If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 28, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,659
  Likes Received: 23,892
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshindi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025 and may be more!, anayesubiri tuu kutangazwa rasmi na kuapishwa. Nimesema 2015 -2025 sio kwa bahati mbaya as if hakuna uchaguzi 2020, no!, nimesema 2015-2025 kwa sababu huu ndio ukweli ninaouona mimi muona mbali ni kuwa kwa nature ya udikiteta huu wa Magufuli, kama hautakuwa countered through proper channels kupitia instruments zilizopo, then, mwaka 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais wala uchaguzi wa vyama vingi!, bali litafanyika igizo tuu la uchaguzi, ambao utakuwa ni uchaguzi wa chama kimoja tuu CCM!. Uchaguzi mwingine wa vyama vingi wa rais na wabunge ni 2025 tena only if hatautumia udikiteta wake kubadili katiba kwa mlango wa nyuma, ili aendelee kama Mkuruzinza, Kagame, Museveni na Mugabe!.

  Kuna walioshindana nae ndani ya CCM, hawa ni washindani, kati nyao kuna waliopingana nae, hawa ni wapingani, kuna waliopigana nae vikumbo!, hawa ni wapigani, na kuna waliopingana naye kisiasa, hawa ni wapinzani. Kwa vile sasa mshindi ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hii inamaanisha, hao wengine wote who were fighting, they tried to fight him but couldn't beat him!, as a result thay lost, hivyo as of now, wote walioshindwa, are all are the looses!. Kwenye unrepresentative democracy, the winner takes it all, and the looser standing small!. Kura ni zile milioni 8 tuu!, zile milioni 6 is nothing!, ukiishashindwa unasimama pembeni, ama uendelee kulia na kuugumia maumivu ya kushindwa, au ukubali kushindwa, na kujipanga upya kwa mpambano unaofuata!.

  Kuna huu msemo wa wahenga usemao, "if you can't beat them, join them!". Nawashauri makundi hayo yote walioshindwa, kwanza kukubali kushindwa, kwani asiyekubali kushindwa sio mshindani, hivyo natoa mwito kwa washindwa wote, ku surrender kwa kuweka silaha zao chini na to join him, sio kwa kupenda, but they have to join him because, there is no any other way out, or any options but they have either to join him or to fall out!, hiyo ndio salama yao wakati wa kusikilizia kama atakuwa dikiteta kweli au a benevolent one!. Akiwa dikiteta kweli usipomjoin, umekwisha!, hivyo Tanzania tunaelekea kwenye totalitarian nakurudi kuwa nchi ya chama kimoja!. Hata akiwa a benevolent one, bado upinzani hatafurukuta hata kule kwenye ubunge na udiwani, wapinzani wataokarudi bungeni 2020 ni by personal merits only, as of now, namuona mpinzani mmoja tuu mwenye uhakika wa kurejea bungeni 2020, huyu ni ZZK pekee, wapinzani wewngine wote ni majaaliwa!.

  Wito huu wa kumjoin Magufuli, unatolewa regardless umeshindwaje!, iwe ni kwa ushindi halali, ushindi haramu, bao la mkono, etc, etc, kwenye uchaguzi, the end will always justify the means!, mshindi ni Magufuli, sasa tumpatie tuu kila aina ya ushirikiano wa kutosha kwa kum join himn ili aweze kulitawala viruzi taifa letu hili.

  Tena hapa mtawashuhudia baadhi ya wale ma-opportunists waliojiengua CCM kumfuata Edward Lowassa upinzani, wakitumaini Lowassa angeshinda lakini kwa vile Lowassa ameshindwa, na CCM ndio imeshinda, they see no more opportunities in Chadema, mtawashuhudia wakipiga magoti na kulamba matapishi yao kwa kurejea CCM, because walijiunga upinzani just in search of opoortunities tuu, now they see no more opportunities they expected kwenye opposition, hivyo watajilambia tuu matapishi yao na kujirejeleza zao nyumbani kwao CCM kama alivyofanya mwana mpotevu, na watapokelewa kwa shangwe hadi wengine kufanyiwa karamu!.

  Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM nilipandisha uzi huu,
  Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,

  Makundi hayo ni ..."The Top Ten who can make the worst dictators
  Kundi la 8: The Top Ten who can make the worst dictators
  Nikizungumzia kuhusu baadhi ya wagombea urais wa CCM, wakipita wana hatari ya ku make the worst dictators, John Pombe Magufuli was number 2 ya Rais who can make the worst dictator this country has ever had!.


  Hoja kuwa Magufuli ni dictator haina mjadala, kwa watu wenye jicho la tatu, wanaona the fire on his eyes, and then fear is the weapon on his heart kwa kutoa hotuba za ukali kama agamba!, ambayo ni kiashiria cha seriousness ya hasira ambayo inaweza kugeuka chuki na kupelekea visasi toka moyoni mwake, kwa kila atakayetofautiana naye!, na wenye sikio la tatu wanaisikia tone ya ukali wa ukatili kwenye sauti yake!, hii ni ishara kuwa huyu sio mmtu wa masaihara, watakaotofautiana nae, wanaweza kuumia au hata ...(God forbid). Kitu cha muhimu sana cha kufanya kwa sasa ni sisi waote Watanzania, katika umoja wetu, kumuombea tuu kwa Mungu, very seriously angalau Mungu amfanye kuwa ni a benevolent one ili huo udikiteta wake ulisaidie taifa kusonga mbele kiuchumi na kiustawi at a price of dead democracy!, vinginevyo akiwa the real one, tutajuta!.

  Jakaya Kikwete ukiondoa mambo yake ya uswahili swahili, alikuwa ni mtu wa watu, ni mtu mwenye huruma sana iliyopitiliza kiasi cha kutafsiriwa kuwa Kikwete alikuwa ni Rais dhaifu, hivyo CCM ya Kikwete ilikuwa ni CCM dhaifu! hivyo Kikwete alibezwa, alitukanwa, na kufanywa CCM ya mchezo mchezo, lakini CCM ya Magufuli itakuwa sio CCM ya mchezo mechezo, au CCM ya huruma huruma, itakuwa hakuna mchezo wala mswalie Mtume, hii CCM ya hapa kazi tuu!, CCM imara ni kitu hatari sana kwa majaaliwa ya upinzani!.

  Upinzani Tanzania umeweza kushamiri kutokana na CCM lege lege, hivyo Magufuli akijenga CCM imara, huu upinzani lege lege uliopo nchini Tanzania hivi sasa, mwisho wake utakuwa ni 2020, Tanzania tunarudi kule kule kwenye nchi ya chama kimoja!. Ndio maana nimesema 2020 hakuna uchaguzi wa rais kutafanyika tuu igizo la uchaguzi!.

  Kwenye uzi wangu huu,
  Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour!, nilimzungumzia JK kuwa sifa kubwa iliyomfanya CCM impitishe ni cheko na bashasha zake!, hivyo JK tumemchekea, tumemdhihaki, tumembeza, tumemkejeli, hadi kumchezea sharubu kama babu na wajukuu zake huku yeye akicheka tuu na kuyaacha yapite. Lakini kwa Magufuli, sijui kama kutakuwepo kuchekacheka au kuchekeana, kubezana na kuchezeana, na kubembelezana, kwa Magufuli ni mambo serious kwa kwenda mbele na hakuna mchezo mchezo, ni kazi tuu!.

  Wajameni japo kwa sasa naongea kama utani au mzaha, lakini hili ni angalizo muhimu sana kwa majaaliwa ya freedom of expression, freedom of speech, na freedom of press ya uhuru huu usio na mipaka tulionao sasa nchini mwetu, tukiwemo sisi humu jf, tulio enjoy wakati wa Kikwete, lakini mbele ya unpredictable dictator kama Magufuli, kiukweli kabisa huko tuendako, kama hatabadilika, then ni mashaka matupu!, salama yetu hata sisi jf pia ni tumjoin him kwa kumsifu kwa nyimbo na mapambio, vinginevyo....

