IGP - Mtandao huu ni hatari - Part I | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP - Mtandao huu ni hatari - Part I

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by We know next, Feb 17, 2012.

 1. W

  We know next JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Kamanda Mwema - IGP,

  Nadhani utakuwa na taarifa na kama huna taarifa basi tunaomba uanze kuifanyia kazi taarifa hii:

  Kuna Genge moja la Kitapeli ambalo limezuka hapa jijini na kufanya utapeli wa kuvamia viwanja vya watu na kujifanya ni vya kwao. Genge hili linafanya kazi zake zaidi maeneo ya Kawe, Mbezi Beach, Tegeta, Boko mpaka Bunju. Genge hili la matapeli wanatembea na Magari yameandikwa Free Mansos, na wanatembea na silaha ( Bastola) vibindoni mwao na inasemekana wanapesa nyingi sana, ambazo ni pesa chafu. Wamekuwa wakifanya utapeli na usumbufu huo kwa baadhi ya watu wenye viwanja vyao ktk maeneo husika.

  Kwa nini basi ni mtandao hatari?

  Genge hili limejiimarisha sehemu zote muhimu ambazo linaweza kufanikisha kufanya mambo yao kwa urahisi, maeneo hayo ni katika Jeshi lako la Polisi, ofisi za manispaa, mahakama za ardhi, Wizara ya Ardhi na Makapuni binafsi ya ulinzi.

  1. Jeshi la Polisi - Kuna baadhi ya polisi wanashirikiana na genge hili katika kuwadhurumu watu haki zao za msingi, tena kuna wengine ni maafisa wa juu kabisa ktk jeshi hili la Polisi. Maafisa hao wamekuwa wakikataa kutoa msaada kwa waathirika kwa misingi kuwa, migogoro ya ardhi Polisi haihusiki, ni wizara ya ardhi pekee. Hata mtu akienda kuripoti kuwa kuna wavamizi, wamevamia kiwanja, wamevunja nyumba, na wamekuja na silaha, bado polisi hao wanakataa kutoa msaada kwa walalamikaji. Badala yake, Polisi hao hao, wanakushauri kuwa la kufanya na wewe anza kubomoa kila anachokifanya huyo mvamizi. Kamanda, Tanzania tumefika hapo kweli? Yaani kimbilio la walalahoi limekuwashubiri? Unataka watu wachukue sheria mikononi? Maafisa hao wachache wasiokuwa na utu wala kufahamu kazi yao, wananunuliwa na pesa za hongo kutoka ktk genge hilo na kuwafanya kuwa nao ni wanamtandao, yaani polisi wanamsaidia mharifu? Je ni maadili ya kazi hakuna? Au ni sababu ya mishahara midogo? Kitakachokuja tokea Kamanda, watu wanaanza kukosa imani na Jeshi lako, na hata kuanza kujenga uadui na polisi, sababu tu, ya hao maafisa wachache wa polisi. Itafika kimbindi watatengwa kutokana na mambo haya. Genge hilo, limejijenga ndani ya polisi kwa ajili ya kupata usalama wao, kwani wanajua kabisa, wakifanya uvamizi huo, watu watakimbilia polisi kutoa taarifa, kwahiyo polisi hawata respond kwa haraka kama inavyotakiwa.

  Maswali yangu ni haya kamanda,

  i. Wananchi waende wapi ikiwa kama kimbilio lao, yaani polisi wakati wa matatizo ya uhalifu na ya jinai kuna kuwa hakuna msaada?

  ii. Ikiwa kama maafisa hawa wataendelea kununuliwa na kuwa wanamtandao wa kiuhalifu, je unajenga jeshi la namna gani?

  iii. Hivi wananchi wakipoteza imani na polisi tutakuwa salama kweli?

  iv. Ni Kwanini maafisa wachache wa polisi waharibu sifa ya jeshi lako lote?

  v. Nilisema mwanzo kuwa, unaweza kuwa umelisikia kundi hili au hapana, lakini je jibu lake au suluhisho lake ni nini kwa lolote kati ya uelewa au kutoelewa kuwepo kwa Genge hilo?

  Nafahamu, kunaweza kuwa na wanajamvi wengine ambao wamesha lisikia au kukutana na mambo ya Genge hili, labda wanaweza kuongezea kwa hapa nilipoishia....! Kamanda, Mtandao huu ni hatari, chukua hatua.. PART II itaendela na maeneo mengine..

