabisa sasa watapanda kwenye majukwaa na Maroketi. Washindwe na Walegee!
 
kazi kazi mpaka kieleweke .. .
Safari hii nadhani Igunga itawagawa watanzani yaani jimbo limekuwa hot kama uchaguzi wa rais vile! Ikitokea upinzani umeshinda nitaomba gamba lingine lijivue aanze Lowasa kisha upinzani uchukue ile tunamaliza tu gamba lingine linajivua ambalo ni chenge. Ikitokea hivyo nadhani hazina itakauka kwa jinsi nguvu na rasilimali nyingi zitavyokotumika.
 
Yale mahindi ya magamba yanayotoka Shinyanga ya kuwapa rushwa wana igunga bado hayajafika? Kweli CCM kazi ipo labda wabadilishe mbinu. Ninawashauri sasa wanapowahutubia wananchi wawaambie kwamba wao ni Chadema-B huenda wakaambulia vikura vichache vya huruma
 
Akhsante sana Mh Nanyaro,

ila kwa kweli imeniuma sana kuuona umma huu uliogubuikwa na umasikini umekuwa mteja wa CCM na mhindi rostam

muda wa kuzinguka ni huu!!! mimi na familia yangu tumewaweka kwenye maombi Chadema na Igunga. J2 nitatoa sadaka kanisani 10.000 kwa ajili ya kuSHUKURU kwa ajili ya ushindi wa Chadema Igunga. nitashukuru kwa amani iloendelea kushamiri kwa kuwepo uchaguzi wa huru na haki. nitamshukuru pia Mungu kwa kuwapofusha na kuwatia uoga WEZI WOTE WA KURA...

KILA LA KHERI!
 
Akhsante sana Mh Nanyaro,

ila kwa kweli imeniuma sana kuuona umma huu uliogubuikwa na umasikini umekuwa mteja wa CCM na mhindi rostam

muda wa kuzinguka ni huu!!! mimi na familia yangu tumewaweka kwenye maombi Chadema na Igunga. J2 nitatoa sadaka kanisani 10.000 kwa ajili ya kuiombea Chadema ishinde Igunga. pia amani iendelee kushamiri kwa kuwepo uchaguzi wa huru na haki. nintaomba pia Mungu AWAPOFUSHE WEZI WOTE WA KURA...

KILA LA KHERI!

Kweleakwelea Mungu akutangulie maana Igunga imevuta hisia za watu tofauti na mtazamo wa awali. Kuna kitu kipo behind the scene, noamba uchaguzi uende kwa amani na watu wajitokeze ili tuweze kuona matunda ya demokrasia na si uchachuaji.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom