IGP: Polisi tumejipanga (Sensa 2012) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP: Polisi tumejipanga (Sensa 2012)

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by abdulahsaf, Aug 25, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  25th August 2012


  • Wananchi washiriki bila wasiwasi
  • Watakaovuruga kukiona cha moto

  Jeshi la Polisi nchini limesema litapambana na kuwachukulia hatua kali watu watakaojihusisha kuvuruga zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza usiku wa kuamkia kesho.

  Hatua hiyo inafuatia baadhi ya vikundi vya dini kusambaza vipeperushi vinavyowakataza waumini wao kushiriki katika zoezi hilo.

  Tamko hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja, na kuhakikishia wananchi kuwa wamejipanga kufanya ulinzi wa kutosha.

  Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, alisema kuna baadhi ya vikundi vichache visivyopenda maendeleo ya taifa kwa kutaka kuvuruga zoezi la hilo na kuwatahadharisha kuwa hawatafanikiwa kwa kuwa wamejipanga ili amani isivurugwe.

  Alisena lengo kuu la sensa hiyo ni kujua idadi ya watu nchini na kukusanya taarifa muhimu kwa ajili ya maendelo ya nchi.

  Alisema kutokana na umuhimu wa jambo hilo nchini, jeshi la polisi linawaomba wananchi wote kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo bila hofu wala wasiwasi kwa vile ulinzi utaimarishwa sehemu zote kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu.

  Alisema jeshi la polisi halitawavumilia watu wachache ama kikundi cha watu kitakachoonekana kuwashawishi watu wasishiriki zoezi hilo au wanaotaka kutumia mwanya huo kuvuruga amani na usalama ndani ya nchi.

  "Vitendo vyovyote vitavyoashiria kuwatishia, kuwazuia au kuwaletea fujo makarani na wasimamizi wa sensa ili kuwazuia wasitimize wajibu wao havitavumiliwa ni vyema wote tukaheshimu sheria za nchi pasipo kusubiri hadi ushurutishaji ufanyike," alisema Chagonja.

  Alisisitiza kuwa "Tunapenda tuwahakikishia wananchi wote kwamba tumejipanga kuhakikisha kwamba tunadhibiti vitendo vyovyote vitakavyoashiria ukiukwaji wa sheria na kuzuia mchakato wa sensa kufanyika," alisema.

  Hata hivyo, aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu za watu ama kikundi chochote kinachopanga mipango ya kuzuia ama kuleta fujo katika zoezi hilo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.

  Alisema kitendo cha mtu kuzuiliwa kushiriki zoezi la sensa ni kumkosesha haki yake ya msingi hivyo, jeshi la polisi halipo tayri kuvumilia suala hilo.

  Naye, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina Robert Manumba, alisema jeshi lake limeendelea kufuatilia kwa umakini mchakato wa maandalizi ya sensa katika kutambua wahalifu.

  Alisema kuna watu waliokamatwa kwa ajili ya kuzuia watu wasishiriki zoezi hilo ambapo hakuwa tayari kueleza idadi kamili.

  WANAOPOTOSHA ZOEZI LA SENSA KUKIONA
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya vyombo ambavyo vinaendelea kupotosha zoezi la sensa linalotarajia kuanza usiku wa kuamkia kesho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Sadiki alisema kuwa, vyombo hivyo vinakiuka sheria na havina vibali toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
  Sadiki alisema zoezi hilo la sensa sio la mtu mmoja wala kikundi fulani bali ni suala la Watanzania wote bila kujali dini, rangi na kabila.

  "Zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya wenzetu ambao wanapinga kuhesabiwa, nawasihi wanaohamasisha na wanaohamasishwa kuacha hujuma hiyo mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuiingiza nchi katika msuguano usio na tija," alisema.

  Sadiki alisisitiza kuwa, zoezi hilo lipo kwa mujibu wa sheria namba 1 ya Takwimu ya mwaka 2002 hivyo kwa yeyote atakayekaidi au kukwamisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  Akikumbushia kuhusu zoezi hilo jinsi litakavyofanyika, Sadiki alisema siku hiyo karani wa sensa atafika katika kaya akiwa na dodoso la sensa na kuliza maswali ambayo yatajibiwa na mkuu wa kaya au mwanakaya mwingine.

  Alisema karani huyo atakuwa na kitambulisho na sare maalum zitakazomtambulisha na ataongozana na kiongozi wa eneo husika.

