Ifahamu Cabotage Law

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,955
12,532
Cabotage Law hii ni sheria inayowekwa na nchi ili kulinda huduma za usafirishaji wa ndani wa majini kwa wazawa/kampuni za ndani kutoa huduma kati ya bandari moja na nyingine ndani ya mipaka ya nchi.

Mfano, kwa bandari zilizo pwani ya Bahari ya Hindi ambazo ni Tanga, Dar es Salaam, Mtwara, Unguja na Pemba, kama kuna kampuni itatoa huduma lazima iwe ni ya Tanzania.

Asilimia 80% ya nchi 91 zenye pwani ya bahari zimepitisha sheria hii ili kulinda maslahi ya huduma na makampuni ya ndani. Moja ya hayo mataifa ni China, South Korea, Russia, Japan, Chile, Mexico, Brazil, Argentina, Australia, and Canada.

NCHI NYINGINE ZILIVYO TAFSIRI

India

Wao Cabotage Law imeruhusu meli za kigeni kufanya usafirishaji wa mizigo ya ndani ambayo ipo kwenye kontena kutoka bandari moja kwenda nyingine ndani ya nchi. Sababu kubwa wao waliona ni kuwapunguzia gharama wasafirisha mizigo.

Nigeria
Cabotage Law nchini kwao wao wanataka ili usafirishe mizigo ndani ya bandari zilizo katika mipaka ya nchi lazima meli iwe imesajiliwa na inapepea bendera ya Nigeria na mmiliki awe na uraia wa Nigeria.

Tanzania bado tuna vyombo vichache baharini hivyo tutumie sheria hii kuwapa Wazawa nafasi wawekeze na waachiwe kazi zote za usafirishaji ndani ya mipaka ya nchi.
 
Back
Top Bottom