IGP Said Mwema kushitakiwa ICC

Dec

Member
Jul 13, 2011
66
26
Kama kawaida, nilikuwa napata masimulizi ya hapa na pale katika saluni – na nilisimuliwa jinsi mama daktari wa kujitolea mgiriki alivyofariki dunia, jijini Dar, chanzo na mtiririko wa matukio.Hii ni simulizi na si habari iliyothibitishwa. Kwa kifupi mama huyu mgiriki alikuwa anatembea Ali Hassan Mwinyi Road na vibaka walipita na gari na kuvuta begi lake la mgongoni (back pack) na kumburuza mita kadhaa na gari. Hatimaye walichukua begin a kumwacha huyu mama. Sehemu hii imethibitishwa – ni kweli ilitokea. Ila sasa nilichoendelea kusimuliwa ni kuwa wagiriki wenzake walihangaika tokea saa 12jioni hadi saa 2 usiku wakijaribu kupata form ya polisi – kwani bila hiyo fomu hupokelewi hospitalini. Walifika hospitali ya Aga Khan saa 2 lakini pamoja na kujitahidi kwa madaktari wenzake wagiriki (ambao waliamua kuingia katika harakati za kumwokoa) lakini mama huyu alifariki.Katika simulizi hii yote kilichonisikitisha ni kuwa mtu anapopata ajali ni lazima apate fomu ya polisi kabla ya kutibiwa! Hii si sawa! Nimewahi kushauriwa na polisi afisa mmoja na hata leo saluni walinishauri “Ukikuta mtu kagongwa barabarani, usihangaike kusimama. Utasumbuliwa na unaweza ukakuta kesi inakugeuka” Hii haiingi akilini! Hivi kweli tumefikia hatua ya kuacha binadamu wenzetu wakivuja damu barabarani kwa sababu ya sheria mbovu? Hivi kweli tumeshindwa kushinikiza bunge, serikali nk kwamba sheria hii ibadilishwe! Mtu ambaye amepatwa na ajali hata awe mhalifu ana haki ya kupata huduma ya kwanza! Na mtu yeyote asibugudhiwe atakampomfikisha mtu aliyejeruhiwa hospitalini, bali waendelee kuchukua maelezo yake huku mgonjwa akiendelea kupata huduma ya kwanza. Okoa maisha kwanza! Suala hili mi binafsi nitalifuatilia lakini naamini ni jukumu letu sote kuhakikisha sheria hii inafutwa na badala yake uwekwe utaratibu mzuri ambao utathamini maisha ya mwananchi wa Tanzania, kuliko kesi ya polisi. Sheria hii ni mbovu na inapaswa kupigwa vita kwasababu watanzania wengi wamepoteza uhai wao kwasababu ya sheria hii... nashauri mwanasheria mkuu,i.g.p na viongozi wote mkae chini muitafakari upya hii sheria bila sivyo TUTAWASHITAKI DEN HAAG UHOLANZI
 
Yaani uandishi wako kama ndiyo umetoka std 7 na kujiunga shule ya kata. Huna connection kabisa ya stori na kushitakiwa kwa IGP S. Mwema. Jiandae kuvurumishiwa matusi kwa kupotezea watu muda wao kusoma mivuke.
 
Nime wahi kumuokota mtu pale M Tower akiwa hoi baada ya ajali nilifika naye Polisi Obay Ila kupata PF 3 it took me like 40 minutes hadi tukagombana Kijana yule alikaa ICU for a month but later alipona so naelewa mapungufu haya ya polisi
 
Kule wanashitakiwa watu waliopanga na kutekeleza ukatili vidi ya binadamu mfano mauaji ya Zanzibar.
 
Ila naona tuanzishe thread mpya kaibisa kuhusu huu wizi wa maeneo ya mjini kwa magari. Na kwa taarifa usipite eneo la Gymkana kwa miguu hata kama mko kumi kuna kundi la watu kama 20 hivi wananyanganya vitu na polisi wana jua. Any way ngoja nijipange nipate data za kutosha tuanzishe hii kitu hapa na wale ambao ndugu zao wameshakumbwa watashea then tuombe watu wa magazeti watupelekee huko kwa habari. It is shameful to this dhaifu country now. My lovely Tanzania.
 
kuna uhusiano wowote na attack iliyofanyika kwa watanzania nchini ugiriki?
 
Kuna kundi la vijana wa kiarabu/wahindi wanaofanya wizi huu wa kutumia magari katika barabara za upanga i.e Ali Hassan Mwinyi Road, Regency Hospital etc. Daktari wa Kigiriki na wanafunzi wake walikuja kwa ziara hapa nchini na walikuwa wamefikia Hotel ya Palm Beach na walikuwa wanatembea kwenda kwenye Kanisa la Kigiriki karibu Hellenic Club walipovamiwa na hao wezi. Baada ya tukio hili la aibu na la kusikitisha walikatisha ziara hiyo na kurudi kwao. Pia inasemekana polisi wanawafahamu wezi hao lakini hawachukui hatua.
 
Yaani uandishi wako kama ndiyo umetoka std 7 na kujiunga shule ya kata. Huna connection kabisa ya stori na kushitakiwa kwa IGP S. Mwema. Jiandae kuvurumishiwa matusi kwa kupotezea watu muda wao kusoma mivuke.
did you understand the contents? if yes,message delivered n thanx. If no please edit it, put everything you want on it n come with a very good title.
 
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya heading na Contents. Kuipa hii thread heading hiyo si sahihi... Mwema ashitakiwe ICC kwa lipi kati ya hayo uliyoyaeleza?
 
Dec!

Mbona kama vile haujasomeka ktk post yako iende sawa na heading uliyoangusha humu?

IGP kushitakiwa bado sijaona sbb ktk post yako,ingali ana yake mengi sana lakini bado haujasomeka!

Rudi upya tafadhali!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom