Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwamdala iliyopo kijiji cha Igudi, tarafa ya Igalula, Juma Masanja (28), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Igunga kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 18 ambaye ni shemeji yake na kumsababishia ujauzito.
Awali mwendesha mashitaka wa polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi kuwa kati ya Septemba mwaka 2016 na Mei 2017, mshitakiwa Masanja kwa nyakati tofauti alimbaka binti huyo (jina limehifadhiwa).
Kweyamba aliendelea kuiambia mahakama kuwa mshitakiwa Masanja pamoja na kumbaka binti huyo ambaye ni shemeji yake, pia alimtishia maisha yake kwa kumtaka kuweka siri ya kubakwa na endapo angetoa siri hiyo angempotezea maisha yake.
Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 7, 2017 na mshitakiwa yuko nje kwa dhamana.
HabariLeo