Hii ni moja ya dini changa iliyoanzishwa karne ya 19.
Ilianzia Mashariki ya Kati katika nchi ya Iran.
Waanzilishi wa dini hii ni Bab na Bahaullah.
Makao makuu ya dini hii ni Haifa nchini Israeli.
Wabahai wapo takribani millioni 7 duniani,huku nchi ya India ikiwa namba moja kwa wingi wa Wabahai wanaofikia milioni 1.
Kenya ni namba moja kwa Afrika ikiwa na waumini 522,000+ huku Tanzania ikiwa na waumini 109,000+!
Wabahai wanaamini dini zote ni sawa na waanzilishi wote wa dini zilizo duniani kuwa wanamwakilisha Mungu
Wanaani kuwa kila baada ya miaka 1000 Mungu hutuma mdhihirishaji/nabii ambaye huja duniani kuleta ujumbe wa Mungu kuwafundisha watu.
Wadhihirishaji hao ni Adamu,Abrahamu,Isaya,Buddha,Krishina,Zoroaster,Yesu Kristo,Muhammad,na sasa Bahaullah!
Hivyo baada ya miaka 1000 atatokea nabii wa kuchukua nafasi ya Bahaullah!
IMANI YA WABAHAI:
1)Wanaamini uwepo wa Mungu mmoja,
2)Wanaamini Mungu hawezi kujulikana kirahisi na kila binadamu,hivyo kila baada ya miaka 1000 hutuma mdhihirishaji au nabii kuja kuufundisha ulimwengu
3)Wanaamini dini zote ni sawa kwenu yale mambo inazofundisha yanatoka kwa Mungu
4)Wanaamini katika usawa kijinsia,kitaifa na kidini
5)Wanaamini katika utafutaji wa ukweli pasipo kufungwa na imani za uchawi au mila za jamii ulimo.
Somo linaendelea...