Ignorance is bliss

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,031
1,603
Kuna wakati ujinga inakuwa ni faida kwa mjinga. Nikitafakari tukio la shambulizi lilofanywa kwa Lissu mchana kweupe kwenye nyumba za viongozi tena penye geti linalolindwa 24/7, nabaki nashangaa.

Geti ambalo siku zote lina ulinzi, na siku zote mgeni hawezi ingia mpaka askari wapate maelezo ya yeye ni nani, anakwenda kwa nani, askari uwasiliana na familia ya kiongozi husika ili akiridhia ndo mgeni huyo uruhusiwa kwenda lakini kabla ya hapo askari uandika kwenye kitabu chao majina ya mgeni, namba za gari, na time in.

TUNAMBIWA KWAMBA SIKU HIYO GETI LILIKUWA WAZI NA HAPAKUWA NA ASKARI!!!!!!!!!!!.
Anayetoa hayo majibu anaridhika kwamba ametoa majibu.

Serikali kupitia waziri wa afya inasema ipo tayari kumtibia Lissu popote duniani.Tamko hili linakuja wiki mbili toka alipopigwa risasi. Tena linatoka kwa watu walioisha sema kwamba kwakuwa amepelekwa Nairobi badala ya Muhimbili, basi serikali haitoshughulika na matibabu yake. HUYU NAYE BAADA YA KUSEMA HAYO KARIDHIKA KWAMBA AMETOA UFAFANUZI.!!!!!!

Jaji mkuu kasema kuhusu uchunguzi wa tukio hili, tusilete Scotland Yard, tutumie vyombo vya ndani. Huyu ni mtu wa mahakama. Shauri hili halijaenda mahakamani. Duniani kote, majaji huwa siyo watoaji wa matamko kwa mashauri nje ya mahakama. Wao utoa hukumu kisha ukaa kimya. Huyu wetu kaapishwa juzi. HUYU MZEE KASEMA HAYO NA YUPO ANAKULA CHAKULA CHAKE AKIIMANI KWAMBA KAJIBU SWALI KUHUSU LACK OF CONFIDENCE IN OUR POLICE.

Polisi hawajamkamata yeyote maana taarifa za kiitelegensia bado hazijawafikia japo waendesha bodaboda wanasema siku ya tukio trafiki walizuia magari ili wavamizi wapate njia ya kukimbia mara baada ya kumuangamiza Lissu. Polisi wapo wanamsubiri dereva wa Lissu. HAWA NAO WAMERIDHIKA KWAMBA KWAKUSEMA WANAMSUBIRI DEREVE WA LISSU, BASI WAMETIMZA WAJIBU WAO!!!!

Nikayaangalia haya, nagundua kwamba kumbe ujinga ni baraka.
 
Back
Top Bottom