IGP Mwema atoboa siri ya mapolisi kushiriki ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema atoboa siri ya mapolisi kushiriki ujambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 26, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  • Atoboa uadilifu umeporomoka
  • Sasa chaanzishwa kitengo maalum
  • Asema Ze Utamu bado wanasakwa

  Jeshi la Polisi nchini lipo katika mkakati madhubuti wa kujisafisha ili kulirejeshea maadili kutokana na baadhi ya askari wake kulichafua baada ya kubobea katika vitendo vya uhalifu.

  Kupitia mkakati huo, Jeshi la Polisi linatarajia kuanzisha kitengo maalum kitakachokuwa kikifuatilia maadili ya ya askari.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, alidokeza kuhusu mkakati huo wa kuwarejesha katika maadili baadhi ya askari wake wakati akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum.

  Mwema alisema kuwa hatua ya kuanzishwa kwa kitengo hicho kinatokana na baadhi ya askari wake kukosa maadili na kujihusisha na vitendo vya kihalifu kinyume cha maadili ya jeshi hilo.

  IGP Mwema alisema hataweza kuvumilia askari wake yeyote atakayejihusisha kwa namna yoyote katika vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikilishushia heshima jeshi hilo mbele ya wananchi.

  "Kwa kawaida askari ni mlinzi wa raia, lakini pindi inapotokea anakuwa mhalifu kwa kweli maadili ya kazi yanakuwa hayapo, na mara nyingi inapotokea askari wangu anajihusisha na vitendo hivi hatua huchukuliwa mara moja ambazo ni za kukiuka maadili na baadaye hufikishwa mahakamani," alisema IGP Mwema.

  Alisema kuwa askari wote wa jeshi hilo waliodaiwa kuhusika katika matukio ya ujambazi wiki kadhaa zilizopita katika mikoa ya Mara, Mwanza, Rukwa na Arusha watachukuliwa hatua kwa mujibu wa vipengele viwili vya makosa vya ukiukaji wa maadili na makosa aliyoyafanya askari.

  Aliongeza kuwa, pamoja na kuwepo kwa kanuni za maadili, lakini baadhi ya askari wake wamekuwa wakizikiuka na kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

  Mwema alisema mkakati wa kuanzisha kitengo hicho wameamua kuuanzisha kutokana na kubainika kuwa baadhi ya askari wanajihusisha na uhalifu hivyo kurudisha maadili ya jeshi hilo.

  Alisema mkakati mwingine ni Jeshi la Polisi kuwa na uwezo wa kimafunzo katika kupanga mikakati, mbinu za kuzuia na kuthibiti uhalifu wa aina zote nchini.

  IGP Mwema aliongeza kuwa mkakati mwingine ni jeshi kuwa na mpango wa mafunzo ya maadili ambayo yatawahusisha askari wake wa vitengo tofauti.

  "Haya yote ni kuhakikisha ile dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii inaendelea kufanikiwa zaidi na jeshi linapokea taarifa mbalimbali za kihalifu kupitia wananchi wake.

  "Tunahitaji kuwa karibu na wananchi na sio kuwa maadui, ikiwa maadili hayatarudishwa, nchi itaendelea kuwa na matatizo ya kiusalama na kiuchumi," alisema.

  Hata hivyo alisema ukosefu wa uadilifu si tatizo kwa Jeshi la Polisi pekee, bali ni la taifa zima.

  "Uhadilifu unatakiwa kuanzia kwenye ngazi ya familia na maeneo mengine kama mashuleni.. inakuwa ni kurekebishana, lakini kama huko chini mtoto anakua hana maadili basi hata anapoanza kazi tabia huwa ya aina hiyo," alisema IGP Mwema.

  Katika hatua nyingine, Mwema alisema mpaka sasa Jeshi hilo halijafanikiwa kumtia mbaroni mmiliki wa Mtandao wa Ze Utamu, ambaye anatuhumiwa kuwadhalilisha viongozi kadhaa nchini.

  IGP alifafanua bado jeshi lake linaendelea kumfuatilia kwa kushirikiana na nchi nyingine kutokana na makosa ya kimtandao kuhusisha zaidi ya nchi moja.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  siasa miiingi!.....
  hamna kitu hapo
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kulindana kama kawa lazima wadumishe mila
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  sijaelewa anachosema au alichotaka kusema. Polisi hawana maadili halafu unaanzisha kitengo maalamu, imeanzishwa kanda maalumu hamna kitu, tossi kaanzisha kikosi maalumu anazunguka na helikopta na kushika wapika gongo na mangaliba, hii ya sasa itasaidia nini kama polisi hana maadili fukuza kazi basi hakuna compromise.

  mungu wangu, kumomonyoka maadili ni shauri ya ukosefu wa mafunzo kweli au ni tabia ya mtu binafsi na tamaa zetu, unataka kusema nini bwana IGP.

  Polisi shirikishi na polisi jamii ni kutokana na jeshi la polisi kutotekeleza majukumu yake sawasawa. Kama wangefanya kazi vizuri kusingekuwa na haja ya vitu hivyo.

  Jipange vizuri na polisi watekeleze wajibu wao, hamna short cut kwenye hilo.
   
 5. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #5
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IGP Mwema huko juu katika jeshi la Polisi wamejipanga vizuri kabisa na mikakati mingi yenye maana lakini wanaanguswa na huku chini chini kabisa.

  Askari polisi huku chini wanajiona mungu watu,kwa makusudi kabisa wanatesa watu, wananyanyasa watu,dhuluma waziwazi,rushwa ndio usiseme,ukienda kituoni wewe na mtuhumiwa wako wote mtalazimika kutoa rushwa lazima, lazima kabisa.
  Mimi nasema hawa polisi hawato badilika ha baada ya miaka 200,labda Bwana Yesu afufuke arudi duniania.
   
 6. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Awaongezee mishahara MARADUFU. Haina haja ya kitengo maalum.. Hicho kitengo kitatumia pesa nyingi, na hakuna lolote litakalofanyika.. ONGEZA MSHIKO, watu wako waache rushwa na uhalifu mwingine.
   
Loading...