IGP unawafahamu ma "paluanja" ?

IGP unawafahamu ma "paluanja" ?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Kuna watu ni maarufu sana usiku wanafanya kazi nzuri sana wanaitwa mapaluanja.
Watu hawa hufanya kazi kama askari polisi ama askari wa Maliasili au uhamiaji. Inawezekana ni watoa taarifa (informer)..
Pamoja na kazi yao kuwa nzuri wengi wao si waaminifu na wanalidharirisha Jeshi la Polisi.

Nawasilisha.
 
Polisi wa Tz ni waonevu kwa raia IGP tunakuomba u deal na polisi wabaya wanaofanya raia huku tusilipende jeshi lako ni waonevu na wanaendeshwa kwa rushwa zaidi kuliko kutetea na kusimamia haki.
 
Mkuu ungeongeza ongeza na sisi vichwa maji tuelewe vizuri
Kuna siku utakutana nao mkuu usihofu, huwa hawana/ama hawavai sare. Itakuwia ngumu sana kuwatofautisha na askari halisi ni kama Tanesco na vishoka.

Ama chipukizi lisilo rasmi kutoka katika mti mkuu.
Kama hujanielewa bado mkuu pole..
 
Ni Nchi nzima?
juzi usiku km saa 2:30 nimekuta gari 2 zimeziba barabarani, moja Pick-up Double cabin na wameshuka jamaa wawili wanamsaidia mwenye Corolla au wanamhoji maswali, kwa vile niliona D/c Toyota imemulika taa hiyo Corola sikuhisi kitu nikapita kuelekea mahali, dk 5 tu nageuza namkuta Corolla peke yake na abiria kaduaa nikampigia honi nikapita, mra naona anakuja kwa kasi
Ghafla nikamtambua, nakanihemea kwa hofu WEZI SANA WALE ASKARI FIX
nini tena jamaa yangu?
ETI WAMENIFUMA NAMPAPASA ABIRIA WANGU (wa kike) NDANI YA GARI NA WAMENIPIGA PICHA
sasa unahofu nini km ni uongo
SI WAMETAKA MILIONI 2 LA SIVYO WASAMBAZE PICHA ZANGU
sasa km uongo achana nao
HAPANA WAMECHUKUA PESA NA VIFAA VYA MAMA
duh sikuamini kweli alikuwa anambanjua au kaibiwa lkn nikajua kuna viaskari vinajipaga majukumu km hayo
kumbe ndio hao paluanja?
 
Kuna watu ni maarufu sana usiku wanafanya kazi nzuri sana wanaitwa mapaluanja.
Watu hawa hufanya kazi kama askari polisi ama askari wa Maliasili au uhamiaji. Inawezekana ni watoa taarifa (informer)..
Pamoja na kazi yao kuwa nzuri wengi wao si waaminifu na wanalidharirisha Jeshi la Polisi.

Nawasilisha.
oya dogo kulikuwa na aja gan kuja kutuanika hapa. Ngoja sasa tukutrack
 
Usijali mkuu utakuwa na wenzio au peke yako? Nadhani tone zetu za sauti zinafanana karibu sana mkuu.
Ni sahihi wako wengi sana wanajifanya askari na muda wao ni usiku hata hii barabara ya kusini.kuanzia ikwiriri kuelekea lindi watu wanasimamishwa sana kumbe.ni.waporaji
 
Back
Top Bottom