Ifahamu sayari ya Mars...

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,962
Natumai mko poa wakuu.

Leo tunaendelea tena na kufahamishana juu ya madude yaliyo ktk mfumo wetu wa jua, hebu tuiangalie sayari ya Mars kwa undani zaidi.

1. Sayari ya Mars ni ya nne (4) kutoka umbali wa jua.

2. Ni sayari ya 2 kwa udogo baada ya sayari ya Mercury.

3.Ina miezi (moons) 2 ambayo ni midogo,ambapo mkubwa unakisiwa kuwa km 11 na mwingine km 6.2.

4. Mars ni terrestrial planet. (yaani ina ardhi kama yetu duniani)

5. Nguvu yake ya uvutano (gravity) ni sawa na kusema ukiwa Mars hatua yako ya kawaida huku duniani, ukiwa kule Mars inakuwa zaidi ya mara tatu na nusu. ( kwahiyo utakuwa kama unarukaruka)

6. Kilo zako za duniani unazipunguza kwa 38. (kwa mfano ukiwa na kilo 65 huku, kule utakuwa na kilo 27.)

7. Mars ulizunguuka jua kwa siku (days) 687,na hivi ndio inavyolizunguuka jua.

170px-Marsorbitsolarsystem.gif


8. Ni sayari iliyotembelewa na vyombo vingi sana kutoka duniani.

Na hapa ni jinsi miezi yake miwili,phobos na deimos inavyoizunguuka Mars.

Orbits_of_Phobos_and_Deimos.gif



Haya sasa ONGEZEENI AU PUNGUZENI NA KAMA VIPI REKEBISHENI ILI TUELIMISHANE ZAIDI.
 
Bila shaka nitakuwa nazeeka kwa kasi sana, maana sijakupata kabisa japo nimerudia mara 7 kusoma.
Jamaa yupo sahihi tofautisha mass na weight hiyo table uliyoweka hapo inaendana na weight na siyo mass, mass kizio ni kg, gram na weight ambayo SI unit yake ni Newton(N). Kwa mfano we mass yako ni 100kg basi weight yako ni 1000. Weight=mass*gravity, kwa hiyo gravity inatofautiana kutoka sayari moja hadi nyingine ambayo dunia kimakadirio ni 10.
 
Jamaa yupo sahihi tofautisha mass na weight hiyo table uliyoweka hapo inaendana na weight na siyo mass, mass kizio ni kg, gram na weight ambayo SI unit yake ni Newton(N). Kwa mfano we mass yako ni 100kg basi weight yako ni 1000. Weight=mass*gravity, kwa hiyo gravity inatofautiana kutoka sayari moja hadi nyingine ambayo dunia kimakadirio ni 10.
Hapa nimeelewa.
 
Mass ni uzito haubadiliki popote pale ktk universe hii Tunaupima kwa kilogram ukiwa na kilo moja earth utakuwa nayo hio hio mars tofauti tu ni kuwa ktk kila sayari kuna gravitational yani force inayovuta vitu kuelekea ktk centre ya icho kitu, Force hio ya kuvuta kitu downward inatofautiana sasa combination ya hio force na mass ya hicho kitu unapata weight, yani Pulling force toward the centre of something..Gravity ina vary hata hapa dunia 9.8 ni constant theoretical but walio ktk poles za dunia gravity ni kubwa kidogo compare na wengine kuna sehemu gravity mbili zina balance huko angani na panakuwa weightless tunapaita Null point
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom