Nani kati ya hawa kurithi mikoba ya IGP Said Mwema?

Spanishboy

Senior Member
Apr 24, 2011
119
0
Nimeupata ujumbe huu mahala nikaona niupitishe na kwenu wanajukwaa
"Wanaotajwa sana kulingana na vyanzo mbalimbali na nukuu katika baadhi ya vyombo vya habari ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya DCP Diwani Athumani,cheo ambacho ametunukiwa hivi karibuni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu na DCP Thobias Andengenye ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha"
Sasa endelea kusoma...

Ni takribani miaka 8 sasa inakaribia kumalizika baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Interpol Said Mwema kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Omar Mahita ambaye alikuwa IGP kwa takribani miaka 10 akiwa amevaa viatu vya marehemu Harun Mahundi.

Tofauti na aliyekuwa mtangulizi wake Said Mwema amejizolea sifa lukuki za utendaji wake katika Jeshi la Polisi na kuibua dhana nyingi ikiwemo Polisi Jamii, Ulinzi Shirikishi na hata Utii wa Sheria Bila Shuruti.

Kwa kutumia weledi wake wa kazi Mwema ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Interpol alikuwa RPC Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ambaye alirithi mikoba ya aliyekuwa RPC mkoani humo Laurian Sanya.

Kwa kufuata weledi ule ule wa kazi kutoka kwa mtangulizi wake akiwa RPC mkoani Mbeya aliweza kufanikiwa katika wimbi kubwa la majambazi kwa wakati wake na kupunguza kwa kasi kubwa, tatizo la mauaji ya kishirikina na hata ujambazi wa uporaji na utekaji wa magari.

Kutokana na sifa hiyo na mengine mengi Said Mwema alipata tunu adhimu ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Interpol na baadaye kuteuliwa na Rais kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi nchini akirithi mikoba ya Omar Mahita ambaye alielezwa kutofanikiwa vizuri katika nafasi hiyo.

Wakati wa Mahita kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji na hata vitendo vya ukatili vilivyoelezwa kufanywa na Jeshi la Polisi hususani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 hususani katika Visiwa vya Zanzibar, alijipachika jina maarufu la NGUNGULI kwa kile kilichosemwa kukabiliana na nguvu ya chama cha Wananchi CUF wakati ule maarufu kwa jina la NGANGARI.

IGP Mwema alimudu kuwavuta na kuwaaminisha wananchi kuwa Jeshi hilo lipo kwa ajili ya kuwatumikia Raia na si vinginevyo na hivyo kujaribu kufunika maovu ya mtangulizi wake Mahita ambaye aliwafanya raia wengi kulichukia Jeshi hilo.


Hata hivyo weledi wa IGP Said Mwema ambao umempatia sifa lukuki unaelezwa kuwa unakaribia kufikia tamati mwishoni mwa mwaka huu ambapo VICHWA vitatu vinatajwa kuwa vinaweza kurithi nafasi hiyo kutokana na sifa walizonazo na umahiri na weledi wa utendaji wao ndani ya Jeshi la Polisi nchini.

Wanaotajwa sana kulingana na vyanzo mbalimbali na nukuu katika baadhi ya vyombo vya habari ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya DCP Diwani Athumani,cheo ambacho ametunukiwa hivi karibuni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu na DCP Thobias Andengenye ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha.


Kila mmoja kati ya hao ana sifa zake katika utendaji uliotukuka katika Jeshi hilo ambapo kwa kuweka uwiano wa utendaji wao ndani ya Jeshi la Polisi kila mmoja anazo sifa zinazotajwa kusukuma mbele utendaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Kwa kuona umuhimu wa wa kumpata kiongozi mahiri aliyetukuka Blogu hii na Bloga wadau wanaopenda kushiriki katika mchakato huu tunaweka fursa ya wananchi kufuatilia kwa makini utendaji wa Makamanda hawa na hatimaye kupiga kura kupitia FB ambazo zitakuwa wazi kwa wasomaji wa mitandao ya Kijamii kuweka mustakabali wa uongozi ndani ya Jeshi la Polisi nchini.


TUNAAMINI KATIKA UTII BILA KUSHURUTISHWA!!!.
 

Fabolous

JF-Expert Member
Sep 23, 2010
2,016
2,000
Mwni Mwema aondoke tu ila damu ya watu wa Arusha aliowaua kwenye maandamano ipo mikono mwake.
 

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,273
2,000
Mleta mada tukujue kwanza wewe ni nani
msemaji wa jeshi la polisi kama siyo au ndiyo
rudi nyuma kasome PGO kwanza na ongezea katiba ya nchi halafu utuambie mkuu wa majeshi anateuliwa kwa kufatataratibu zipi jeshi halina siasa kama vyuo vya nessing
 

vyuku

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
501
225
Ukweli hasa kwa Andengenye hafai kwa sababu ni kiongozi dhaifu sana,hana maamuzi na hajiamini kwa cheo chake,IGP MWEMA kamuamini sana huyu kaka lkn hana ajualo zaidi ya kuomba rushwa kwa askari wenzake,hata wakati mwengine inapotokea askari ameonewa labda na RPC fulani au wakuu fulani jeshini,anapopewa kazi na IGP kufuatilia lalamiko km hilo huwa haamui hata km askari kaonewa bali hupendekeza kile kile walichopendekeza wachini yake kwa kuwaonea aibu au haya kuwakosoa,na ndio maana jeshi la polisi wanadhulumiana sana,bado Andengenye hafai ameshapimwa sana anafeli,hao wengine sijui.
 

vyuku

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
501
225
Ukweli hasa kwa Andengenye hafai kwa sababu ni kiongozi dhaifu sana,hana maamuzi na hajiamini kwa cheo chake,IGP MWEMA kamuamini sana huyu kaka lkn hana ajualo zaidi ya kuomba rushwa kwa askari wenzake,hata wakati mwengine inapotokea askari ameonewa labda na RPC fulani au wakuu fulani jeshini,anapopewa kazi na IGP kufuatilia lalamiko km hilo huwa haamui hata km askari kaonewa bali hupendekeza kile kile walichopendekeza wachini yake kwa kuwaonea aibu au haya kuwakosoa,na ndio maana jeshi la polisi wanadhulumiana sana,bado Andengenye hafai ameshapimwa sana anafeli,hao wengine sijui.

Ni kweli mkuu huyu jamaa anajipendekeza sana kwa IGP lkn hafai akiondoka IGP humng'ong'a,huwa anashirikiana kula rushwa na akina Byatao na Ambika,namshangaa IGP kumuweka Byatao kuwa mkuu wa kitengo cha nidhamu wakati ye mwenyewe hana hana nidhamu
 

umatemate

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
755
195
napendekesa kamanda kova awe igp atapendeza sana siku akishika majambazi we utapenda tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom