Ifahamu Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Joined
Jun 26, 2024
Posts
33
Reaction score
46
Taarifa binafsi ni mali ya mhusika (mmliki wa taarifa). Haitakiwi kutolewa na mtu mwingine, kwani mhusika ndiye anayefahamu taarifa zake kwa usahihi, isipokuwa pale inapobidi kisheria au kwa ridhaa yake.

Ukusanyaji wa taarifa binafsi unatakiwa kufanywa na mamlaka au vyombo husika kwa kuzingatia sheria na miongozo na lazima uzingatie malengo ya ukusanyaji wa taarifa hizo. Taarifa zinazokusanywa zinapaswa kuwa sahihi na mahsusi kwa ajili ya lengo husika na si vinginevyo.

Kabla ya ukusanyaji au uchakataji kuanza, wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi wanapaswa kutoa elimu ya kina kwa wamiliki wa taarifa. Elimu hii itahusu; aina ya taarifa binafsi zitakazokusanywa, malengo au matumizi ya taarifa hizo, namna taarifa zitakavyohifadhiwa, muda zitakapotunzwa na hatua za usalama zinazochukuliwa ili kulinda taarifa hizo.

Ni jukumu la kila mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi kuomba ridhaa ya mmiliki kabla ya kuzikusanya au kuzichakata. Wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi wanao wajibu wa kuhakikisha taarifa ziko salama na hazitatumika kinyume na malengo yaliyotolewa wakati wa ukusanyaji.

Ili kuhakikisha ushirikiano kati ya wamiliki wa taarifa binafsi na wakusanyaji au wachakataji wa taarifa hizo, ni lazima elimu itolewe awali kabla ya ukusanyaji au uchakataji kuanza.

Je una kero ambayo umekutana nayo katika watu au Taasisi mbali mbali kuomba taarifa zako binafsi bila ufafanuzi wa kujitosheleza? Ziandikie kwenye Comments!!!
 
kero tunaleta hapa au e-mrejesho?
 
hivi ni binafsi za ukweli ama kwa wachache tuu inasikitisha sana .
 
Back
Top Bottom