figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimvisha nishani IGP mstaafu Omari Mahita, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (ARPCCOS) kwa kuwa IGP wa kwanza Tanzania kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya Mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu akimvisha nishani IGP mstaafu Saidi Mwema, nishani ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa kuwahi kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo na kuliletea sifa Jeshi la Polisi Tanzania kimataifa. IGP Mangu amemvisha nishani kwa niaba ya mwenyekiti wa shirikisho hilo wa sasa. Tukio lilifanyika jana katika chuo cha taaluma ya Polisi Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.