Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,139
- 12,286
Ni uzwazwa tu kuanza kujikosha leo wakati tayari timu ya kamati ya Bunge ipo kazini...subirini sindano iwaingie
Nguruvi3Na wapi mtu huyo ana historia ya kazi kama hizo? Kilitafutwa kigezo cha ugaidi ili kuhalalisha uharaka wa kupeana ulaji. minyoo kasema inatafutwa skendo kutuondoa hapa.
Ninachoshangaa watuambuaji hapa wamekwama! Tunasikia ripoti za kwingine hapa ngoma muzito
Tulisema kuanzia awali, zile kimbia kimbia tupiana mpira n.k. ni mbinu tu za kuvuta muda mafaili yakae uzuri. Kwa bahati mbaya au nzuri taarifa zilishafikia vyombo vya habari na sasa wanabaki kubabaika tu
Hili la Lugumi lita define mapambano dhidi ya rushwa! likifunikwa basi tuendelee na utamaduni wetu wa kawaida. Washangiliaji wote mbio! hakuna anayekuja kujibu hoja
MsemajiUkweli tuambie ukweli. Simiyu Yetu hiliunalisemaje maana limenata na litaibuka kila asubuhi
Mkuu tuwekee basi mchanganuo wa gharama Za hivyo vifaa hapa.mkuu huo mladi ulibuniwa kwa lengo la kupiga pesa hizo mashine Thamani yake harisi ni kidogo sana.
Well, huenda nina hisia lakini kila mara hisia hizo hudhihirika kuwa kweli. Sijatoa hukumu kwa hili swala, naomba niweke rekodi sawa.Nguruvi3
Nilishakuambia mimi siwezi kuanza kujadili masuala ambayo sina uhakika nayo kwa sababu mimi siyo mwanaharakati ambaye moja ya tabia zao ni kuongea sana bila kuwa na balanced opinion and without concrete fact.
Hizi hoja za kusema suala la Lugumi lita-define mapambano ya Rais Magufuli dhidi ya rusha ni hisia zako tu kama ulivyo ujenzi wa hoja zako zenye msingi wa hisia.
Ni wewe toka siku ya kwanza ya Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ulisema hana jipya lakini ninashangaa kwa sasa hoja zako unajenga mazingira kuwa hili suala ndiyo benchmark na litatoa mwerekeo wa Rais Magufuli. Hii inaonyesha huna hata msimamo kifikra kuhusu utawala wa Rais Magufuli au kwa maana nyingine, unahamisha magori ya kisiasa kila mara kulingana na mazingira na hisia zako.
Kila siku ninasema ukweli hauwezi kufichwa bali unaweza kucheleweshwa tu. Tunafahamu kwa sasa kuna Kamati ndogo ya bunge inatafuta ukweli kama umefichwa na baada ya wiki nne tutafahamu.
Kuanza kujadili na kutoa hukumu kwa suala ambalo tutapata ukweli baada ya wiki nne ni kupoteza muda au kufurahisha genge la Jamiiforums.
Lugumi au polisi kama watakuwa wameficha ukweli watastahili kuwajibishwa lakini pia tujiandae kuupokea ukweli kutoka kwenye kamati ndogo.
Ninafahamu kama ukweli utaletwa tofauti na jinsi baadhi ya watu walivyohukumu, kuna wengine wataanza kuukataa na kusema umepikwa.
Tuiache Kamati Ndogo ya Bunge ifanye kazi, Wiki nne siyo mbali.
....Hela kubwa imeshapigwa hapa sasa wanahangaika kuficha dhambi zao kwa kukingiana vifua. Haiwezekani kabisa mkataba wa pesa nyingi kiasi hiki usainiwe ndani ya siku moja tu bila kuwepo wengine waliotuma maombi yao ya kuomba kupewa kazi hiyo. Wako busy kuhalalisha kwamba kazi imefanyika bila kujali je mkataba alipewa kihalali? Je, taratibu za mikataba ndani ya taasisi za Serikali zilifuatwa? Je, taratibu za malipo Serikalini zilifuatwa? Hiyo kazi ilifanywa katika viwango vinavyokubalika?
...Lugumi kaiweka serikali na Bunge mfukoni kupitia kitwanga ambaye yupo Dodoma anahaha usiku na mchana kuwapoza wabunge wasimwandame akatumbuliwa.
Hapo sterling ataishia ukonga tu
Rudi kasome tena IT. Mawasiliano ya Mwanza na kituo kikuu Dar yatafanyika kwa LAN?
Tatizo unataka kujikweza tu huna IT yoyote ulichosoma ni historia ya IT.
Tofauti yangu na wewe kuhusu kwa hili suala ni moja. Wewe unajenga hoja kwa kutumia msingi wa nadharia, Mimi ninajenga hoja kwa kutumia msingi wa uharisia.Well, huenda nina hisia lakini kila mara hisia hizo hudhihirika kuwa kweli. Sijatoa hukumu kwa hili swala, naomba niweke rekodi sawa.
Nilichosema kuna kuficha ficha na kusita kulishughulikia.
Nadhani nimekuonyesha jinsi ambavyo ubabaishaji unavyoendelea na kujikanganya.
Sasa kama huelewi mwenye dhamana na suala hili, kwa nini unasema kuna kuficha ficha.Hatuelewi nani mwenye dhamana na suala hili, mara tunasikia PCCB mara kamati ya bunge.
IGP anasema hakuna shida, kamati ya ulinzi na usalama inapokea nyaraka ambazo ilisema ni mkataba, bunge linasema ni maelezo ya kina.Hapo sina shaka na hisia zangu na nitasimama nazo
Sasa kama ulishahitimisha fikra zako kuhusiana na utendaji wa Serikali, kwa nini unahangaika na masuala ambayo ulishayafahamu?Kuhusu serikali hii, ni kweli kuanzia mwanzo nilisema hayo tena niongezee nilichosema '' Huwezi kupata kondoo mzuri kutoka genge la fisi' Ninasimama na hilo. CCM ni ile ile na watu wale wale katika mfumo ule ule na hapa tunaona wa kulindana
Utakielezaje kilicho cha kweli bila ukweli? Ukweli wa Mkataba wanaofahamu ni polisi na Lugumu.Hii habari ya kusema tuachie muda fulani ni kukwepa ukweli.
Ukweli si tuhuma, ni kueleza kile kilicho cha kweli.
Huu ni mtazamo wako ambao hauwezi kuwa ni sheria au mwanvuli kwa kila mwananchi.Nasema hili lita define utawala wake na mapambano ya rushwa kwasababu ikiwemo double standard basi kila kitu kitakuwa kwa mwendo huo.
Na washangiliaji kama ninyi mtashindwa mahala pa kusimama na kumwacha mzee mwenyewe.
Tutafeli kama Taifa
That's exactly what's gonna happen to him.....mark my word!Nahofia isije kuwa kama ya mama Kilango
Si kwamba anaongea asiyoyajua, anajua kila kitu mwache aingize kitanzi shingoni.Mimi ni IT proffesional na sizdhani kama hizo biometric system ili zifanye kazi zinahitaji internet connection wala sio kweli Mangu anaongea mambo asiyo yajua. Only LOcal area network inahitajika kwenye hiyo system. Anajaribu kutetea uovu huyu Mangu
Ukiisha amka ukanawa uso utajua.Mkuu unaweza kunijuza na mie Kitwanga kafanya nini maanake naskia sikia ila sikljapata taarifa kamili??
Sidhani unatumia uhalisia, vinginevyo usingebabaika ukihamisha magoli kila asubuhi. Hujaeleza 'uhalisia' wa bunge kusema abcd, kamati zake efg, serikali hjk n.k.MsemajiUkweli, post: 16008019, member: 91662"] Wewe unajenga hoja kwa kutumia msingi wa nadharia, Mimi ninajenga hoja kwa kutumia msingi wa uharisia.
Alaa, si ulisema ni la kamati ya ulinzi na usalama na mambo ya nje?Ni nani unadhani anaficha ficha na kusita kulishughuliki, Kamati Ndogo ya Bunge inalishughurikia
.Kwakweli sikujua kama kuna mauza uza hayo, nadhani Watanzania wengi hawakaaujua ikiwemo PAC na PCCB. Wangalijua uchunguzi usingehitajika.kama isingekuwa PAC,hisia zako zisingewepo,usingefahamu kuna mkataba unaohitaji clarification kutoka polisi.
PAC
Ulisema tuache kamati ya ulinzi na usalama ifanye kazi zakeTuache Kamati Ndogo ya Bunge ifanye kazi zake labda kama hatuiamini
Kwasababu kila mmoja anakimbia ! ndio msingi wa kusema hakuna anayechukua dhamana. Sidhani kama unaweza kunielezaSasa kama huelewi mwenye dhamana , kwa nini unasema kuna kuficha ficha.
Ni kweli kabisa, lakini mawasiliano gani ikiwa hawakuweza kueleza tofauti ya mkataba na maelezo ya kina.Kupitia tamko rasmi la Bunge mwenye dhamana ni Bunge kupitia PAC. Bunge ni taasisi mawasiliano.
kuchukua maandishi kutoka kwenye Magazeti au mitandao na kuyafanya ni maelezo ya Bunge inakuwa ni kununua udaku.
OK si kamati ya ulinzi , usalama na mambo ya nje? Si PCCB? Si serikali?Nimekuambia, wiki nne siyo mbali, tusubiri ukweli utufikie kutoka kwenye chombo kilichopewa kazi kisheria ambacho ni Kamati Ndogo ya Bunge.
Ili kukabiliana na washangiliaji wanaopotosha umma, wanaotaka umma uamini mambo safi, wanaosema uongo.Sasa kama ulishahitimisha fikra zako kuhusiana na utendaji wa Serikali, kwa nini unahangaika na masuala ambayo ulishayafahamu?
Nani kaukupoka matumaini mkuu? Endelea na matumaini wala usiahangaike na watu kama sisi. Jenga matumaini kwa nafsi na nafasi yako. Ni haki yako kikatiba na kibainadamu. Kuishi kwa matumaini hata kama ni mkate wa mawe! Hapa unatusingizia kufifisha matumaini yako! Si kweli. Kazi uzi mkuuMtu mwenye hekima na busara angesubiri baada ya 2020 kwa sababu anafahamu huu utawala hauna jipya.
Watu kama mimi tungebaki na matumaini yetu kwa sababu tunaamini we are at war with the army we have (Rais Magufuli), not the army you might want or wish to have at your irrational thoughts and ideas!
Hapana suala la muda ni jambo binafsi na sioni linajibu vipi Lugumi.Kuendelea kukosoa serikali uliyosema toka siku ya kwanza haina jipya huku umejificha katika vazi la uzalendo ni kuendeleza unafiki tu au kupoteza muda wako adhimu.
Hewalaa, ni mkataba wa umma, penye utata nini kinafichwa? Halafu una uhakika gani kama Polisi wanao?Ukweli wa Mkataba wanaofahamu ni polisi na Lugumu.
Sijui kabisa, ndio maana nashangaa kwanini mwezi mzima kuna kutupiana mpira, na baada ya wiki takribani tatu 'mwenye makataba' kwa mujibu wako anakuja na maswali badala ya majibu?Kwa hiyo unataka kutuambia unafahamu yote kuhusiana na mkataba wa polisi na Lugumi?
Wapi mtazamo waangu nimeuita sharia au mwamvuli kwa wananchi?Huu
ni mtazamo wako ambao hauwezi kuwa ni sheria au mwanvuli kwa kila mwananchi.
Bandarini chereko, TRA chereko, Darajani kicheko, wafanyakazi hewa nderemo. Lugumi kimyaaa!Eti tutashindwa mahala pa kusimama. Huoni kama kusema tutashindwa pa kusimama ina maana kuwa kwa sasa tuna mahali pa kusimama au kwa maana nyingine unasema, The President is doing fantastic job.
Mimi jinga Fulani linalohoji mambo yasitokiwa. Nafiki Fulani lisilokubali kuimba wengine wakiserebuka.Kama mimi ni mshangiliaji, wewe ni nani?
Network inaonyesha Kama alishawahi ku commit crime kwengine etc.Kuchukua alama za vidole na vitu kama hivyo kama DNA haitaji any connectivity zaidi ya equipment za sehemu husika....analysis yake ndo inaweza kuhitaji connectivity na server ku fetch na compare na saved data.
Anyway kama hii ilikuwa ndio mradi ulivyotakiwa kuwa(Synchronized System) maana yake mradi haujakamilika na jamaa wamelipwa pesa yote. Ndio maana ni muhimu kujua mkataba ulikuwaje internet ilikuwa sehemu ya SOW au ni contractor mwingine alikuwa anafanya?
Ndio maana hawajamaliza kulipwa pia. Hakuna haja ya kuwa na kihelehele cha kushusha tuhuma nyingi wakati kamati itatujuza chamno ni nini kilichofanya swala hili kuchukua msukumo mkubwa kutoka kwa wanahabari.Kuchukua alama za vidole na vitu kama hivyo kama DNA haitaji any connectivity zaidi ya equipment za sehemu husika....analysis yake ndo inaweza kuhitaji connectivity na server ku fetch na compare na saved data.
Anyway kama hii ilikuwa ndio mradi ulivyotakiwa kuwa(Synchronized System) maana yake mradi haujakamilika na jamaa wamelipwa pesa yote. Ndio maana ni muhimu kujua mkataba ulikuwaje internet ilikuwa sehemu ya SOW au ni contractor mwingine alikuwa anafanya?