TBS na SUMUKUVU: Vichochezi, Madhara na Udhibiti wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,230
2,000
SUMUKUVU, VICHOCHEZI,​
MADHARA YAKE NA UDHIBITI
________________________________
______
19 AUG, 2020
USUNGILO HOTEL
(Yusto Wallace)
Utangulizi

Shirika la Viwango Tanzania (TBS)​

Ni shirika la umma chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, lililoundwa chini ya Sheria ya Viwango, Nambari 3 ya mwaka 1975, na kuanzishwa upya chini ya sheria ya Viwango Nambari 2 ya mwaka 2009.

Sheria mpya ya viwango (namba 2 ya mwaka 2009) imelipa shirika uwezo zaidi wa kuchukua hatua kwa wahusika endapo itabainika uwepo wa ukiukwaji wa taratibu za uthibitishwaji ubora na usalama wa bidhaa zinazotumika nchini Tanzania.
Sababu gani zinazochochea mazao kuchafuliwa na sumukuvu?
1615104180112.png
1615104249673.png

Mazingira yenye joto na unyevunyevu mfano katika nchi za ukanda wa tropiki kama vile Tanzania ambapo hali ya hewa ya joto na unyevunyevu huchangia kuota kwa fangasi hao.
Sumukuvu hutokea kwenye mazao wakati gani?
Wakati mazao ya chakula yakiwa shambani kabla na baada ya kuvunwa na pia wakati wa kusafirisha au kuhifadhi.

Unawezaje kugundua mazao yaliyoathiriwa na sumukuvu?
Sumukuvu haionekani kwa macho, haina harufu wala radha.

Uwepo wa ukungu (fangasi) katika mazao ni ishara kwamba mazao husika yatakuwa yamechafuliwa na sumukuvu.
Mazao yenye fangasi au ukungu hubadilika rangi na kuwa na weusi au kijivu kiasi.

Huendelea kubaki kwenye mazao yaliyochafuliwa na sumu hizo hata baada ya chakula kusindikwa au kwakupikwa.

Aina mbalimbali za sumu kuvu.

•Aflatoxins,
•Fumonisins,
•Deoxyivalenol,
•T-2 toxin
•HT-2 toxin,
•Zearalenone,
•Ochratoxin A
Mazao yanayoathiriwa na sumukuvu
Nafaka: Mahindi, Mtama, Uwele
Mbegu za mafuta: Karanga, alizeti, pamba
Viungo: Pilipili, Pilipili manga, Binzari (manjano)
Vyakula jamii ya mizizi vilivyokaushwa: Mihogo
9​
Madhara ya kiafya
Hujitokeza baada ya muda mfupi au mrefu kutegemea na muda uliotumika, kiasi cha chakula kilicholiwa na kiwango cha sumukuvu kwenye chakula hicho, umri na hali ya afya ya mlaji.
Madhara baada ya muda mfupi
mtu anapokula chakula kilichochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu.
Dalili ni:(a) Maumivu ya tumbo (b) Kutapika (c) kuvimba tumbo (d)Homa (e) Kuharisha (f) Degedege (g) Kuwa manjano sehemu mbalimbali za mwili (mfano viganja, nyayo na macho) Madhara haya huweza pia kusababisha kifo.

Madhara........
Madhara baada ya muda mrefu
Mtu anapokula chakula kilichochafuliwa na sumukuvu kwa kiasi kidogo kwa muda mrefu.
Madhara hayo ni pamoja na:
Saratani ya ini, figo na koo
Kuathiri kingamwili
Kuathiri ukuaji wa watoto chini ya umri wa miaka 5 (udumavu).
Athari za aflatoxins kwenye sekta ya mifugo
Hupunguza uzito wa kuzaliwa na huweza sababisha athari ya ulemavu katika mifugo.
Hupunguza uzalishaji wa mayai, hupunguza uzito wa mayai na huongeza idadi ya vifo kwa kuku
Hupunguza uzalishaji wa maziwa, huongeza maradhi na kupunguza uzazi
Mifugo ikipewa chakula chenye uchafuzi wa sumukuvu, sumukuvu hio huweza kupatikana katika vyakula vitokanavyo na mifugo kama vile maziwa na nyama.

Athari za sumukuvu katika sekta ya uchumi
Kupungua kwa nguvu kazi
Uzalishwaji mdogo wa mali ghafi
Ongezeko la gharama za matibabu kwa magonjwa kama saratani
Uharibifu wa chakula
Kukataliwa kwa bidhaa za chakula katika soko la kimataifa

Viwango vya udhibiti kwa mujibu wa TBS au
Codex
Aflatoxin B1 = 5μg/kg ( mikrogramu 5 kwa kila kilo moja ya mahindi)
Aflatoxin jumla (B1 + B2 + G1 + G2) = 10μg/kg (mikrogramu 10 kwa kila kilo moja ya mahindi)
Fumonisins 2000μg/kg
Deoxynivaleno 750 μg/kg
HT-2/T-2 au zote kwa pamoja = 50 μg/kg
OTA = 3 μg/kg
ZEA = 75 μg/kg
15​
Mbinu za kukabiliana na sumu kuvu
Huitajika mikakati
Mazao yakiwa shambani
Baada ya mazao kuvunwa

Tatizo la uchafuzi wa sumu kuvu ni mtambuka.
Ushughulikiaji wa tatizo huitaji ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika mnyororo wa chakula kama vile;
Kilimo
Afya
Wafanyabiashara
Walaji
n.k

1. Mazao yakiwashambani
Matumizi ya kanuni bora za kilimo imethibitika kupunguza viwango vya sumu kuvu katika mazao kabla ya kuvunwa shambani kama vile;

Matumizi sahihi ya viuatilifu
Kutumia mbegu bora/vumilivu
Kuvuna kwa wakati sahihi
Kuepuka mkusanyiko wa mazao yanayovunwa sehemu moja
Uondoaji wa mabaki ya mazao yaliyoathiriwa shambani kabla ya msimu mpya kuanza.
Matumizi ya mbinu za kibaiolojia (atoxigenic strains of fungi* ili kudhoofisha fangasi wenye kusababisha sumu kuvu katika mashamba.

2. Baada ya mazao kuvunwa
Ukaushaji wa haraka nafaka baada ya kuvunwa ili kupunguza kiwango cha unyevunyevu kabla ya kuhifadhiwa gharani;
Note: Uchafuzi wa sumu kuvu hutokea gharani endapo kiwango cha unyevunyevu kitazidi 13%.
Usafi – wakati wa kukausha na kuhifadhi nafaka gharani
Kuchambua na kuharibu mbegu zinazoonekanaka kuathiriwa na fangasi, kubadirika rangi na zinazoharibika kabla ya kuhifadhiwa gharani.
Kukausha mazao juu ya vichanja (epuka kukausha mazao chini kwenye udongo)
Kuondoa/kuua wadudu wakati wa kuvuna, kusafirisha na kuhifadhi nafaka
Kuepuka kiasi cha unyevunyevu kilicho juu sana zaidi ya 25% wakati wa kuhifadhi nafaka.
Kuhakikisha kunakua na mzunguko mzuri wa hewa gharani wakati wote.
Wakati wa uandaaji chakula
Kusafisha/kuandaa; Mahindi na karanga zisafishwe vizuri kabla ya kutumika kama chakula.
Kuchambua na kuziharibu mbegu zinazoonekana kuathirika na kubadirika rangi na hata kuharibiwa na wadudu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom