Igunga: Mangula abanwa na wananchi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Monday, 26 September 2011 08:05Daniel Mjema, Igunga

MWANANCHI wa Kitongoji cha Mwamsungu,Jimbo la Igunga, Nzile Faregaro, amembana Katibu mkuu mstaafu wa CCM, Philip Mangula, awahakikishie kuwa mgombea wao, Dk Dalaly Kafumu, hataiga hulka na tabia za mtangulizi wake, Rostam Aziz.


Tukio lilitokea jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM wa kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, ambao ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Athuman Mfutakamba.


Baada ya kumaliza kuhutubia, makada hao wa CCM waliruhusu maswali matatu ndipo muuliza swali wa tatu, Faregaro alipoibua hoja hiyo kwamba tangu wamchague Rostam hawajawahi kumwona kwa miaka 15.


“Tangu tumchague Rostam hajawahi kututembelea kwa miaka 15 sisi tutawapa kura, lakini tunataka mumlete mgombea hapa tumuulize maswali na atuhakikishie kama hatatutelekeza kama alivyofanya Rostam,” alisema Faregaro.


Akizungumza kwa hisia kali, mzee huyo aliongeza kuwa hata kama anatuona ni wajinga, lakini alitakiwa kuja tu siyo kuishia huko mjini na ndiyo maana tunamtaka Kafumu aje hapa tumuulize maswali.


Hata hivyo, Dk Kafumu hakuwapo katika mkutano huo kutokana na utaratibu wa CCM, ambao wamejigawa makundi 12 kushambulia mikutano ya hadhara na Dk Kafumu alikuwa kwenye mkutano mwingine.


Pia, Faregaro alitaka fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) Sh30 milioni ambazo zimetolewa na Serikali kwa kitongoji hicho kujenga Lambo kwa ajili ya mifugo, zitolewe ili zitumike kwa kazi hiyo.


Hata hivyo, swali hilo ambalo lilielekezwa meza kuu, lilijibiwa na Dk Mfutakamba ambaye aliwaahidi wananchi hao kumpeleka mgombea huyo, ili awahakikishie kuwa yeye ndiye mkombozi wa kero mbalimbali zinazowakabili.


Kuhusu fedha za Tasaf, Dk Mfutakamba alisema masharti ya fedha hizo ni wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 10 ya gharama za mradi ambazo ni Sh3 milioni, lakini hadi sasa wananchi wamechangia Sh1.5 milioni.


Mzee mwingine, Mboje Mkete, yeye alienda mbali na kusema japokuwa watamchagua Dk Kafumu, lakini wanataka ikifika Oktoba 20, ambazo ni siku 18 baada ya uchaguzi ahakikishe malambo yote kijijini hapo yamejengwa.


Awali, akihutubia mkutano huo, Mangula aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuepuka kuingia katika mtego wa kuwa sehemu ya kuanzisha vurugu, akiwataka kusimama imara na mwanasiasa atakayewashawishi hivyo wamwambie ‘hapana’.


Mangula alisema yapo mambo mazuri aliyoyaanzisha Rostam ikiwamo ujenzi wa sekondari na mwaka 1994, jimbo hilo lilikuwa na shule tatu, sasa lina shule 36 hivyo akawaomba wamchague Dk Kafumu ayaendeleze. 

Memo

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
2,157
759
Huyo mzee aliyeuliza swali ni wale tunawaita vibuyu!!
Eti hatujamuona Rostam kwa 15 years tangu tulipomchagua, pambafu kabisa. Kwani walimchagua mara moja awe mbunge kwa miaka 15???
Hivi hawa ccm na wanachama wao kumbe vichwa vyao vimefanana!!!
 

Lyceum

JF-Expert Member
Oct 1, 2009
1,043
567
Huyo mzee aliyeuliza swali ni wale tunawaita vibuyu!!
Eti hatujamuona Rostam kwa 15 years tangu tulipomchagua, pambafu kabisa. Kwani walimchagua mara moja awe mbunge kwa miaka 15???
Hivi hawa ccm na wanachama wao kumbe vichwa vyao vimefanana!!!

Mkuu ulitegemea asemeje wakati ameshasema kura atawapa na hapo hapo analalamika Rostam hajaonekana kwa miaka 15. Watu kama hawa wanatakiwa wafe njaa kwa kukumbatia ujinga. Kwa staili hii hatakwepa kifo cha aibu; NJAA NA TAABU
 

Memo

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
2,157
759
Sijaona "kubanwa" hapo zaidi ya maswali/swali la kawaida tu

Hwa magamba wananiudhi sana hawa!!!
katuni-majira-10-12-20101.jpg
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
35,233
35,205
kwa kweli maendeleo bado hata maswali yanayoulizwa ni laini sana watu bado hawajajua wajibu wa nchi yao kwao.
 

Juaangavu

JF-Expert Member
Nov 3, 2009
935
132
Duh! Tanzania ina mambo - wananchi hawana key performance indicators za kumpima mwakilishi wao. Ni kuchaguana kwa kwenda mbele; kisha baadaye kulalama - mwakilishi hatujamuona miaka kumi na mitano ilopita - hapa ndipo palipo na utamu wa bongoland!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
CCM sasa hivi hawana watu wa maana wa kwenda kufanya kampeni Igunga, karibu wote wanayo magamba. Wanaokoteza okoteza tu hapa na pale, hasa wale wenye kubeba tuhuma za ufisadi, maana wanajuwa hawatathubutu kukataa. Ufisadi sasa umekuwa mtaji katika kulazimishana. Huyu Mangula alilazimishwa tu kwa sababu ana tuhuma za EPA, hivyo anaogopa. hata Magufuli, kashfa yake ya ufisadi ya kuuza nyumba za wananchi zajulikana wazi na hivyo anaogopa kukataa.

Mbona makongoro Nyerere amegoma kwenda, amawatolea nje CCM na kuwaambia huko huko! Kwa kuwa Makongoro ni msafi hawawezi kumfanya lolote.

Sure: The guilty are always afraid.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom