IGP awaomba radhi Wanahabari, asema kuwakamata wakiwa katika kazi zao si msimamo wa Jeshi la Polisi

Hivi M. gambo hawezi kubeba hii lawama? Binafsi siwalaumu askari bali yule aliyewapeleka/watuma.


Hapa inatakiwa M.gambo apigwe pin sawasawa na wachukua nauli kwenye daladala.
 
awachukulie hatua kwa ujinga walioufanya ili iwe fundisho kwa wngine
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu, amesema vitendo vya polisi kuwakamata waandishi wa habari wanapokuwa katika majukumu yao ya taaluma siyo msimamo wa jeshi hilo bali ni bahati mbaya.

Alisema waandishi na vyombo vya habari ni wadau muhimu wa jeshi hilo lazima washirikiane nao.
IGP Mangu ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho la wakuu wa Polisi wa nchi Kusini mwa Afrika (Sarpcco) unaondelea Arusha.

“ Askari wanapokuwa katika eneo la tukio anakuwa na tabia fulani ambayo kila mmoja wetu anayo ya kulazimisha mambo. Ninyi ni wadau wetu lazima tufanye kazi pamoja hatuna ugomvi wowote na waandishi wa habari”. Alisema Mangu

“Yanapotokea matukio ya aina hiyo ya kukamatwa au kusumbuliwa tujulishane kwa sababu askari wadogo wakati mwingine hufanya vitu ambavyo siyo msimamo wetu sisi viongozi”. Alimalizia kusema IGP Mangu.

Chanzo: Kwanza Tv
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Uungwana ni vitendo.. Nilikuwa nashangaa jamaa wanakosea matukio mengi, lakini kwanini kuomba kwao msamaha ni nadra.!
 
Dah waandishi wakikugomea sijui unaanzaje kuwapa wananchi taarifa labda utakuwa unaitisha mkutano wa hadhara
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom