Ifahamu Barchelor of science in audiology and speech language pathology

Ifahamu Barchelor of science in audiology and speech language pathology

Dr kijaji

Member
Joined
Apr 17, 2025
Posts
9
Reaction score
13
Shahada hii inalenga kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kutambua, kutathmini, na kutibu matatizo ya usikivu, usemaji, lugha, na kumeza kwa watu wa rika zote. Wataalamu hawa husaidia watu wenye matatizo ya kusikia, kuzungumza, na kuelewa lugha.

Vyuo Vinavyotoa Programu Hii:
Kwa sasa, chuo kinachotoa shahada hii nchini Tanzania ni Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) na imeanzishwa 2023/24, ikimaanisha mpaka Sasa hakuna mtaalamu ata mmoja alie graduate. Na capacity ya chuo ni wanafunzi 10 Kila mwaka.

Kwa muhtasari huo, mpaka Sasa hakuna wataalamu wa hiyo fani tanzania Bali kazi zao maranyingi hufanywa na ma specialist wa ENT( otorhinolaryngologist) na baadhi ya medical officers waliopitia mafunzo maalumu.

Idadi ya wataalamu ni ni chache sana, na fursa za ajira ni kubwa. Ni wakati wa kiwashauri wadogi zetu wanaotarajia kumaliza advance mwaka huu kufikiria program Kama hizi na nyinginezo, kuliko kukariri program za afya Kama MD, pharmacy, nursing zenye mafuriko ya watu.
 
Back
Top Bottom