Ifahamu water witching na maajabu yake

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Water witching au kwa jina lingine inafahamika kama dowsing ni Njia maarufu na ya kale inayotumika kutambua uwepo wa maji chini ya ardhi ,Yani kama unataka kuchimba kisima Cha maji sasa ili kutambua ni sehemu gani Kuna mwamba wa maji unatumia Njia hii .

Njia hii inasemekani ni ya muda mrefu sana inakadiliwa kuwa iligundulika miaka 4000 iliyopita ila Mimi binafsi ndio nimeifahamu sasa sikiwahi kusikia hapo kabla

Inavyofanya kazi Nadhan na wewe itakushangaza kama ilivyonishangaza Mimi kwa mara kwanza, hakuna uchawi unaofanyika ila sijui kitu gani kinasababisha mwenywe sijapata jibu

Jinsi ya kufanya tafuta kijiti au kitawi Cha mti kidogo chenye pacha mbili then kashike kwa kuinua juu kama unavyoona kwenye picha
Screenshot_20230415-214613.png

Kisha anza kupiga hatua za taratibu kwa kwenda mbele ,kama utaona kijiti kinatazama chini chenyewe kama kimewekewa kitu kizito.
Screenshot_20230415-215152.png

Basi hio ishara kuwa hio sehemu Ina maji chini ya ardhi lakini hautajua yapo kiwango gani na umbali gani labda kama utatumia na Njia nyingine za kisayansi

Usahihi wake
Binafsi Bado sijafanya practice lakini baada ya kufanya utafiti mdogo mtandaoni nikaona baadhi ya watu wamethibitsha kuwa ni kweli inafanya kazi kwa kalibia 100% .

Wakwanza alifanya experiment ya kwa kuweka chupa yenye maji juu ya ardhi(surface) kisha akapita na kijiti alivyofika usawa wa chupa kijiti kikainamia chini ya chupa

Na mtu wa pili naye alifanya hivyo hiyo ila huyu alienda mbali zaidi akaita wataalamu na vifaa vyao matokeo yalionyesha ni kweli Kuna maji.

Pia Kuna Njia kama hii lakini ni kwa ajili ya kutafuta vyuma vilivyofukiwa chini ya ardhi jinsi ya kufanya tafuta vyuma vidogo wili vyenyewe umbo namba saba au L ,then vishike kama inavyoshikwa bastola mikono miwili na anza kutembea taratibu
4729.jpg

Ukifika sehemu yenye chuma chini ardhi vyuma hivyo vidogo vitagusana na kutengeneza umbo la X.
Screenshot_20230415-214330.png

Njia zote hizo ni za kale na zimethibitishwa zina ufanisi mkubwa ila Bado najiuliza maswali ni kitu gani kinasababisha kijiti kiiname.

Tazama baadhi ya hizi video.

Ila ipo effective kwa maji yalio karibu na ardhi (water table) sio aquifers.

Za copper rods ndio unyama. Nilivojaribu sikuamini tukapiga VES ikasema maji yapo pale pale. Nilinyoosha mikono.
Duh Mimi ndio nimejua leo mkuu hicho kitu tena baada ya kuona video YouTube,nikafanya tafiti ndogo ndio nikayajua haya machache.

Hiyo ya copper nayo inapima yakiwa kwa umbali gani?
 
Duh Mimi ndio nimejua leo mkuu hicho kitu tena baada ya kuona video YouTube,nikafanya tafiti ndogo ndio nikayajua haya machache.

Hiyo ya copper nayo inapima yakiwa kwa umbali gani?
Hiyo ya vijiti na maji Wana wakifanya kitambo Sana,1990s huko..nilishangaa
 
Nime pitia wikpidia, ilianza kumbe toka miaka ya 1500 ilipigwa marufuku na utawala wa kikatoriki na matin ruther kwenye makanisa yetu kuwa ni ushirikini na upigaji lamli
Mwaka 1568 huko spain Teresa alienda sehem ambayo ilikuwa haina maji kuna jamaa anaitwa Friar Antonio akaenda na kitawi chake kwenye uwanja na akaonesha ishila ya msaraba kisha akatembe kitambo kidogo akamwambia mtu chimba hapa kweli wakapata maji ya kunywa, ila Teresa anasema hana uwakika kama alionesha alama ya msaraba hii inapatika katika kitabu cha Psychical Research 1911 kilicho andikwa na sir william F barret
Achia mbali dini zetu uko ujerumani njia hii ilianza kutumika toka 16 century kama inavyo tumika leo kutafutia vyuma ardhini
Pia 20's & 21's century dowsing inatumika jeshini ku-detect vilipuzi ardhini kama ADE 651, Sniffex na GT200
Kumalizia mwaka 1999 the United States National Institute ilitoa ushauri kupigwe marufuku uuzaji wa vifaa vinavyo support dowsing
 
Aisee kumbe hiki kitu ni ancient hivi sijui kuna nguvu gani kati inafanya haya yote.

Bado sijajua sayansi ina majibu gani juu ya hili , Ngoja niendelee kufanya utafti.
 
Ipo na ile ya kutumia yai
Yai la kuku lile jepesi ila sifahamu kama ndiyo yai viza au inakuaje
Unaliweka kwenye kiganja linakuwa limelala,unatembea uelekeo wowote ila kama sehemu kuna maji linasimama lenyewe hapo kwenye kiganja chako
Hii nimewahi kuifanya ni uhalisia unaweza kujaribu..
 
Acha utani mkuu yai litasimama wima lenyewe kabisa...
 
Mkuu,
Lina simama au lina tulia (kuto tingishika)?
Ipo na ile ya kutumia yai
Yai la kuku lile jepesi ila sifahamu kama ndiyo yai viza au inakuaje
Unaliweka kwenye kiganja linakuwa limelala,unatembea uelekeo wowote ila kama sehemu kuna maji linasimama lenyewe hapo kwenye kiganja chako
Hii nimewahi kuifanya ni uhalisia unaweza kujaribu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom