Kuushitaki mtandao huo kwa IGP ni sawa na kesi ya Ngedere kumpelekea Nyani, kwani ukiisoma vizuri taarifa ya Mwakyembe ile inayokanusha maelezo ya DCI hapo utapata picha halisi iliyojificha ndani ya jeshi letu la POLISI, hebu angalia huyo IGP alivyosigina sheria na uadilifu kazini.......
, alisemasiku chache baada ya kumkabidhi IGP Mwema barua hiyo, alitumiwa timu yawapelelezi ofisini kwake ili kuchukua maelezo yake ya ziada. Alifafanuakuwa timu hiyo ilikuwa inaongozwa na Ofisa wa polisi ambaye wiki chachezilizopita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengola kumbambikizia dawa za kulevya mtoto wa mmoja wa wafanyabiashara maarufunchini, suala alilodai kuwa mpaka sasa uongozi wa Polisi umeshindwa kulitoleamaelezo ya kuridhisha.
Alisema kwa msingi huo,aliona ameletewa mtuhumiwa wa rushwa na ujambazi kuendesha uchunguzi wawatuhumiwa wengine wa ujambazi jambo ambalo haliwezekani na kwamba suala lakelimefanyiwa mzaha. Mwakyembe alisema wiki chache baada ya barua yakekuwasilishwa kwa IGP na timu ya polisi kuanza kazi, Jeshi hilo likachukua hatuaya kuwapongeza na kuwazawadia askari aliowatuhumu kushirikiana namajambazi. "Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwaujumbe tosha wa kunipuuza,"ilibainisha taarifa hiyo.
Alisema tuhuma za askari polisikujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto nakuwagusa askari, wale aliowatuhumu kwenye barua yake, walihamishiwa mikoamingine. Mwakyembea alisema ili kumkatisha tamaa kabisa, barua yake ya ‘siri'kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kamahabari iliyokebehi na kukanusha taarifa nzima aliyoitoa "Sijui kwafaida ya nani," alihoji katika taarifa hiyo na kuongeza, " Lakini huu ni mchezowa kawaida kwa Jeshi la Polisi. Akitoa mfano wa Waziri Sitta, kuwa hivikaribuni, kiongozi huyo alihojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisiofisini kwake, wakiwa wawili tu, lakini taarifa ya mahojiano ikaonekana kwenye moja ya magazeti, ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta nakubainisha kuwa
Akamalizia kwa kusema.......
uadilifu wauongozi wa Jeshi la Polisi, umefikia pabaya.
JE HAPO BADO MNASEMA TUNA POLISI WA WANAINCHI WA TANZANIA?