GE2025 IGP Wambura: Hatuendi vitani lakini tunakwenda kusimamia usalama, amani, utulivu wa taifa letu kabla, wakati na baada ya uchaguzi

GE2025 IGP Wambura: Hatuendi vitani lakini tunakwenda kusimamia usalama, amani, utulivu wa taifa letu kabla, wakati na baada ya uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Akizungumza leo Agosti 11, 2025, katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi uliofanyika katika shule ya Polisi Moshi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Camillus Wambura ameeleza kuwa hali ya usalama ni shwari na Jeshi hilo linajiandaa na uchaguzi kwa kuweka mikakati.

"Shughuli yoyote kubwa na muhimu ni lazima iwe na mipango mahususi, lazima iwe na mipango iliyopangiliwa kwajili ya kwenda kutimiza shughuli hiyo kwa umakini mkubwa, kwa kawaida hakuna vita inayopiganwa kwenye uwanja wa mapambano," alieleza IGP Wambura katika shughuli hiyo ambayo Makamu wa Rais Philip Mpango alikuwa mgeni rasmi.

"Vita yote hupiganwa mezani na pale mezani ndipo mikakati hupangwa na pale mezani miongoni mwa mikakati inayopangwa ni kubaini nguvu ya adui ,kubaini vifaa anavyotumia adui, iliujue Je? wewe unahitajika Kwenda na AK-47 au unahitajika Kwenda na mizinga au kwenda na aina gani ya silaha lakini ni vizuri kujua idadi ya askari alionao adui na utakapofika vitani ni utekelezaji wa mikakati ulikwisha kujiwekea," anendelea kufafanua IGP Wambura.

"Hatuendi vitani lakini tunakwenda kusimamia usalama, amani, utulivu wa taifa letu kabla, wakati na baada ya uchaguzi," alisisitiza Wambura.

 
Haaaaaaa hizi reference jamani -- adui ndio nani ? wananchi ? mko tayari kuumiza wananchi kwasababu ya watu kuchoka umaskini na ufisadi ? are you serious ? you have made it very clear kazi ya polisi ni kulinda watawala.

*** I see through the suppression of information even if it no longer involves the deletion of threads 🙂
 
Policcm mzigo upo kwenye akaunti! Kilichobakia hapo ni kumdhuru tu yeyote atakaye jitokeza kupinga dhuluma.
 
Unawatisha watu kwa faida ya ccm?
Traffic wanaokula rushwa hadharani tena kwenye njia unayopita wewe wamekushinda utaweza nguvu ya umma?
Wambura PAMBANA KWANZA NA TRQFFIC WALA RUSHWA kama unaouwezo
Mambo ya uchaguzi chama chako kitashinda tu kama wagombea wenyewe ni KINA CHEYO??
 
Back
Top Bottom