  Thanks God, mimi ni mmoja wa wana jf wachache, waliopata priviledge ya kujua huyu Magufuli aliibukia wapi na ilikuwaje kuwaje hadi akawa ndie akawa mgombea wa CCM na sababu ni zipi zilifanya awe ni yeye. Ukilisoma bandiko hili ukazijua sababu zilizosababisha akawa Magufuli, labda utanielewa nazungumzia nini!.
  Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!

  Hivyo kwa nature na hulka ya udikiteta wa Magufuli, let's hope, kuwa zile sababu zilizopelekea kuwa mgombea wa urais wa CCM ndizo pekee (the ones and only) zitakazo weza kumcheck and balance him in between being a real dictator and a benevolent dictator vinginevyo hata hao CCM wanaoshangilia ushindi kwa sasa, akitokea kuwa a real one, hata CCM wenyewe nap watakuja kujuta!, therefore, to be on a safe side, it's better if you can't beat them, just join them, to be on a safe side!.

  Wapinzani wote wakiwemo wana Chadema, wana UKAWA, na Watanzania wenzangu kwa ujumla, najua wengi wenu mlimtaka Lowassa, mmemkosa!, na badala yake mkapewa Magufuli, hivyo natoa wito wa "If you can't get what you want, just take what you get!", ukikosa ulichotaka, then pokea ulichopewa!, tumkubali Magufuli kwa moyo mkunjufu, hivyo hivyo alivyo na udikiteta wake, tumpokee na kumpatia kila aina ya ushirikiano wote unaohitajika kumuwezesha kuiongoza vema na sala hii Tanzania yetu. Tanzania sio nchi ya Magufuli wala Tanzania sio mali ya CCM, Tanzania ni ya Watanzania wote, ni nchi yetu sote, hivyo it can be done kama kila mmoja wetu will play his part!.

  Sio tumjoin Magufuli kwa sababu sasa ndio tunampenda hivyo tumemkubali, no way, tumjoin Magufuli kwa kumkubali ndie the only one rais tuliyepatiwa na Mungu, hivyo we have duty and a responsibility to join him kwa lazima, tutake tusitake, tupende tusipende, yeye ndie rais wetu hivyo we have to join him and support him because we have to!.

  Kwa kuweka tuu kumbukumbu sawa, hata mwaka 2010 Chadema waliposhindwa, walisusia matokeo walijidai kunsusa na kujidai hawamtambui JK, lakini hatima yake ilikuja kuwa hivi

  Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza!

  Bandiko hili liliwaudhi sana Chadema humu jf, Mwana JF, Regia Mtema (RIP) akanitaka niombe radhi
  Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya ....

  Radhi iliombwa
  Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya ...

  This same, same scenario inataka kujirudia kwa Chadema na Ukawa kujidai kutaka kumsusia Magufuli!. Kuna vitu mtu unaweza kususa na kuna vitu huwezi kususa!,kwa hata 2010 Chadema walisusa lakini tukawashuhudia makamanda wakifakamia chai, juice na vitafunwa vya ikulu, huku meno 32 nje kwa vicheko, hivyo hata awamu hii ya Magufuli, msije kushangaa Mbowe akiwaongoza tena makamanda, akiwemo Lowassa kubisha hodi ikulu na kumpongeza Magufuli.

  Paskali
   
 2. babatovu

  babatovu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2015
  Joined: May 5, 2014
  Messages: 2,747
  Likes Received: 1,068
  Trophy Points: 280
  Over my dead body....
   
 3. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2015
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tumekusikia Pasco .... my laugh comes last!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 28, 2015
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,523
  Trophy Points: 280
  The prospect of CCM being in power for almost 60 years makes me sick to my stomach!

  Not only that.

