Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,542
- 3,451
- Thread starter
- #21
Karanga zinapendwa sana na kuvu...Asilimia kubwa ya wabongo wanaweza wasiwe exposed kwenye kiwango kikubwa cha aflatoxin na aina nyingine za sumu kuvu kutokana na kula ugali wa sembe, kukoboa mahindi kunapunguza sumu kuvu kwa kiwango kikubwa sana. Kwa wale wanaopenda dona, ni bora ukaandaa mahindi yako mwenyewe, ukaaondoa yale mahindi mabovu, ukaosha na kuanika kabla ya kwenda kusaga.
Kwa sababu karanga zinaweza kuwa na kiwango kikubwa cha aflatoxin, inafaa kuzichambua na kuondoa zile mbovu na zilizosinyaa. Kwa wale wanaoandaa unga kwa ajili ya watoto wawe makini zaidi kuchambua mahindi na karanga kwa ajili ya kusaga unga kwa ajili ya uji wa mtoto, nafikiri tumeelewana ndugu zanguni....