Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama unafahamu haki zako huwezi lalamika, namba ya simu ya huyo IGP ipo mpigie mweleze na ushahidi uwe nao
Utakaporudi na hiyo part 2 uje na majina ya hao wahalifu pamoja na hao makamanda
Mkuu mimi sijajua kama hilo genge lipo ila jana nikeona gari limewekwa stika ya neno free marson nikashangaa ila nilivyochungulia kwa ndani nikamuona ni kijana tu. IGP inabidi alifanyie kazi aisee polisi imeshakuwa corrupted
police jamii
Kwani kinachowashinda kubeba mawe, mikuki na mapanga na kuingia mitaani kumtaka kikwete ang'oke ni nini? Maana Kikwete is a completely failed leader. Ukishakuwa na rais mbovu kama Kikwete usitegemee kwamba kutakuwa na utendaji mzuri huku chini. Mapambano yaanze dhidi ya Kikwete kwanza kabla hatujawakataa wahuni wengine wengi.Wakati Mwakyembe linamkuta ulisema haikuhusu na hata sasa watanzania tutasema haituhusu, hivi kwanini isifike mahali tuwe wazalendo? Tukubaliane nini cha kufanya.
kama kweli upo police jamii fatilia eneo lililotajwa na ndohela kuliko kumtaka aje hapo uliposema, kwa sababu za kiusalama. Simshauri ndohela aonane na wewe. Unanipa mashaka, au nawe ni kati yao?
Kama wewe na afande jamii nchi hi imejaa mavilazaMweee ndio nini leteni post za kweli tufanyie kazi sio viroba at work
... ya kudhulumu watu viwanjaUpo kwenye system ipi?
hapo kwenye red siku hizi ni wambea wa taifa hakuna kituHabari hii ni kweli kabisa. Wiki tatu nyuma walivamia kiwanja Mbezi beach maeneo ya Five Star na kuzungusha ukuta na kuleta walinzi. Nina habari mwenye kiwanja hakupata ushirikiano kabisa na polisi ya Wazo zilipo ofisi za OCD hivyo kwa msaada wa ofisi ya mwanasheria wake waliweza kupata amri ya kusimamisha ujenzi iliyotolewa na mahakama ya Ardhi na kesi itaanza karibuni. Katika uvamizi huo walitumia risasi za moto kumtisha the legal owner na majirani na hata baada ya ku report polisi hawakuchukua hatua yeyote. Habari ni kuwa tapeli mmoja papaa mfadhili wa bendi ndie kiongozi wa kundi lakini anawatumia wasaidizi wake kuongoza uhalifu huu kwa kuwa ameshaonywa karibuni na baadhi ya viongozi wa Polisi na hajatii alichoonywa. Naomba ifahamike kabisa hutapata msaada polisi hawa jamaa wakivamia kiwanja chako na hii ni kwa sababu ya wanalindwa na baadhi ya viongozi wa polisi. Nadhani huu ni uonevu uliokithiri na swala hili lingefuatiliwa na usalama wa Taifa kwani linakua kwa kasi. Nawakilisha wakuu