IGP Simoni Sirro, Pokea pongezi na angalizo kamanda

Ila hiyo stendi inamambo ya ajabu sanaa yaani hata wale wanaokaa kwenye mageti ya kuingila nina uhakika wana hela ya kutoshaa.
 
Kibaya zaidi huduma ni mbovu sana, hata upangaji wa magari kwa ajili ya kupakia inategemea pesa yako
 
Pokea pongezi zangu na tahadhari pia.

Kamanda Simon Sirro;

Wewe ni miongoni mwa makamanda bora kutokea katika nchi hii kwa haya yafuatayo;

1. Ulipoingia kwenye nafasi hii ulikuta suala la Kibiti likiwa tete na mashaka makubwa lakini kwa weledi wako haikuchukua muda mrefu hali ilitulia.

2. Ulikomesha ujambazi kwa muda mfupi tu kwa wakati ule na hata wa hivi karibuni juhudi zako zilionekana.

3. Dar ilizidi kwa uhalifu na ulichukua hatua ngumu na najua ilikugharimu kumwondoa kijana wako Dar na kumleta Wambura hatimaye jembe Muliro.

4. Juhudi zako unazoendeleza kurejesha hali ya usalama ni kubwa mno kwani kwasasa umeshuka hadi ngazi ya vitongoji.

Ni mambo mengi mno unafanya mheshimiwa kwa ajili ya kuhakikisha raia wanakuwa salama...pokea pongezi nyingi

...ANGALIZO KWAKO...

STAND YA MAGUFULI UMEFUGA JOKA:

Mzee wangu pamoja na pongezi nyingi, na pamoja kuwa utumishi uliotukuka kumbuka katika jeshi la polisi hii ndio nafasi yako ya mwisho kabisa kwani mambo yakienda kombo hakuna cha kurudi ofisi kama ambavyo wewe utenguapo makamanda wa mikoa unasema fulani anarudi makao makuu...kwako hiyo nafasi haimo labda upewe cheo kingine nje ya jeshi la polisi.

Ninasema hivyo sababu jambo ambalo huenda utaliona dogo lakini laweza kuchafua jina lako na likakuaibisha.

Stand ya Magufuli mambo hayaendi vizuri, kituo kinanuka rushwa.

Mhusika wa ufisadi huu ni Mkuu ukaguzi wa magari katika kituo hiki cha Magufuli terminal, anadai kituo hicho kinalisha wakuu wa polisi Tanzania.

Mwaka jana aliondolewa Ubungo lakini wewe ulikuja alfajiri na uliamuru arudishwe, akarudishwa na kesho yake alitamba sana.
Na hapa watu wanaunganisha matukio.

Kuna wenye magari wasiotoa rushwa kuhusu ukaguzi wa magari, hufanyiwa vitimbi vya kila aina pamoja na namba za magari yao hung'olewa na kudaiwa ni mabovu hivyo huzuiliwa kusafiri ilhali waliotoa rushwa nono huwa hawakaguliwi hata mabasi yakiwa hayaridhishi...pindi ajali zikitokea haya yote yatasemwa, chukua tahadhari katika hili.

Ukitaka kuujua ukweli wa hili hizi zifuatazo ndizo namba za uwakala zinazokusanya rushwa za wenye mabasi na zipo traffic Makao Makuu banda la Uwakala.

Na namba yake ya tigo inayoanza na 0714 na kuishia na 7070

Mjumbe hauawi ukipokea hewala ukipuuzi pia ni sawa.

Nikutakie majukumu mema na utumishi mwema
Umenena vema hii stand polisi waifanyie kazi

Kuna Vita ya vikundi hasimu vya vibaka kilichokuwa ubungo vs kilichokuwa mbezi stand ya zaman ,wa ubungo wanasema wamehama na stand yao wambezi wanasema wao ni wazawa

USSR
 
Tatizo stand hii ni mradi wa wakubwa
 
Pokea pongezi zangu na tahadhari pia.

Kamanda Simon Sirro;

Wewe ni miongoni mwa makamanda bora kutokea katika nchi hii kwa haya yafuatayo;

1. Ulipoingia kwenye nafasi hii ulikuta suala la Kibiti likiwa tete na mashaka makubwa lakini kwa weledi wako haikuchukua muda mrefu hali ilitulia.

2. Ulikomesha ujambazi kwa muda mfupi tu kwa wakati ule na hata wa hivi karibuni juhudi zako zilionekana.

3. Dar ilizidi kwa uhalifu na ulichukua hatua ngumu na najua ilikugharimu kumwondoa kijana wako Dar na kumleta Wambura hatimaye jembe Muliro.

4. Juhudi zako unazoendeleza kurejesha hali ya usalama ni kubwa mno kwani kwasasa umeshuka hadi ngazi ya vitongoji.

Ni mambo mengi mno unafanya mheshimiwa kwa ajili ya kuhakikisha raia wanakuwa salama...pokea pongezi nyingi

...ANGALIZO KWAKO...

STAND YA MAGUFULI UMEFUGA JOKA:

Mzee wangu pamoja na pongezi nyingi, na pamoja kuwa utumishi uliotukuka kumbuka katika jeshi la polisi hii ndio nafasi yako ya mwisho kabisa kwani mambo yakienda kombo hakuna cha kurudi ofisi kama ambavyo wewe utenguapo makamanda wa mikoa unasema fulani anarudi makao makuu...kwako hiyo nafasi haimo labda upewe cheo kingine nje ya jeshi la polisi.

Ninasema hivyo sababu jambo ambalo huenda utaliona dogo lakini laweza kuchafua jina lako na likakuaibisha.

Stand ya Magufuli mambo hayaendi vizuri, kituo kinanuka rushwa.

Mhusika wa ufisadi huu ni Mkuu ukaguzi wa magari katika kituo hiki cha Magufuli terminal, anadai kituo hicho kinalisha wakuu wa polisi Tanzania.

Mwaka jana aliondolewa Ubungo lakini wewe ulikuja alfajiri na uliamuru arudishwe, akarudishwa na kesho yake alitamba sana.
Na hapa watu wanaunganisha matukio.

Kuna wenye magari wasiotoa rushwa kuhusu ukaguzi wa magari, hufanyiwa vitimbi vya kila aina pamoja na namba za magari yao hung'olewa na kudaiwa ni mabovu hivyo huzuiliwa kusafiri ilhali waliotoa rushwa nono huwa hawakaguliwi hata mabasi yakiwa hayaridhishi...pindi ajali zikitokea haya yote yatasemwa, chukua tahadhari katika hili.

Ukitaka kuujua ukweli wa hili hizi zifuatazo ndizo namba za uwakala zinazokusanya rushwa za wenye mabasi na zipo traffic Makao Makuu banda la Uwakala.

Na namba yake ya tigo inayoanza na 0714 na kuishia na 7070

Mjumbe hauawi ukipokea hewala ukipuuzi pia ni sawa.

Nikutakie majukumu mema na utumishi mwema
Majungu
 
Back
Top Bottom