Ifahamu pinephone, simu inayotumia mfumo endeshi(os) ya linux

Cainan

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
414
470
Pinephone ni Moja ya simu ambayo hutumia mfumo endeshi wa Linux , simu hii hutengenezwa na kampuni ya pine64 huko Poland

Kwa wale watu ambao wanapenda uhuru katika matumizi ya simu janja, basi Moja kwa Moja watakubaliana na Mimi ya kuwa simu za Linux zinatoa usalama mkubwa ukilinganishwa na mifumo endeshi mingine

Simu hii imejikita zaidi katika matumizi yalio wazi (privacy and freedom).

Moja kwa Moja nizitaje specifications za simu hii ..TAHADHARI. Simu hii haina features nzuri zaidi kwa upande wa hardware hivo huwafaa zaidi watu wanaojikita katika privacy na freedom hivo kwa wale ambao hupenda picha na multitasking hii sio simu yao .

Body... Simu hii Ina mwelekeo (dimension) wa 160.5mm , Ina uzito wa gram 185 , imetengenezwa kwa material ya plastik , inakuja na option Moja tu ya rangi nyeusi pia hutumia line ndogo zilizokatwa (micro Sim)

Muonyesho (display) simu hii inakuja na technolojia ya HD IPS (In plane switching) capacitive touch screen hii ni control display ambayo hutumia electrical properties za mwili wa binadamu kama input , Simu hii Ina ukubwa wa inch 5.95 .. resolution (uwezo wa simu kuonyesha pixel au doti hupimwa kwa pixel per inch ) ni 1440x 720 pixels ni kiwango Cha kawaida kwa simu kama hii...pia aspect ratio(uhusiano kati ya urefu na upana) ya simu hii ni 18;9

Operating system (OS) ya simu hii ni LINUX , hivyo mtumiaji anaweza kuhama kutoka os Moja kwenda nyingine mfano Debian kwenda Ubuntu ,, simu hii huja ikiwa pre installed na Manjaro hivo simu hii huweza ku support Hadi OS 7 za Linux hivo kupata uhuru

Chipset: simu hii Inakuja na chipset za allwiner A64 kama unavyojua chipset hizi zimekuwa zikitumika katika computer basi simu yako ya pinephone inaweza kutumika kama computer ikiwa connected kwenye monitor

CPU ya simu hii 64bit Quad core 1.2 GHz ARM cortex hivo hufaa kwa matumizi ya kawaida

GPU (hii ni processor ambayo inajihusisha na kurahisisha utengenezwaji wa picha ) MALI-400MP2

Kwa upande wa storage
Simu hii huja na 16/32GB versions internal memory kutokana na model utayochagua,,

RAM ya simu hii ni 2/3 GB versions
Kwa upande wa external memory simu hii huweza kusapoti Hadi 2TB hivo kuwa na uwezo mkubwa

CAMERA
Camera ya nyuma simu hii huja na Single 5MP, 1/4" ikiwa na LED flash
Camera ya mbele simu hii huja na 2MP ,f/2.8, 1/5"
Pia huja na audio jack Ambalo huweza kusapoti loudspeaker
Simu hii husapoti LTE, 3G ,2G

Targeted specs
Simu hii imekuja na technolojia ya kuzima switches
Simu hii inauwezo wa ku disable GPS , LTE , CAMERA , WIFI , BT & MIC
Hivo kutoa usalama kwa mtumiaji pindi anapotumia , kwa mfano simu huwa na kitu kinaitwa MAC address hivyo kutoa location ya kifaa hivo kupitia simu hii utaweza kuzima na kujiongezea anonymity

La mwisho kabisa ni bei ambayo ni $ 149 kwa model ya kawaida na 199$ kwa 3GB/32GB . Simu hii hupatikana kwenye store ya pine 64

WELCOME TO LINUX FAMILY.

1630908145423.png
 
Daah picha imegoma kufunguka ila ntaitafuta hii...kwaio nayenyewe ni mwendo wa kutembea command tu au??hii inaweza kuperform kaz kama linux ya PC mkuu?yaani ninamaswali mengi ila NTAITAFUTA By hook,by croock
 
yaani ninamaswali mengi ila NTAITAFUTA By hook,by croock
Pitia reviews zake online/youtube.

Nimependa hii comment hapa chini

"The wider Linux community is also hard at work porting a swathe of other OSes to the device. Regardless of which OS the handset actually ships with you’re free to download, boot and install any OS you choose, both internally and from the phone’s microSD card."
 
Daah picha imegoma kufunguka ila ntaitafuta hii...kwaio nayenyewe ni mwendo wa kutembea command tu au??hii inaweza kuperform kaz kama linux ya PC mkuu?yaani ninamaswali mengi ila NTAITAFUTA By hook,by croock
Ndio mkuu inasapoti application za desktop Linux pia inaweza kuwa turned into a computer ikiwa connected na USB C dock yake ambayo inakuja kwa model ya convergence package unaweza connect monitor, keyboards and other peripherals
 
Bora utumie simu za Sony, zipo model ambazo unaweza weka os yoyote za kisasa na reliable. Mfano Xperia 10 II.
Hii ni kwaajili ya developers na the likes , can be used as a second phone ...sio simu kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikumbukwe Kila mtu ana kitu anachokipenda kwenye masuala ya simu ...THIS IS FOR DEVELOPERS that's why haijatoka community version ambayo ingetumika kama official product ..Wana hama hama from different Linux distribution Ili ku determine which OS work best ..na ndio maana price tag inaanzia $149~200

Je bei ya Xperia 10 II ni Tsh ngap ?
Je inaweza support Linux distros ?
Anyway all in all ni kutokana na preference ya consumer
 
Nimekutajia Hio simu makusudi sababu nafahamu matumizi ya pine unafanya pia kwenye hizo xperia.

So far Ukitaka kutumia sailfish os (moja kati ya reliable distro ya Linux ya simu) inabidi utumie hizi xperia.

Unaweza ukaona list yake hapa

Baadhi ya os unazoweza kuweka ni kama Sailfish os, Ubuntu touch, post markets (inayokuja na hio pine phone) na dsitro nyengine.

Na kwa bei zipo za bei za Chini kama xperia XA series nyingi ni chini ya hio $150.
 
Okay tupo pamoja mkuu ..thumb up
 
Back
Top Bottom