Naunga mkono hoja kwani hawa wazee wanaojifanya wana hekima na busara ndo kabisa wanaturudisha nyuma zaidi ya miaka 50. Hebu tufikirie tu wenyewe shule ya serikali inakosa madawati wakati misitu tunayo ya kutosha kabisa hapa Tz lakini magogo yanpakiwa kwenye meli kupelekewa wazungu as if ni wa maana sana kuliko watz; wizi mtupu.
Hata zile chache zenye madawati yanachangwa (kama hela) na wazazi wa wanafunzi kwa kila mwanafunzi anayeingia shule, hata dawati lenyewe halinunuliwi kwani waliotangulia wakati shule inaanza waliacha madawati yao, wizi mtupu kwani akimaliza harudishiwi dawati lake na kila atakaeingia atachangishwa kama kawa.
Swala la rushwa na ubadhirifu (ufisadi) imekuwa ni nomo praktisi, inafanywa wazi wazi bil hata uficho na bahati mbaya ikigundulika aliyehisika ataambiwa arudishe kwa hiari na hata asiporudisha hachukuliwi hatua yoyote, wizi mtupu.