Ifikapo 2015 wasomi tusiogope kugombea ubunge kupitia CHADEMA

Wasomi ni watu wenye vigezo gani?

Mwalimu unauliza msomi ana vigezo gani? Lakini cha muhimu nafikiri mleta mada angesema wenye uelewa na uchungu wa nchi hii maana tunao wasomi na ndio hao walio tuifikisha hapa.
 
Mi sio msomi ila ntagombea jimbo langu na watz wenzangu wanajua kuwa nina akili timamu na ninajua kusoma na kuandika, nia na uwezo wa kugombea ninao. Na ni kijana mwenye nguvu.
 
Mwalimu unauliza msomi ana vigezo gani? Lakini cha muhimu nafikiri mleta mada angesema wenye uelewa na uchungu wa nchi hii maana tunao wasomi na ndio hao walio tuifikisha hapa.

Nauliza kwa sababu kila mtu ana vigezo vyake. Kuna sehemu nyengine aliyefika Form Six ni msomi wakati wengine kama hawajasikia PhD hawajaona kama msomi

Wengine waliosomea mambo ya kiimani katika taasisi zisizokuwa rasmi ni wasomi na wengine huwaita wasomi wale wenye vyeti vya taasisi zilizorasimiwa tu hata kwenye mambo ya ki taaluma

Kwa hiyo anaposema msomi ana vigezo gani? Ili tusijekuwa tunazungumzia watu tofauti bila ya kujijua

Suali linalofuatia ndilo hilo uliloliulizia, usomi pekee ni kigezo tosha?
 
Mi shy town lazima nikinukishe aise! huyu Masele lazima achape rapa!! kama yupo humu nasema kabisa haibiwi mtu kura 2015!!
 
Sijaona kijana wa Kumtoa jamaa wa Morogoro mjini, Monduli, bariadi mashariki!! vijana jitokezeni tuanze mikakati mapema
 
Nauliza kwa sababu kila mtu ana vigezo vyake. Kuna sehemu nyengine aliyefika Form Six ni msomi wakati wengine kama hawajasikia PhD hawajaona kama msomi

Wengine waliosomea mambo ya kiimani katika taasisi zisizokuwa rasmi ni wasomi na wengine huwaita wasomi wale wenye vyeti vya taasisi zilizorasimiwa tu hata kwenye mambo ya ki taaluma

Kwa hiyo anaposema msomi ana vigezo gani? Ili tusijekuwa tunazungumzia watu tofauti bila ya kujijua

Suali linalofuatia ndilo hilo uliloliulizia, usomi pekee ni kigezo tosha?

Ahsante sana GJ naona tuweke viwango vya usomi na uelewa na uchungu kwa nchi yetu.
 
ile miposho naweza mi nataka jimbo la selasini maana jamaa aliniboa kwenye ishu ya posho...kwani lazima niwe mchaga kugombea rombo?
ishia hapohapo.....wa2 tumeshajipanga kwa ushindi wa kishindo 2015 af we waleta habari zako?? LOL!
 
Mwaka elfu 2010 vijana wa chadema (Mnyika, Wenje, Mdee, Zitto n.k) waligombea nafasi ya kuwania ubunge kupitia Chadema na kufanikiwa kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, nashauri vijana chipukizi wanaomaliza Vyuo kuwaiga vijana tajwa hapo juu kwani wametuonyesha njia. Tuchangamke inawezekana kuwabwaga wazee wa ccm. John Heche, Dr. Kitila Mkumbo, Deus Kibamba msituangushe changamkeni.

Mi niko tofauti na wewe... Nataka ama nashauri vijana wajitokeze kwa wingi kugombea ubunge,kwa vyama vyote...
Once ukiongelea vijana, basi usibague... Utofauti wa vyama utakuja kwenye utendaji na utekelezaji wa ilani ya chama kilichopo madarakani... Na wote,watafanya maamuzi bora kwa ajili wanachi,na Taifa kwa ujumla.
 
Mwaka elfu 2010 vijana wa chadema (Mnyika, Wenje, Mdee, Zitto n.k) waligombea nafasi ya kuwania ubunge kupitia Chadema na kufanikiwa kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, nashauri vijana chipukizi wanaomaliza Vyuo kuwaiga vijana tajwa hapo juu kwani wametuonyesha njia. Tuchangamke inawezekana kuwabwaga wazee wa ccm. John Heche, Dr. Kitila Mkumbo, Deus Kibamba msituangushe changamkeni.

kama nia unayo jitambulishe sasa,
2015 utakuwa umechelewa-Unaweza kuwa mzuri lakini ukaonekana mamluki. muda huo si mzuri kuna mengi yanajitokeza.
Nenda ktk uongozi wako wa wilaya/mkoa na uanze kushiriki shughuri za chama.
Mikakati mbali mbali ya kukitangaza chama hasa mikoani pia ushiriki.
Hata ukikosa Ubunge tutakufukiria kwenye ubalozi kama usomi wako tutaona unafaa.
Shukrani kwa kuonesha nia.
 
mi nadhani hoja ya usomi isipoteze mantiki ya mtoa thread... Hoja ni vijana wajitokeze... Maana kama ni usomi,hata wazee wapo waliosoma mpaka ukiongea nao,kazi kunukuu vitabu...
So there is no need,and it is unnecessary to diverge the course of the thread..
 
Mi shy town lazima nikinukishe aise! huyu Masele lazima achape rapa!! kama yupo humu nasema kabisa haibiwi mtu kura 2015!!
Masele alishindwa hilo liko wazi, ila jamaa walipoona Shy ingekuwa ni mkoa pekee ulio na majimbo zaidi ya matano yakiwa chini ya CDM. Waliyabaka matokeo na kwa kweli kufariki kwa Jembe letu Shilembi pale Shy ndiyo pona yao
Kumbuka hata Kahama ilikuwa kama Shy na hilo pia ni destinanion nzuri kuitarget.
Jimbo la Nsalala linafika mpaka Isaka huku Maige(waziri mwenye kashfa maliasili) anang'oka mkijipanga wana shy.
Jimbo la Nsolwa lina Mwarabu std iv-Inamaana hakuna watu Tinde,Didia,Mwantini na Iselamagazi-Nindo? Come on-please fanyeni kweli.
 
Vijana wote wana haki ya kugombea sio wasomi tu,na mnaposema wasomi mnaamanisha nini? maana hata aliyemaliza la saba kasoma naye ni msomi pia. cha muhimu wale waliobobea katika fani mbali mbali wabaki kuwa washauri na watendaji katika wizara na sekta mbali mbali,hapo tutasonga mbele. HUO NI MTAZAMO WANGU

Hao wasomi wa darasa la saba akina Professor Maji Marefu hivi kweli wanaelewa miswada inayopelekwa bungeni??? No woder miswada inabidi ibadilishwe na kupelekwa kwa kiswahili kila siku. Nimeshangaa leo kwa Michuzi nimekuta Professor ni mjumbe wa kamati ya Bunge.
 
Yeyote mwenye kuhitaji kugombea nafasi yoyote kupitia CHADEMA, dawa ni kuanza sasa hivi kufanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi pamoja na uongozi wetu huko huko mashinani.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba wala usipoteze muda kuwapikia wengine majungu kwa uongozi wa juu taifa maana jibu la nani atakua mgombea wetu uko hapo hapo ulipo mashinani.
 
Back
Top Bottom