Ifahamu miji iliyowahifadhi wauaji...

Ifahamu miji iliyowahifadhi wauaji...

Online Pastor

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
1,948
Reaction score
1,524
Ukiua sharti uuawe.
Ila ukiua bila kukusudia ungependa ufanywe nini?


Enzi za Biblia,mtu anapoua bila ya kukusudia,ili asiuawe ilimbidi akimbie na kujificha kwenye moja
ya miji sita ya kimbilio kati ya miji 48 ambayo
kabila la Walawi walipewa katika
Israeli nzima.


Lengo la miji hii sita ya kimbilio ilikuwa ni kuwapa wakosaji nafasi ya kupata hukumu iliyo haki,kwani baaada ya kukimbilia kwenye hii
miji,wauaji waliwekwa kizimbani na ilipofahamika kuwa ni waovu na waliua kwa kusudia ilibidi wabaki kwenye hiyo miji sita hadi kifo cha kuhani mkuu wa wakati
huo.


Kuhani mkuu akishakufa walikuwa huru kwenda majumbani pasipo
na mtu yeyote kuwafanya
chochote!

Ila walipokaidi na kurudi
makwao walikosababisha
majanga,wale ndugu wa
marehemu walikuwa na haki ya kumwua ili kulipa kisasi.


TUNAJIFUNZA NINI?


Kimbilio kuu la mwanadamu la
kwanza ni Serikali,ila Serikali inaposhindwa basi Mungu ndiye
kimbilio la mwisho
Mungu ndiye mtoa haki asiye na mawaa.
Tumtwike fadhaa zetu,yeye atazitatua!


REFERRENCES:
Yoshua 20
Hesabu 35:1-28

Nakaribisha mialiko ya semina,warsha na makongamano ya kiroho.
Wasiliana nami @ pastoronline4@gmail.com

=============
Nakaribisha mialiko ya semina,makongamano,warsha na mikutano ya kiroho.
 
Pamoja sana mchungaji kwa somo la asubuhi..
Qn. Enzi za Biblia ni zipi? Zilianza mwaka upi na upi?
 
Hawa Walawi ndo wale wa fungu la kumi?
 
Sumu unamanisha ndiyo kundi lililopokea fungu la kumi?

Kama ndiyo,hao ndiyo wenyewe!
 
Mji wa kimbilio
the_city_of_refuge.jpg
 
Hivi ninyi akina Online pastor, ni nani mnafundishwa nani hizo heresies au upotofu? Ni lini Mungu wa Yesu Kristo (labda una mungu tofauti) alisema kuwa kimbilio la watu ni serikali? Yohana 15:3 Kaeni ndani yangu nami ndani yenu, bila mimi HAMWEZI JAMBO LOLOTE.
Jitahidini kuacha mafundisho yenu ya akili mwenu!
 
Verily Verily mamlaka ziko duniani kwa niaba ya Mungu,zikishindwa kutatua shida za watu ndipo Mungu huingilia kati.

Au uliposikia Serikali ukafikiri namanisha hii ya CCM pekee?
 
Back
Top Bottom