IGP Mwema anasubiri nini kung'atuka?

IGP Mwema anasubiri nini kung'atuka?

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
WanaJF,

Kuibiwa kwa upanga wa dhahabu aliokuwa amekabidhiwa IGP Mwema kuashiria uongozi wake wa muda,ambao ni mali ya shirikisho la wakuu wa majeshi ya polisi wa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO),kumelifedhehesha na kuliaibisha Taifa!

Kutokana na uzembe uliosababisha kuibiwa kwa upanga huo wenye thamani kubwa inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 600 za kitanzania,IGP Mwema hana budi kuwajibika kwa kung'atuka madarakani bila shuruti yoyote!

Yeye kama kamanda mkuu anastahili kuoyesha mfano katika kukabiliana na adui ambaye ni uzembe,rushwa na wizi uliokithiri katika jeshi la polisi nchini na kuwapa changamoto wanaobaki nyuma yake kwani cheo ni dhamana!

Swali
:Ni nani anayeweza kuingia ofisini kwa IGP Mwema akaiba Laptop yenye mambo nyeti au upanga wa dhahabu unaotakiwa kulindwa masaa 24 na kutoka bila kukamatwa?
 
Kaka swali lako lilivo uliza,nami nna jibu hivi!Anasubiri viongozi wa chadema waseme maovu ya Polisi,na wananchi waandamane kushinikiza ajiuzuru/ang'atuke.ndipo kwa aibu kubwa tutasikia tamko lake,kupitia vyombo vya habar i.
 
Na kweli ang'atuke,maana utajiri kashaupata.,mil 600(siamini kama ameibiwa)
 
Mungu ni mwaminifu sasa policccm waseme ni chadema, mungu kawa funua wazi kwa ukatili wao.
Akamweleze shemeye jk.
 
Naona ni wakati muafaka sasa kwa yeye kwenda kufanya kazi nyingine au kupumzika
 
Huo Upanga kapiga mwenyewe!!
 
khs kuwajibika hilo halipo%.. lkn shemej yake ataagiza mgodi mmojawapo utoe panga la dhahabu jingne.. hii ndio tz bwana.
 
Ningekuwa rais ningemuhamisha nakumpeleka kuwa mkufunzi wa jk tena dodoma makitupora huko miaka miwili bila mshahara
 
Nyie mnalalama tu lakini mjue hizo millioni 600 za kufidia huo upanga mtazilipa nyinyi walipa kodi kwa uzembe wa mtu mmoja!!! Ndio mana watu wanasema bongo ni nchi tambarale!!!
 
Naona ndo kiinua mgongo chake maana nimesikia anastaafu!
Maana ipo siku tutasikia watu wameiba dayari ya raisi IKULU!
YAANI LACK OF SERIOUSNESS KABISA
ILA KWA POLISI SISHANGAI KAMA UNGA UNAYEYUKA,ASKARI ANATEMBEA NA KICHWA CHA MTU KUBAMBIKIA RAIA,ALL THESE NONESENSE WATU BADO WAKO KWA OFISI ZAO WANAKULA MISHAHARA
 
Bora kumuachia Fisi nyama unaweza ukaikuta kuliko kumuachia upanga wa mil 600 mtoto wa kichaga!
 
Na kweli ang'atuke,maana utajiri kashaupata.,mil 600(siamini kama ameibiwa)

Ni ajabu sana! Kamanda mkuu ambaye analindwa na ofisi yake inalindwa masaa 24 anaibiwa kirahisi rahisi namna hiyo!
 
Kaka swali lako lilivo uliza,nami nna jibu hivi!Anasubiri viongozi wa chadema waseme maovu ya Polisi,na wananchi waandamane kushinikiza ajiuzuru/ang'atuke.ndipo kwa aibu kubwa tutasikia tamko lake,kupitia vyombo vya habar i.

Sidhani kama watanzania tunaweza kuchukua maamuzi magumu ya kuandamana zaidi ya kulalamika pasipo kuonyesha hisia zetu kwa vitendo! Ni kama vile tumerogwa na kuwa watu wa porojo muda wote! Tuliowachagua kutuongoza wanaiba badala ya kulinda na kuendeleza mali za Taifa!
 
Nyie mnalalama tu lakini mjue hizo millioni 600 za kufidia huo upanga mtazilipa nyinyi walipa kodi kwa uzembe wa mtu mmoja!!! Ndio mana watu wanasema bongo ni nchi tambarale!!!

Baba anakomba ugali, watoto wanakomba mboga!!
 
Kwa hiyo kamanda amekula njama ya kuiba,kweli tunapoelekea ni kubaya!

Hata kama hajakula njama ya kuiba huo upanga,yeye kama askari alitakiwa kuchukua tahadhari ya hali ya juu katika kuulinda na kuutunza huo upanga wa dhahabu! Hivyo basi kwa uzembe wake anatakiwa kung'atuka mara moja. Inashangaza wakubwa zake nao bado wanashindwa kufanya maamuzi magumu ya kumshinikiza aondoke madarakani!

Hapa tulipo sasa ndiyo pabaya pasipo na kifani kuliko huko tuendako, kwani hakuna anayeijua kesho! Tumwombe Mungu hiyo kesho tusiyoijua vyema, atupatie viongozi wenye uzalendo na heshima kwa watanzania!
 
Huo Upanga kapiga mwenyewe!!

Kuna utata mkubwa katika kupotea kwa upanga huo wa dhahabu! Mpaka sasa haijulikani umeibiwa lini kwani imegundulika kuwa haupo na kutangazwa umeibiwa pale ulipotakiwa kupelekwa nchini Namibia!
 
Hata kama hajakula njama ya kuiba huo upanga,yeye kama askari alitakiwa kuchukua tahadhari ya hali ya juu katika kuulinda na kuutunza huo upanga wa dhahabu! Hivyo basi kwa uzembe wake anatakiwa kung'atuka mara moja. Inashangaza wakubwa zake nao bado wanashindwa kufanya maamuzi magumu ya kumshinikiza aondoke madarakani!

Hapa tulipo sasa ndiyo pabaya pasipo na kifani kuliko huko tuendako, kwani hakuna anayeijua kesho! Tumwombe Mungu hiyo kesho tusiyoijua vyema, atupatie viongozi wenye uzalendo na heshima kwa watanzania!
Nasikia muda wake wa kuondoka ni mwezi wa kumi na mbili,kwakuwa tumezoea kubebana wameamua asubiri muda wake ufike,ili aondoke kwa heshima!
 
Back
Top Bottom