   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu yaani mimi nilishapoteza imani na maaskari kitambo sana na tena nikishuhudia kapigwa risasi na mwangalia mpaka anakufa kama walivyomfanyia rafiki yangu inauma sana..

  RIP Eddy Clux..
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kama unafahamu haki zako huwezi lalamika, namba ya simu ya huyo IGP ipo mpigie mweleze na ushahidi uwe nao
  Utakaporudi na hiyo part 2 uje na majina ya hao wahalifu pamoja na hao makamanda
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hizi zote ni ishara za a confirmed failed system.... umafia, neglience without accountability, a corrupt force, total control by a few hooligans (who in most cases are not even as reach as they portray) calling all teh shots
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  naomba unisamehe, let me call you mpuuzi, yani ni bora kupuuzwa, waliofanya hivyo either hawapo tena au kama wapo, basi hawatafanya tena hiyo jitihada

  ukiona mtu kaleta hapa kwa namna hiyo ujue hizo jitihada nyingine ameshafanya
   
 6. kitonsa

  kitonsa JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  We unafikiri bila kupora viwanja vya watu hao mapeneshee watapata wapi pesa za kutunza wanamuziki wa dansi na wakina falii ipupa..
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Nchi hii huu ujanja ujanja hatufiki popote. Tunajitengenezea mabalaa tu
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Makamanda wa polisi wawe wanachaguliwa na wananchi....
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Badala ya kuwa watendaji wamekuwa wanasiasa tangu intelijensia...ilipo fail IGP amepoteza umaarufu!!!
   
 10. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi sijajua kama hilo genge lipo ila jana nikeona gari limewekwa stika ya neno free marson nikashangaa ila nilivyochungulia kwa ndani nikamuona ni kijana tu. IGP inabidi alifanyie kazi aisee polisi imeshakuwa corrupted
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Aisee! hii ni hatari sana.... IGP chukua hatua dhidi ya suala hili la sivyo litaumiza wengi.
   
 12. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kiukweli pasipo na majina ya wahusika inakuwa ngumu kuitofautisha na hadithi za erick..
   
 13. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Piga ile namba yao ya kutoa taarifa
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa hili ingekuwa bomba kweli kweli!
  Na hata RC angetakiwa achaguliwe na wanainchi na siyo kuteuliwa kijinga kama inavyofanya chama cha majambazi

  Sina budi kusema kwamba hata hili genge hawako mbali na hii chama kijani.

  Tuwe wapole kidogo kwani tutasikia mengi sana kuhusu hili.
   
 15. n

  ndoleha Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari hii ni kweli kabisa. Wiki tatu nyuma walivamia kiwanja Mbezi beach maeneo ya Five Star na kuzungusha ukuta na kuleta walinzi. Nina habari mwenye kiwanja hakupata ushirikiano kabisa na polisi ya Wazo zilipo ofisi za OCD hivyo kwa msaada wa ofisi ya mwanasheria wake waliweza kupata amri ya kusimamisha ujenzi iliyotolewa na mahakama ya Ardhi na kesi itaanza karibuni. Katika uvamizi huo walitumia risasi za moto kumtisha the legal owner na majirani na hata baada ya ku report polisi hawakuchukua hatua yeyote. Habari ni kuwa tapeli mmoja papaa mfadhili wa bendi ndie kiongozi wa kundi lakini anawatumia wasaidizi wake kuongoza uhalifu huu kwa kuwa ameshaonywa karibuni na baadhi ya viongozi wa Polisi na hajatii alichoonywa. Naomba ifahamike kabisa hutapata msaada polisi hawa jamaa wakivamia kiwanja chako na hii ni kwa sababu ya wanalindwa na baadhi ya viongozi wa polisi. Nadhani huu ni uonevu uliokithiri na swala hili lingefuatiliwa na usalama wa Taifa kwani linakua kwa kasi. Nawakilisha wakuu
   
 16. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Pole sana mdau!Naamini kilio chako kimewafikia walengwa tusubirie matokeo!
   
 17. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sinauhakika na mtoa mada nikupe simu ya igp said mwema au ya dci manumba mimi mwenyewe nipo kwenye system kama nikweli na ushahidi unao mimi naweza kusaidia
   
 18. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Upo kwenye system ipi?
   
 19. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  police jamii
   
 20. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndoleha Unaweza kukutana na mimi kesho njoo makumbusho unipe data naweza kufanyia kazi kama kweli unayoyasema na ushahidi unao sitaki mambo ya udaku au umepata viroba
   
Loading...