Ifike Mahali tumheshimu Jakaya

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,109
2,000
Huyu jamaa kwani aliwazaje kuongoza nchi iliyojaa ufisadi kiasi kile, lakinin ajira zilikuwepo za kutosha, mishahara ikawa inapanda kila mwaka, makodi na matozo ya kukomoana haya yalikuwa hayapo, Demokrasia ilitawala na watu walikuwa na pesa.

Tangu atoke wameingia hawa wawili ambao wanatuambia ufisadi umepungua lakini maisha tait, ajira hakuna, mishahara haipandi, tozo na kodi za kukomoana ndo usiseme..

Nadhani Jakaya anastahili heshima kubwa sana kt nchi hii
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,156
2,000
Wakati wa JK hakukuwa na ufisadi mwingi kuliko serikali ya BWM, ila tu JK aliruhusu uhuru wa maoni, Aliruhusu demokrasia na upinzani ukawa huru kumsema utakavyo, na aliruhusu kuwepo kwa bunge lenye meno ndiyo maana ulisikia habari za ufisadi . Kama angetaka na yeye angedhibiti vyombo vya habari, angeliburuza bunge, na angepoteza wanaompinga waziwazi hayo mambo ya ufisadi usingeyasikia.

Nikukumbushe tu ufisadi wa EPA, Meremeta, Kuuza nyumba za serikali bei chee, Mikataba mibovu ya madini, Rada, Ndege ya Rais, Kujimilikisha mgodi wa Kiwira, Deep green, Ufisadi wote huo ni wa kipindi cha BWM
 
Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
2,932

Lakini Katibu wetu Mkuu Kamanda Mnyika aliweka bayana JK alikuwa Rais dhaifu.Au ndiyo tuseme tumebadili gia angani tena?
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,915
2,000
Kwakweli lipo la kuijiuliza

Maabara nchi nzima

Kulipa mishahara warumishi hewa(kibwagizo cha magufuli)

Kupandisha mishahara

Kuajiri kwa mkupuo

Ufisadi watu walijipigia tu mifwedha

Mavieitte yalimwagwa

Malendikruza hadi serikali za mitaa huko wakurugenzi wanapiga mnada wanaletewa mapya

Aliwezaje?
 
Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,532
2,000
IMG_0123.JPG
 
baba-mwajuma

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
485
1,000
Siku Zote Jakaya aliamini Watanzania best Duniani ndio wataiinua Tanzania, alichukua watanzania Toka Taasisi kubwa Duniani na kuwa rudisha Nchini ikiwemo pia watu wengine ambao wapo vizuri kwenye kazi zao.

Tido Muhando alitolewa BBC akaletwa TBC, Tv ya taifa ikawa nzuri tukaletewa Nchi nzima mpaka wa Vijijini tukaiona, vipindi vya kisasa mpaka ze KOMEDI tukaletewa, watu wakamletea Figisu Leo yupo Azam tunaona Kazi yake isiobabaisha.

Nehemia Mchechu Alikuja na NHC japo kulikua na Malalamiko ya hapa na pale ila Tuliona Shirika likifufuka, miradi mikubwa mikubwa ikijengwa, nk

Kila Sehemu Jakaya alijaza Mind ambazo zimeprove sehemu kwamba wao ni best kwenye fani zao.

Leo hii sifa ya kiongozi ni kusifu na kuabudu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom