CONSTRUCTIVE THOUGHT
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,158
- 417
Kwa wale wanaokopa mikopo katika taasisi zinazotoa mikopo kwa masharti nafuu mfano FINCA na PRIDE wapaswa kuelewa kuwa hakuna sheria ya dhamana ya mkopo ya vitu vya ndani.
Katika kulitambua hili, taasisi hizi huitaji mkopaja awe katika kikundi kisichopungua watu watano. Hii inamaanisha kuwa ikiwa mkopaji mmoja au wawili watashindwa kurejesha mkopo, wenzake waliobaki watanapaswa kurejesha mkopo wote husika.
Sasa pamekuwa na upotoshaji kwa Taasisi hizi kwa kuwataka wakopaji kuweka dhamana ya vitu vya ndani (Samani za ndani) ili wapate sifa ya kukopeka. Na ikitokea mkopaji kashindwa kurejesha mkopo husika, hufirisiwa / hubebewa vitu vyake vyote vya ndani kama fidia ya kumalizia deni la mkopo.
Kimsingi huo ni uvunjaji wa sheria kwani hakuna dhamana ya mkopo ya vyombo vya ndani kisheria. Hivyo mtu alionyanganywa vyombo, anapaswa kuwafungulia kesi ya wizi wale wote waliohusika katika unyangaji huo.
"Kutokujua sheria sio sababu ya kusamehewa sheria"