IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza mkataba wake na Jeshi la Polisi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,533
3,186
Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”
 
Hapa ndipo IGP amejipalia mkaa na asipokuwa makini hii story itamletea maneno mengi mpaka atajuta kusema hadharani, hivi Thamani ya hivyo vifaa ni bilion 34 ? Uchunguzi uliofanyika kwa kiina Thamani ya Hizo mashine haifiki hata bilion 1 , pesa nyingi ilizidishwa ikaliwa na wajanja wakagawana na sasa ndiyo inatumika kuwanunua wote wanaotumwa kulichunguza hilo sakata, Rushwa imetembea sana na baadhi ya mashine zimefungwa chapchap kwenye Vituo ili kumlinda Said mwema na hii Aibu , lakini Ukweli harisi pesa aliyopewa Lugumi haiendani na Thamani ya hizo mashine bali pesa nyingi imeliwa na wajanja wachache kisha kuleta vifaa ili kuwahadaa Watanzania.
 
Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.
mkuu huo mladi ulibuniwa kwa lengo la kupiga pesa hizo mashine Thamani yake harisi ni kidogo sana.
 
Anafunika uovu wa waliomtangulia siyo!
Muda wote alikuwa kimya, walikuwa wanaweka nyaraka vema
Kama ilikuwa ni hivyo, kwanini mkataba umekuwa nongwa kuwekwa hadharani?

Kwanini afisa wake ameitwa na PAC na kushindwa kujibu hadi kuundwa kamati ndogo?

IGP asituambie eti kazi imemalizika, anatakiwa atuambie tenda ilitangazwa lini, malipo yalifanyikaje na mkataba mzima unasemaje

Tuliwaambia Watanzania kuna jambo!
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”
Zimeshaletwa fasta nini? Tusubiri tuone mwisho wa hili.
 
Si kuna kamati ndogo ya PAC imeundwa kupita kila kituo kuona kama mashine hizo zipo zilifungwa na kufanya kazi, au?

Anajihami kwa lipi ndugu IGP? Awasubirie wanakamati huko huko kwenye vituo vyake na kuwaonesha hizo mashine.

Hata kama Lugumi hakuwa amezifunga, wamwambie afanye fasta kuzifunga kabla kamati haijawafikia. Hata hivyo akumbuke tu kuwa, siku zote siku za mwizi ni 39 ya 40 ananaswa!!
 
Back
Top Bottom