ACP Mkoa wa Singida, unastahili pongezi

c h o l o

Member
Dec 9, 2023
92
156
Nawasalimu kwa jina la jamhuri,

Huyu mama nisipomsifu ntakuwa nimemnyima maua yake kwa kipindi hichi cha mwisho wa mwaka. Saluti nyingi kwako ACP wa mkoa wa Singida kwa kuziishi taratibu na sheria za jeshi la polisi la Tanzania.

Siku ya jumamosi nikiwa katika moja ya mihangaiko yangu ya kutwa katika moja ya barabara za ndanindani katika mji wa Singida ambayo muda wote huwa na msongamano wa watembea kwa miguu na magari yakipishana kwa kuviziana, kulikuwa na gari ndogo aina ya noah iliyokuwa imepaki kimakosa ikiwa inapakia pembejeo za kilimo na kusababisha magari mengine kupita kwa shida sana na hivyo kuleta tafrani katika eneo lile. Moja ya magari yaliyokuwa yakipambania mwanya wa kupita pale ilikuwa ni gari flani nyeupe nadhan n v8 ile.

Kwa mbanano ule ni dhahiri kuwa hapakuwa na nafasi ya kutosha kuipitisha gari ile pasi na kuikwaruza. Ndani ya gari ile alikuepo mwanamama ambaye alikazana kupiga honi angalau apite zake. Mwenye ile noa alimwomba asimame kwa muda amalizie kupakia mazagazaga yake huku akiongea kwa sauti kusema "ww mama na mgari wako mkubwa umefuata nn huku uchochoroni, wenzio wa magari hayo wako barabara pana kule, sio kuja kutubanabana huku". Baada ya kusimama kwa muda yule mwanamama alifungua mlango na kushuka. Alijongea taratibu hadi ilipokuwa ile gari, akagundua kuwa haikuweza kupaki vizuri kutokana na magari na bajaji zingine zilizopaki mbele yake na kuacha nafasi ndogo ambapo ile noah haikuweza kufiti.

Kwa haraka akawaomba wahusika wa zile bajaji kufanya adjustment ili ile noa ipaki kwa ufasaha. Zoezi lilikamilika ndani ya dk 5. Ikapatikana parking space na barabara ikapitika vyema. Alirudi kwa gari yake na kuondoka zake.

Nikiwa na maswali kichwani, kuwa yule ni nani alovaa ujasiri ule wa kufanya vile, nilimsikia raia mmoja akisema ni ACP yule, anaitwa Stella. Kwa akili yangu ya haraka nikavuta taswira ya response ya Polisi wa kibongo kwa sinario ile nikajikuta namwonea huruma mmiliki wa ile noa, mana angeishia kituoni na vifaini kadhaa. Ila mama yule aliamua kuwa askari wa barabarani kwa kutoa mwongozo.

Nilijikuta nikimsifu kimoyomoyo.

POKEA MAUA YAKO ACP STELLA. Unastahili.
 
Wapo viongozi wenye tabia ya kujinyenyekeza nakumbuka kuna muheshimiwa mmoja aliwahi kutusaidia mara baada ya kutukuta katikati ya vijiji viwili tumempakiza shangazi kwenye baiskeli mwaka 2001 tunampeleka hospital wakati uchungu umemshika alitusaidia sana mpaka alipojifungua mtoto akamuita yeye jina la Isidory na bahati mbaya aunt alipojifungua tu alifariki kabisa akasaidia kurudisha maiti kijijini kwa gari yake
 
Asante kwa kumsifia ACP Stella,namkumbuka ni Dada mwema,mpole na muungwana tangu tukiwa Depo CCP 1998/1999. Ni Depo Mate wangu,Platoon Mate mwenzangu(Namba 26) Kombania C,Hongera ACP Stella kwa uungwana wako
 
Asante kwa kumsifia ACP Stella,namkumbuka ni Dada mwema,mpole na muungwana tangu tukiwa Depo CCP 1998/1999. Ni Depo Mate wangu,Platoon Mate mwenzangu(Namba 26) Kombania C,Hongera ACP Stella kwa uungwana wako
Imfikie tafadhali. Ajue tupo tunaotambua mchango wake
 
Asante kwa kumsifia ACP Stella,namkumbuka ni Dada mwema,mpole na muungwana tangu tukiwa Depo CCP 1998/1999. Ni Depo Mate wangu,Platoon Mate mwenzangu(Namba 26) Kombania C,Hongera ACP Stella kwa uungwana wako
Platoon number 26?

Duh!

Kama Kombania moja ilikuwa na platoon mpaka 26 mmmmmh
 
Wapo baadhi ya ma Polisi ambao upstairs wako vizuri. Akikuta na kosa ana kuelimisha kwa kuonyesha sense of human respect. Zipo takataka nyingine wao wanajua kubweka na faini
 
Back
Top Bottom