Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi achukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patribas Katambi amechukuwa form kuwania kiti cha ubunge shinyanga mjini , patrobas katambi amekuwa mtiania wa 49 shinyanga mjini huku wanaitajwa kuwa na nguvu ndani ya chama wakitajwa ni gasper kileo na Steven masele.

=======
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi leo Jumatano Julai 15,2020 amechukua Fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwaka 2015 akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi aligombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA,hata hivyo Stephen Masele (CCM) aliibuka mshindi kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na mwaka 2017 Katambi alijiunga CCM na baadaye kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.


 
Wanajua kucheza na fitina ni hao waliotajwa ,wajumbe mifuko yao IPO waz kusubria watafanya nn
 
Huyu domo zege kutongoza kwenyewe hawezi ndiyo awe mbunge. Atajenga vipi hoja
Kwa sura kama hii yako, walahi naweza kutafuta hata mganga anisaidie!
JamiiForums1434294729.jpg
 
anakosa vyote, kwanza hajaoa anajua baada ya uchaguzi kupita Rais hatakuwa tayari kuteua au kubakia teuzi za MABACHELOR, mabachela mwisho wake mwezi wa kumi. Kwenye ubunge hata wazinzi wasiooa wagombee tu

Nasikitika mkurugenzi wake wa jiji bado hajaoa hadi sasa, sijui nyumba za serikali huko uzunguni kama zipo salama sana......hakuna uchafu huko,watulie waoe kwanza mengine baadae
 
Hahahahahaha umeshawahi kuwa mshuhuda kwenye MITONGOZO yake ukaona anabwabwaja povu tu? By the way hivi kuna Mbunge wa maccm anayejenga hoja siku hizi? Ni mbunge yupi au ni Wabunge gani hao wa maccm wanaojenga hoja zaidi ya kupiga kelele kwenye kila UPUUZI ndiyoooooooo/

Huyu domo zege kutongoza kwenyewe hawezi ndiyo awe mbunge. Atajenga vipi hoja
 
Hujui watu wewe kaa kimya

Watu wapo kazini

Unadhani alikuwa CDM huyu, ndio makosa mnafanya CDM

Watu wapo kazini,endeleeni kuvamia watu,nchi hii ilijengwa na Nyerere.

Period
Hata sijui wapinzani watajifunza lini!
 
Back
Top Bottom