Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Labda ni Tanzania pekee ambako kila siku askari wanasimamisha gari ili watafute kosa kuhusu wewe dereva au gari. Ni kwamba askari anapoamua kusimamisha gari, dereva unakuwa huna kosa aliloona, bali utakaposimama ndio ataanza kutafuta kosa ambalo atakuambia ulilipie faini. Naendesha gari, nafuata kila sheria, gari yangi nzima, halafu unanisimamisha ili unitafutie kosa, kwa nini? Una chuki gani na mimi?
Huu ni uratibu mbaya na haufai, na unakuwa mbaya zaidi pale ambapo unafanywa kama jambo la kawaida la kila siku. Ikiwa huu utaratibu wa kusimamisha gari ili kutafuta kosa ungefanywa wiki ya "Nenda kwa Usalama" wala tusingeona shida. Lakini sasa, kwa nini jeshi la polisi limeamua kwamba haya ndiyo yatakuwa maisha ya kila siku ya wanaoendesha magari?
Je lengo ni nini hasa? NI kwamba serikali imefulia au kufilisika kabisa kiasi kwamba Raisi ametoa agizo kwamba askari watafute hela kwa kuwasumbua wananchi kiasi hiki? Je Raisi au mawaziri hawaoni hii ni kero kwa wananchi kwa kuwa wao hawaguswi na kadhia hii? Ni sawa na Ni sawa na kutembelea Ofisi za TRA na kuwauliza wafanyakazi kama wamepokea rushwa ili uwachukulie hatua!
Kwa nini lakini Raisi Magufuli anaifanya Tanzania kuwa nchi yenye kero na usumbufu usio na msingi? Ana hasira ya kuchaguliwa kuwa Raisi?
Basi sisi kama wananchi tuna ujumbe kwa Raisi Magufuli. Tunaelewa kwamba usalama barabarani ni jambo muhimu, lakini huu usumbufu sio wa lazima ni kero ambayo tusingependa kuwa nayo katika nchi yetu huru. Kama askari wa trafiki wanataka kukaa barabarani basi wasimamishe gari ambazo zinakuwa zimefanya kosa fulani. Sio kunisimamisha ili uanze kutafuta kwa kila namna kosa la kunipigia faini. Huu ni ukandamizaji na unyanyasaji (opression and harassment) ndani ya nchi yetu wenyewe unaopaswa kupingwa kwa nguvu zote na wananchi huru wa Tanzania.