IGP, Mwanasheria Mkuu waitwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP, Mwanasheria Mkuu waitwa mahakamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jan 25, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,907
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]IGP, Mwanasheria Mkuu waitwa mahakamani
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 24 January 2012 20:54 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP),Said Mwema

  James Magai
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewataka mahakamani hapo leo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ili kutoa maelezo ya kwa nini walimkamata na kumshikilia Kiongozi wa Chama cha Movement for Solidarity and Development (MSD) cha Burundi, Alexis Sinduhije (46).

  Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa jana na Jaji Lawrence Kaduri baada ya kukubaliana na ombi lililowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Sinduhije, Hubert Nyange.

  Katika maombi hayo namba 7 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya kiapo cha dharura, Nyange anadai kuwa kitendo cha Sinduhije kukamatwa na kushikiliwa ni kinyume cha utawala wa sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu.
  Sinduhije alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kwa hati ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) akitokea Kampala, Uganda kuja nchini na Januari 13 alifikishwa mahakamani Kisutu, lakini hakusomewa mashtaka.

  Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mwanzilishi wa Redio Publique Africaine (RPA) ya Burundi, alikamatwa na polisi na kushikiliwa kwa wiki mbili mfulululizo katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, huku kukiwa hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini na jeshi hilo kuhusu sababu za kukamatwa kwake.

  Wakati akikamatwa na Interpol, Sinduhije alituhumiwa na Serikali ya Burundi kuhusika na mauaji ya Mwakilishi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Dk Kassi Manlan raia wa Ivory Coast na aliyekuwa mtumishi wake na pia mauaji ya halaiki ya Katumba.

  Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo aliyotoa polisi, Sinduhije ambaye pia ni mwandishi wa habari za uchunguzi alidai kuwa ndiye aliyefanya uchunguzi wa mauaji ya Dk Manlan, ambao uliwezesha watuhumiwa kukamatwa na kushtakiwa na kisha kupatikana na hatia.

  Kuhusu mauaji ya mtumishi wake, alidai aliuawa na wakala wa Serikali ya Burundi wakimfananisha naye kwa kuwa walikuwa wakimtafuta kumuua yeye.

  Mtikila aibuka
  Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete akishauri kiongozi huyo aachiwe bila masharti.

  Katika barua hiyo, Mtikila amedai kuwa Sinduhije hakuhusika na tuhuma za mauaji zinazomkabili nchini mwake na badala yake ndiye aliyefanya uchunguzi wa kifo cha Dk Manlan na kukibainisha.

  “Inajulikana wazi kwamba mtumishi wa Sinduhije aliuawa na wakala wa Serikali kwa makosa wakidhani kuwa wamemuua Alexis Sinduhije mwenyewe,” alisema Mtikila kwenye barua hiyo.

  Aliongeza kwamba, Sinduhije hakuhusika na mauaji ya Katumba kwa kuwa wakati mauaji hayo yakitokea Novemba mwaka jana, kiongozi huyo wa MSD hakuwepo Burundi baada ya kukimbia kutokana na uhasama wa kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Akizungumzia barua hiyo, Mtikila alisema alipoipeleka Ikulu aliambiwa kuwa Rais Kikwete hakuwepo na kushauriwa kuwasiliana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Sinduhije alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 13 mwaka huu, lakini hakusomewa mashtaka na badala yake alirudishwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako alikuwa akishikiliwa bila kupelekwa mahakamani.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tungekuwa na akina Mtikila kumi hivi hata Tanganyika,mgombea binafsi yote yangeshapatikana by now!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,608
  Trophy Points: 280
  Intelijensia yetu imeishia kwa CDM Arusha na waandishi wa habari tu?????kweli UWT uliondoka na baba yetu wa taifa ck hizi ni wapifa deal tu...
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Vyombo vyetu vya usalama vina uonevu wa hali ya juu kwa baadhi ya human races. Hata hivyo, ukisoma taarifa hii ktk gazeti la mwananchi utagundua kuwa mtuhumiwa Bwana Sinduhije ameshaondolewa nchini hata kabla ya IGP na AG kuleta hati ya kiapo kinzani(Counter affidavit). Naddhani vyombo vyetu vya usalama vimegundua kuwa vimefanya uonevu sasa vimeamua kumuonea zaidi kwa kuepuka aibu ya kubwagwa mahakamani na hoja na wakili Nyange.
   
 5. l

  luckman JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Tumebanki na wa piga dili! Na hii ndo athari ya kumpa rais majukum mazito ya kumchagua kila mtu!
   
 6. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  inaweza kuwa kama ilivyotokea kwa zambia na malawi baada ya malawi kumkamata michael satta(rais wa sasa wa zambia) akiwa mpinzani mkuu wa serikali ya zambia wakati huo.Michael satta alipoingia malawi,serikali ya malawi ilihisi kuwa ataleta uchochezi kwa wapinzani wa serikali ya malawi,sasa tangu juzi michael satta alipochaguliwa kuwa rais wa zambia mahusiano ya nchi hizi mbili yamedorora.Hivyo serikali yetu kuamua tu kumkamata huyu mpinzani wa burundi bila kuwa makini,athari zake zinaweza kuanza kuonekana siku za usoni kwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili.Lazima usalama wa taifa uwe makini kulinda usalama wa nchi sio kwa leo tu bali hata kwa siku zijazo.
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine ni kutafuta sifa tu ili Tanzania Polisi ionekane inafanya kazi vizuri. Tunajikomba kwa mataifa ya nje kuwa tunajua sheria kumbe hakuna lolote.

  mbona hapa Tanzania tunashindwa kuwachukulia hatua wahusika wa makosa mfano EPA, ubadhirifu wa mali za Umma na Ujambazi. Lakini badala yake tunafuatilia mambo ya nje kutafuta sifa ya Kimataifa.

  AAAACHENI HIZOOOOOOOOOOOOOOO POLISI TANZANIA. YENU YANAWASHINDA!!!!!!!!!!!!!!!:lol::shock:


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...