  Pia alitaja madhumuni ya sensa kwa mwaka huu kuwa ni kukusanya takwimu sahihi za uhakika ili ziweze kutumika katika kiwango cha maendeleo kinachotakiwa pamoja na kuandaa miongozo itakayotayarisha mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu.

  Kadhalika, amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa kitendo cha kuhamasisha wananchi katika kushiriki zoezi hilo.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Saalam, Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusiana na mabango yaliyoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislam kupinga kuhesabiwa, alisema wamejipanga kwa yeyote atakayevunja sheria.

  "bosi wangu ameshatoa taarifa leo (jana) juu ya zoezi zima la sensa, nachoweza kusisitiza kwenye hili, yeyote atakayeenda kinyume tutamchukulia hatua kama alivyosema IGP Said Mwema," alisema.

  SHEIN AHIMIZA WAZANZIBARI

  RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka Wazanzibari kujitokeza kuhesabiwa kwenye sensa ya watu na makazi kwani sensa ni muhimu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo iliyoandaliwa na serikali kwa watu wake.

  Dk. Shein alitoa wito huo jana katika taarifa kwa umma aliyoitoa kupitia vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa wananchi kushiriki sensa.

  Alisema si jambo la kufurahisha kusikia kuwa baadhi ya watu wanawashawishi wengine wasishiriki sensa bila ya kutoa sababu za msingi.

  Alisema historia inaonyesha kuwa Wazanzibari kwa kipindi kirefu wamekuwa wakishiriki sensa ikiwemo ya mwanzo iliyofanyika mwaka 1948.

  Aliwataka kuzingatia kuwa sensa haina uhusiano na matakwa ya watu binafsi bali inalenga kuleta mafanikio kwa wote na kuiwezesha Zanzibar kujua idadi halisi ya wananachi wake.

  Aidha, Dk. Shein alisema sensa zote ni muhimu, lakini sensa ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa taarifa zitakazokusanywa zitatumika kufuatilia na kutathmini mpango wa serikali wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

  Dk. Shein alisema kuwa taarifa kutoka Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo zimebainisha kuwepo na mafanikio makubwa katika kukuza uchumi katika kipindi cha miaka miwili iyiliyopita.

  Alieleza kuwa pato la jumla la mtu binafsi limeongezeka kutoka wastani wa Sh. 782,000 mwaka 2010 hadi kufikia Sh. 960,000 mwaka 2011. Aidha, taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia 6.8 katika mwaka 2011 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya mwaka 2010.

  Aliwataka maofisa wa sensa kufanyakazi kwa bidii na nidhamu kuhakikisha kazi hiyo inafanikiwa na matokeo yake yatumike kwa maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

  Kauli ya serikali umekuja siku mbili tangu Jumuiya ya Uamsho naMihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMUKI) kuwataka wafuasi wake kususia sensa hadi serikali itakapoondoa urasimu katika upatikanaji wa vitambulisho vya Uzanzibari Ukaazi na kuhakikisha waliopewa bila kuwa na sifa wanavirejesha.

  VIPEPERUSHI VYASAMBAZWA

  VIPEPERUSHI vyenye maelezo ya kupinga zoezi la Sensa vimesambazwa kwa wingi jijini Dar es Salaam, ambapo kati baadhi ya ujumbe uliokuwemo unawataka waumuni wa dini ya Kiislamu kutoshiriki zoezi hilo.

  Usambazaji wa vipeperushi hivyo umefanyika majira ya alfajiri ya jana katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Segerea, ambapo wakazi wake wameshangaa kuona vipeperushi pembeni ya nyumba zao kipindi cha asubuhi bila kujua nani aliyevisambaza.

  Moja ya Kipeperushi ambacho Gazeti hili imefanikiwa kukipata, kimeonekana kuwa na kichwa cha habari 'Dira yetu', Waislamu hawatashiriki Sensa", imebainika kuandaliwa na watu wanaojiita Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania.

  Mwenyekiti wa Mtaa Ugombolwa Mariam Machicha alisema wakazi wa eneo lake walimpigia simu majira ya alafajiri wakimueleza kuna watu wamesambaza vipeperushi hivyo mitaani kwao na kusababisha hofu kwa wakazi hao.

  Maeneo mengine yaliyoripotiwa kusambazwa maratasi hayo kuwa ni Kiwalani minazi mirefu na maeneo ya Vingunguti.

  Alisema baada ya kufika eneo hilo, alikuta vipeperushi hivyo vikiwa vimekusanywa na wananchi hao, ambapo alichukua utaratibu wa kutoa ripoti katika ngazi za juu ili watu waliofanya kitendo hicho wachukuliwe hatua.

  Aidha baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema kitendo hicho cha kusambaza makaratasi hayo haikufanywa na watu wanaoishi eneo hilo, kwa sababu toka mwanzo waumini wa dini hiyo kwenye eneo hilo hawakuwa sehemu ya wanaopinga.

  TAASISI ZA KIISLAMU KUANDAMANA JUMATANO IJAYO
  JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimesisitiza kutoshiriki kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa madai ya kutokuwa na imani na serikali kuhusu zoezi hilo.

  Aidha, Jumatano ijayo wanatarajia kufanya maandamano makubwa kudhihirisha msimamo wao na kupinga zoezi la matumizi ya nguvu dhidi yao.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu wa jumuiya hizo, Ponda Issa Ponda aliyefuatana na baadhi ya viongozi wa jumuiya hizo, wakiwemo mashekhe, alisema kuwa kuna sababu nne kuu zinazowafanya wasishiriki zoezi hilo.

  Alitaja sababu hizo kuwa ni serikali kushindwa kujenga mazingira rafiki yanayowezesha sensa na makazi kuwepo nchini, Mfumo wa sensa nchini hauwezeshi madhumuni ya sensa kufikiwa, Sensa ili iwe Sensa ni lazima iwahesabu watu wote husika na zoezi la Sensa Tanzania limegubikwa na propoganda na matumizi ya mabavu.

  Akitoa tamko lao kwa niaba ya jumuiya hizo, Ponda alisema kuwa zoezi la Sensa linalotarajiwa kuanza Agosti 26, sio zoezi lenye misingi ya haki na ukweli.

  "Chini ya uongozi wa Mabaraza na Jumuiya zetu zisizo pungua 30 tumejiandaa ipasavyo kutoshiriki zoezi hilo, tunaishauri serikali kuahirisha kile wanachokiita sensa ya watu na makazi ili kuuepusha ufisadi mkubwa wa fedha za umma ili kujenga fursa ya kuweka misingi bora katika zoezi la sensa, vilevile tunalaani propaganda na matumizi ya nguvu dhidi ya Waislamu.

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari Katibu Ponda alieleza kuwa serikali inapotosha ukweli na kusisitiza hawatashiriki sensa kwa asilimia 100.

  Alisema matamko yanayotolewa ni hila na propaganda zinazofanywa na baadhi ya watu ili kupotosha ukweli.

  Alisema serikali itakuwa imepoteza bure pesa za wananchi kwani wanaamini kuwa sensa hii siyo kwa maslahi ya taifa bali watu binafsi na kawaida ya serikali kutenga mafungu makubwa tofauti na matumizi yake katika shughuli husika mfano uchaguzi ama zoezi kama hilo ni kwa faida ya watu binafi.

  Akizungumzia kuhusiana na kipengele cha dini, Ponda alisema kuwa wanashangazwa na kitendo cha serikali kutoweka kipengele cha dini wakati nchi ya Rwanda wamekiweka kipengele hicho.

  "Tanzania imeshindwa, kwa nini inapata kigugumizi? Hakika zoezi hili linafanyika kwa maslahi binafsi, serikali imekuwa ikiwabana BAKWATA kila mahali," alisema.

  SHEIKH MSHINDO AHIMIZA WASHIRIKI SENSA
  WAKATI viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, zikiendelea kuwahimiza waumini wa dini hiyo kususia zoezi la Sensa, Sheikh Mkuu wa Temeke, Sheikh Mohammed Mshindo Kingo, amewahimiza Waislam kushiriki zoezi hilo kwa wingi.

  Akiwahutubia waumini wa Msikiti wa Kizuiani, Mbagala, Sheikh Mshindo, alisema Waislam wanapaswa kushiriki na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa Sensa ili kuonyesha ukomavu na ustahimilivu wao.

  Alisema ni kweli Waislam wamekuwa na madai ya msingi dhidi ya dhuluma wanazofanyiwa na serikali, bado hawana sababu ya kuigomea Sensa na kusisitiza ni wajibu waislam wajitokeze na kuishiriki bila kuacha.

  Alisema kama kutaka mabadiliko ya msingi kwa manufaa ya dini yao ni wajibu wao kushiriki kwa wingi katika uchangiaji wa mabadiliko ya katiba wakati wakiwa pia wameshiriki Sensa inayoanza kesho nchini nzima.

  Sheikh Mshindo, alisema suala la kuhesabiwa ni sehemu ya ibada kwa vile limewahi kufanywa hata na Mtume Muhammad (SAW) hivyo hakuna maana ya kususia kwani inaweza kuletwa vikwazo katika harakati zao za kutaka kuona haki dhidi yao zikifanyika kupitia mabadiliko ya katiba mpya ijayo.

  Kauli hiyo ya Sheikh huyo wa Temeke, imekuja wakati uongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, zikiendelea kuhimiza mgomo dhidi ya Sensa na kukanusha taarifa zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba wameridhia kushiriki sensa hiyo bila tatizo.

  WATANO MBARONI KWA KUKUTWA NA VITABU NA VIPEPERUSHI VYA KUPINGA SENSA

  JESHI la Polisi mkoani Tanga linawashikiliwa walimu wa dini ya Kiislamu watano kwa tuhuma za kukutwa na vitabu na vipeperushi vinavyowakataza waumini wa dini hiyo wasishiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26.

  Hatua hiyo inafuatia siku chache tu baada ya NIPASHE kuripoti kuwepo kwa kundi la watu mkoani hapa ambalo linasambaza vitabu na vipeperushi vinavyowataka wananchi kutoshiriki zoezi hilo.

  Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Jaffari Mohamed, alisema watu hao walikamatwa katika eneo la Mtimbwani wilaya ya Mkinga Agosti 22, mwaka huu majira ya saa 2.30 usiku wakiwa katika harakati za kuhamasisha na kugawa vitabu na vipeperushi hivyo vinavyowakataza waumini wa dini ya Kiislamu kutoshiriki zoezi hilo.

  Mohamed aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Chambuso Ramadhan (37), Kassim Mbarak (31), wote wakiwa ni wakazi wa Chuda, Hamad Mohamed (34), Mwalimu wa dini na mkazi wa Mabawa, Hussen Idd (36), dereva ambaye pia ni mkazi wa Mabawa.

  Alisema mmoja kati yao Fadhil Chambo (26) ni mwalimu wa dini na mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Kaimu Kamanda huyo watuhumiwa hao wanadai kufanya hivyo kwa lengo la kutetea haki za Waislamu ambazo zinakiukwa na serikali ikiwemo kutaka kuwepo kwa kipengele kinachoainisha dini ya mtu katika madodoso ya sensa.

  Alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa amewatahadharisha wakazi wa mkoa huo kuwa makini na wajanja wachache ambao watataka kutumia upenyo wa zoezi la sensa ili kufanya uhalifu.

  Gallawa ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga alisema kimsingi zoezi hilo litafanyika nyakati za mchana na makarani wataongozana na viongozi wa maeneo husika kupita katika kila kaya hivyo wananchi wasiruhusu mtu yeyote atakayefika kwenye eneo lao kwa madai kuwa yupo kwenye zoezi hilo kama hana utambulisho wa viongozi.

  DC: WANAOKATAA SENSA WAZOMEWE, KUCHAPWA BAKORA


  MKUU wa Wilaya ya Kilwa,Abdala Ulenga amewataka wananchi kuwachapa bakora na kuwazomea wanaowashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi.

  Akizungumza kwa nyakati tofauti na wasimamizi, makarani wa sensa waliopo kwenye mafunzo ya yanayoendelea katika vituo vya Mandawa, Njinjo, Ulenga alisema kuwa watu hao wanaotumia mgongo wa dini ya Kiislamu wanapotosha na kueleza kuwa hakuna sehemu yoyote ya kitabu cha Korani kinachokataza Waislamu wasihesabiwe.

  " Watu hawa wanaojifanya mashehe uchwara ni wapotoshaji naomba mkiwaona waulizeni ni sehemu gani ya kitabu kitukufu cha Korani au hadithi za Mtume zinapokataza Waisilamu wasihesabiwe?"alihoji mkuu huyo wa wilaya na kuwataka wasimamizi na makarani hao kuwaeleza wananchi umuhimu wa kuhesabiwa.

  Alibainisha kuwa wapo watu ambao wanapita kwenye baadhi ya misikiti hapa wilayani ambao wakiwashawishi Waisilamu kutojitokeza kuhesabiwa kwa madai ya kutokuwepo kipengere kwenye madodoso kinachohoji dini ya mtu na kueleza kuwa hakuna uhusiano wowote wa dini na kuhesabiwa kwani lengo la serikali la kuendesha sensa ni kuwezesha kupanga mipango ya maendeleo na kutumika kwa takwimu na wadau mbalimbali maendeleo ya ndani na nje ya nchi.

  "Lengo la Serikali si kujenga misikiti wala makanisa na ndio maana kwenye dodoso litakalotumika halikuweka kipengere haitaki cha hali ya dini kwani kama jukumu la ujenzi wa misikiti na makanisa haliwahusu," alisema Ulega.

  Alisema kuwa suala la kuhesabiwa ni la kisheria na kuwa yeyote ambaye kwa makusudi hatajitokeza kutohesabiwa atachuliwa hatua za kisheria kwani serikali imetumia kiasi kikubwa cha fedha ili kufanikisha zoezi hilo.

  Hata hivyo amewataka wasimamizi na makarani hao kutowalazimisha watu watakaokaidi kuhesabiwa na badala yake watoe taarifa kwa viongozi wa sehemu husika ili serikali iwachukulie hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria.

  MAWAZIRI WAONGEZA NGUVU

  SERIKALI imelazimika kuwatuma baadhi ya mawaziri wake, kuzunguka kwenye majimbo ya uchaguzi kwa lengo la kuwaomba viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao kushiriki katika zoezi la Sensa.

  Katika mkoa wa Iringa, tayari serikali imetoa tamko zito ikikemea vitendo viovu vya baadhi ya watu wanaoendelea kusambaza vipeperushi vinavyowataka wananchi wasishiriki katika zoezi hilo litakaloanza usiku wa kuamkia kesho.

  Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa yupo katika jimbo la Kalenga akizunguka kata kwa kata kwa ajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na kuziomba jumuiya za madhehebu ya kidini kutokwepa wajibu wao wa kuwahimiza waumini wao kukubali kutoka na kuhesabiwa.

  Akiwa katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya Ilalasimba, Magubike na Kidamali, Dk. Mgimwa alisema kuwa nia ya serikali kufanya sensa hiyo ya watu na makazi, lengo lake ni kuhakikisha umma mpana wa watanzania una hudumiwa kwa idadi halisi ya watu, kuyatambua makundi maalumu, makazi pamoja na kutoa huduma kwa kutumia takwimu zisizo sahihi.

  "Nawaomba sana viongozi wangu wa jumuiya za kidini popote pale mlipo, tusaidiane na serikali yetu kuhamasisha wananchi wanaojitokeza kuhesabiwa kwa sababu tunataka kuachana na takwimu za kubuni buni, tunataka kuachana na utoaji wa huduma usiozingatia uhalisia wa idadi ya watu na makundi ya jamii…Kwa hivi, ndiyo maana tunawaomba viongozi wa dini na wazee wa mila mtusaidie ili tupate ukweli kuhusu idadi ya wananchi wa Tanzania,"alisema Dk. Mgimwa.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi yupo katika jimbo la Isimani akifanya shughuli za uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwa lengo la kuisaidia serikali kufanikisha zoezi hilo kwa mafanikio.

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma amewataka watu ambao wameanza kusambaza vipeperushi vinavyolenga kuhujumu zoezi hilo kuacha mara moja kazi hiyo, kwa kuwa serikali haitakubali kuona zoezi hilo likihujumiwa.

  Dk. Ishengoma alitoa tamko hilo wakati akizungumza katika ziara yake ya kuhamasisha wananchi wa Vijiji vya Kising'a, Nyang'oro, Mahuninga na Ikengeza juu ya kushiriki wao katika zoezi hilo.

  "Tunazo taarifa za kundi la watu ambao wameanza kulihujumu zoezi hilo kwa kusambaza vipeperushi ambavyo vinawataka wananchi wasishiriki zoezi hilo. Hatutakubali kuona baadhi ya watu wasio waadilifu wakihujumu zoezi hilo ili lisifanikiwe.

  Aliwataka wanaume kuacha mila potofu ya kuwazuia wake zao kutoa taarifa za kaya pindi wasipokuwepo nyumbani na badala yake wawaruhusu watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi wakati makarani wa sensa watakapofika kwenye nyumba zao.

  ARUSHA KUENDELEA KUSHAWISHI WANAOKATAA
  MRATIBU wa Sensa Mkoa wa Arusha, Margreth Martin, amesema bado anaamini kuwa elimu zaidi inahitajika kushawishi watu wanaokataa kuhesabiwa kwa sababu za imani za kidini badala ya kuwachukulia hatua za kuwashtaki na kuwafunga.

  Alisema ingawa sheria inatamka kwamba watu wanaokataa kuhesabiwa wanaweza kushtakiwa mahakamani, lakini hakuna sababu ya kufanya hivyo, isipokuwa kinachotakiwa ni kuendelea kutoa elimu ili kuwashawishi waweze kuhesabiwa.

  Alikuwa akizungumzia changamoto inayoikabili kazi ya sensa ambapo baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wametangaza hawana mpango wa kuhesabiwa.

  Katika hatua nyingine, mpango wa kutumia helikopta (chopa) kufanikisha zoezi la sensa kwa baadhi ya maeneo wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, umesitishwa na badala yake zitatumika pikipiki baada ya kutengezwa kwa barabara.

  Awali Mratibu wa Sensa Mkoa wa Arusha, Margareth, alisema kutokana na baadhi ya maeneo wilayani humo kutopitika vizuri kwa magari, walikuwa na mpango wa kutumia chopa kurahisisha kazi ya makarani na wasimamizi wa sensa kuhesabu watu.

  Hata hivyo, alisema jana kuwa baada ya kufanyiwa matengenezo ya barabara wamepata pikipiki 22 zitakazotumika kwa makarani na watumishi kwenye maeneo ambayo awali yalikuwa magumu kupitika.

  Pia alisema Wilaya ya Karatu nayo itatumia pikipiki badala ya chopa na hadi sasa imefanikiwa kupata pikipiki 17 zitakazotumika pamoja na magari ya halmashauri kwa kazi hiyo.

  Alisema idadi ya makarani wote mkoani hapa, ni 4,835 ambao pamoja na watumishi wanafanya idadi yao kuwa ni 5,057 ambayo alisema inatosha kufanikisha kazi hiyo.

  Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha, alisema makarani na watumishi waliokwishapatikana kwa ajili ya sensa ni 1,020.

  Kuhusu vifaa, alisema vitaletwa na chopa ya jeshi kutoka Dar es Salaam, na hakuna tatizo la fedha kwa wilaya zote ili kufanikisha kazi hiyo.

  WANASEMINA 30 WA SENSA WAGOMA KUAPISHWA


  WANASEMINA wa Sensa 30 wa Kata ya Mahembe mkoani Kigoma wamegoma kuapishwa kwa madai ya kutolipwa fedha zao za nauli.

  Wakizungumza na NIPASHE jana katika ukumbi wa semina uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mgawa huko Mahembe, walisema "sisi hatuwezi kukubali kuapishwa wakati hatujalipwa fedha zetu za nauli, zoezi lenyewe linaanza Agosti 26, tukikubali kuapishwa hizo fedha tutalipwa lini, kama wanataka kutuapisha watupatie fedha zetu za nauli," alisema mmoja wa wanasemina hao.

  Walisema kuwa, vifaa vya kuwekea madodoso hakuna, mpaka sasa wamepewa sanduku moja, dodoso 30 na fomu moja ya namba 15, hakuna sare wala begi la kubebea madodoso kitendo kinachowafanya washindwe kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

  Kwa upande wake Mratibu wa Sensa, Wilaya ya Kigoma, Salome Mboye, alithibitisha kutowalipa wanasemina hao nauli ya siku moja na kudai kuwa fedha hizo hazijafika.

  Mboye alisema changamoto zinazowakabili ni usheleweshaji wa fedha wakati wa mafunzo pamoja na vifaa vya sensa kutotosha na vingine kutofika itafanya zoezi hilo kuwa gumu kutokana na vifaa hivyo kuwa vidogo.

  DC MWANGA AHIMIZA ZOEZI
  MADIWANI wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo katika kata zao na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kuhesabiwa na kutoa ushirikiano na makarani wa sensa siku ya zoezi hilo.

  Akizungumza wakati wa kufungua semina kwa madiwani wa halmashauri hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo Shaibu Ndemenga, alisema madiwani wanayo nafasi kubwa ya kuwahamasisha wananchi na kushirikiana na makarani katika kufanikisha zoezi hilo.

  Alisema kutokana na sababu hiyo ni vyema wakawaelimisha watendaji hao kuwa na subira kwani fedha zao zipo na watalipwa japo itachelewa lakini haitapita muda wa wiki moja kuanzia wiki hii wakati kamati ya sensa Taifa ikifanya utaratibu wa namna ya kuwalipa watendaji hao.

  Pia aliwataka madiwani hao kufahamu kuwa zoezi la sensa halina uhusiano wowote na dini kwani serikali haina dini nani vyema wananchi wakawapuuza wale wote wanaoeneza uvumi mbaya juu ya kushiriki zoezi hilo.

  RC MAHIZA KUTOWAFUMBIA MACHO WATAKAOGOMA

  MKUU wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza amesema uongozi wa mkoa huo hautakuwa tayari kuwafumbia macho watakaohusika kugoma kushiriki zoezi la kuhesabiwa.

  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mahiza alisema kuwa muda wa kubembelezana umekwisha na sasa ni muda wa kufuata sheria atakayebainika anakwamisha zoezi hilo kwa makusudi sheria itachukua mkondo wake.

  Mahiza ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kali kwa baadhi ya viongozi wa wadini wanaodaiwa kuwakataza waumini wao wasihesabiwe kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na atafikishwa mahakamani mara moja.

  Aidha alisema katika kipindi hiki cha miaka kumi iliyopita tangu sensa ifanyike ni dhahiri kumekuwepo na ongezeko la watu hivyo huduma mbalimbali zinazohitajika zitolewe na selikali ni lazima idadi ya watu ijulikane.

  DODOMA WALALAMIKIA VIFAA
  MAKARANI wa sensa katika wilaya ya Dodoma mjini wamelalamikia kutopatiwa vifaa vya kufanyia kazi hadi siku ya jana wakati ikiwa imebaki siku moja kabla ya kuanza kwa zoezi la kuhesabu watu.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na NIPASHE, walidai kuwa licha ya kuahidiwa kukabidhiwa vifaa hivyo Agosti 22, mwaka huu siku ambayo waliripoti katika vituo vyao hadi jana vifaa hivyo vilikuwa havijafika katika kata zao.

  Mmoja wa makarani hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema vifaa ambavyo bado hawajapatiwa ni pamoja na penseli, vifutio, vichongeo, madodoso na mageresho.

  Alisema kwa upande wa sare kama vile fulana na kofia bado hawajapewa hivyo wanashindwa kuelewa watafanyaje kazi bila sare.

  Alisema hali hiyo inaweza kusababisha watu kutotoa takwimu sahihi kwa kuwa hawata waamini kuwa ni makarani.

  Alieleza kuwa vifaa walivyopewa hadi sasa ni vile ambavyo vilibaki wakati wa semina kama vile madodoso ya kijamii ambayo yanatakiwa kujaza huduma za kijamii zilizopo katika maeneo yao.

  Pia karani mwingine, alisema mbali na suala la vifaa pia hata fedha hadi jana walikuwa hawajapewa licha ya kuripoti katika vituo vyao toka Agosti 22.

  SIMIYU: MAKARANI HAWAJALIPWA

  KUNA dalili za kudorola kwa kwa zoezi la sensa katika mkoa wa Simiyu kufuatia makarani kudaiwa kufanya kazi hiyo kwa shingo upande baada ya kutolipwa posho zao.

  Habari zilizo patikana katika wilaya za mkoa wa Simiyu zimedai kuwa makarani wengi licha kufika maeneo waliyopangiwa wanadaiwa huenda wakafanya kazi hiyo kwa kulipua tu kwa vile baadhi yao hawajalipwa posho zao licha ya ofisi husika kuahidi kuwa watalipwa.

  Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao katika vyombo vya habari wamedai kuwa inashangaza kuona kuwa katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na tofauti kubwa ya malipo kati ya wakufunzi wamakarani wa sensa katika maeneo yao ikiwemo mikoa ya kanda ya ziwa na Simiyu.

  *Taarifa hii imeandaliwa na Beatrice Shayo, Romana Mallya, Moshi Lusonzo, Fransisco Haule, Badru Kimwaga, Dar es Salaam, Mwinyi Sadallah, Zanzibar, Lulu George,Tanga, John Ngunge, Arusha, Godfrey Mushi, Iringa, Mariam Maregesi, Kilwa, Joctan Ngelly, Kigoma, Charles Lyimo, Mwanga, Margaret Malisa, Pwani, Augusta Njoji, Dodoma na Anceth Nyahore, Simiyu

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hivi mkuu mzima wa polisi hawezi kuvaa uniform nzuri jamani akaonekana kweli ndio top wa polisi?
   
 3. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hawana lolote,walisema hivyo hivyo wamejipanga kuzuia maandamano ya CHADEMA Arusha lakini watu wakaandamana walivyoumbuka wakaanza kuua watu wasio na hatia kwa kutumia risasi za moto na mabomu ya kutupa kwa mkono.
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,807
  Likes Received: 2,581
  Trophy Points: 280
  Mwanzo nilidhani mgambo wanaruka na kukanyagana.
   
 5. hendeboy

  hendeboy JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi niko tayari kuhesabiwa ila dodoso liwe fupi maana dodoso refu litanichosha
   
 6. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ni kukaa mkao wa maana kuangalia sinema hii once again.
   
 7. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa mkoa wa Dar-res-laam. Usiwe muoga wa kusema hali halisi. Eti baadhi ya wenzetu hawataki kuhesabiwa. Kwa nini unaogopa kusema wazi? Kwamba baadhi ya WaIslam hawataki kuhesabiwa. Huu ni wakati wa uwazi na ukweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kauli makini! inaisuta serikali kuwa haikutoa elimu madhubuti kuhusu sensa kwa raia wake, badala yake inatumia nguvu.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Aje atuambie ya Dr Ulimboka au kamuachia Kova yeye anaongea vitu Rahisi tuu?
   
 10. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Afadhali yeye anyewaita Waislamu wenzake "wenzetu" ingawa wametofautiana naye kuhusu suala la sensa kuliko Mufti anayewatoa Waislamu wenzake kwenye Uislamu na kuwaacha waitwe makafiri kwa sababu tu hawakubaliani naye kuhusu suala la Kadhi aliyemchagua.
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Najisikia raha sana fainali imekaribia...(serikali/jeshi la polisi/BAKWATA) vs (Shehe Ponda/Taasisi za Kiislam).
  Itanoga zaidi kama serikali ikiongeza safu yake ya ulinzi kwa kulijumuisha jeshi la wananchi tanzania...
   
 12. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona na wewe unagoma? Hivi ni kweli kwa kushinda kote humu Jf bado hujapata hata kaelimu kadogo ka sensa?
   
 13. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Ha, ha, ha, haa! Jeshi la wananchi Tanzania linasubiri mechi yake na wa-Malawi ambayo tarehe yake bado haijapangwa. Ambayo itafanyika katika viwanja vya ziwa Nyasa/malawi.
   
 14. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Waichukulie mechi hii kama ya kujipima nguvu kabla ya mtanange na wamalawi tuone wakina shehe ubwabwa watatokea wapi...
   
 15. M

  Mbofu JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx to God, waliotoa matamko wote ni waislam,maana hapa angeongea mkiristo yangekuwa Mfumo kiristo,eeh Mungu okoa viumbe wako mana wanaangamia kwa kukosa maarifa.
   
 16. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Khe! si mwanzo mlisema kuwa sahani za pilau tu zinatosha kuwalainisha "Mashehe ubwabwa" ? kumbe sasa linahitajika jeshi!
   
 17. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ubwabwa wameshauzoea hao...wanatakiwa wahesabiwe huku wanaruka kichurachura na kanzu zao ili iwe fundisho kwa vizazi vijavyo.
   
 18. F

  Francis Jr Senior Member

  #18
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unasahau 2001 zanzibar tulivyowachinja kama kuku. Chezeya waislamu. Ukifa katika Jihad Peponi. Unafikiri kuna muislamu anapenda kufa kizembe kitandani.

   
 19. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  teh teh! tuna historia ya kupigania haki zetu kwa zaidi ya miaka 1400 sasa!
   
 20. F

  Francis Jr Senior Member

  #20
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Safari hii Maaskofu wamelipanga draft vizuri kweli. Lakini Bado hawajaondoa maana ya MFUMO KRISTO.

   
Loading...