  The fact that Magufuli is the least qualified of all past CCM presidential nominees and therefore the likely next president for the next 10 years is hard to bear and unforgivably cringeworthy!
   
 5. Malinyingi

  Malinyingi JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2015
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 855
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa uzi wako huu nafarijika sasa kuamini ushindi upo Mlangoni mwa CCM.....CCM Oyeeee
   
 6. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2015
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 280
  Mwanaume asiekuwa na msimamo ni Janga kwenye jamii... kaa hivyo hivyo ka bendela fata upepo
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2015
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,660
  Likes Received: 14,687
  Trophy Points: 280
  Alinselema ....

  Selema selema...

  Tanzania oyee

  Mwanza oyee

  Shinyanga oyee

  Geita oyee

  Simiyu oyee

  Kagera oyee

  Morogoro oyee

  Manyara oyee

  Dodoma oyee

  Singida oyee

  Tanga oyee

  Tabora oyee

  Kigoma oyee

  Ruvuma oyee

  Katavi oyee

  Mbeya oyee

  Musoma oyee

  Iringa oyee

  Musoma oyee

  Dar oyee

  Zanzibar oyee

  Pwani oyee

  CCM OYEE

  Tanzania oyeee!

  Hebu imba kwa sauti ya Magufuli!
   
 8. Ethical Ninja CEH

  Ethical Ninja CEH JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2015
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,491
  Likes Received: 1,897
  Trophy Points: 280
  Uikumbuke hii

  Edward N. Lowasa Rais JMT 2015-2020


   
 9. el nino

  el nino JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2015
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 3,453
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  Magufuli alishakuwa Rais tangia alivyoteuliwa na CCM
   
 10. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2015
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 14,727
  Likes Received: 7,845
  Trophy Points: 280
  tulishwahi kuonya kua nchi haiwezi kuchukuliwa kwa propaganda na uongo uongo mitandaoni, hicho ndio kilichotokea, mkajipange
   
 11. b

  babampigi JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2015
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 364
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Katika watu nilokuwa nawakubali humu jukwaani nawe ulikuwa mmoja wapo! Kwahiyo umekubali hayo matokeo??? SAD.
   
 12. Tyta

  Tyta JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2015
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12,840
  Likes Received: 2,880
  Trophy Points: 280
  there are Two possible outcomes with Magufuli
  1.MAGUGULI BEING ''MAGUFULI''.....
  2.A ''REMOTE CONTROLLED'' MAGUFULI
   
 13. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2015
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,863
  Likes Received: 10,526
  Trophy Points: 280
  Magufuli si dictator!! ni mtu duni mno kifikra (****) labda ungesema tutapata mfalme **** ungeeleweka....

  Nukuu kauli yangu huyu jamaa atakuwa ni kilaza kupita wote waliomtangulia....
   
 14. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2015
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mzeiya vipi tena? Angalia red hizo.
   
 15. m

  mtoto wa mjini JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2015
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 1,756
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Pasco, always ahead.
   
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2015
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,511
  Likes Received: 3,032
  Trophy Points: 280
  Kumkubali Magufuli kwa shingo upande inawezekana, lakini kuikubali CCM...hell noooo!!
   
 17. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,711
  Likes Received: 5,591
  Trophy Points: 280
  Magufuli will be remotely controlled from Msoga..!!! Like Bulldozer...!!!

  Naamini 100% kwa uhakika kabisa.....MAGUFULI HAWEZI kamata mali ya ma trillions za JK, Mkapa au Kinana...!!!

  Naamini 100% kwa UHAKIKA..!! MAGUFULI HAWEZI fumua mikataba mibovu JK aliyo ingia hata kidogo...!!!

  So, WATANZANIA watabakia MASKINI WA KUFA...ufukara hadi wakome...!!!

  Watanzania ndio WAKOME... NATAKA WAPATE SHIDA KUU, NA DHIKI KUU... ILI wapate akili na kujua adui wa maisha yao ni CCM...!!!

  Na DHIKI kuu kwa wananchi ndio INAANZA...!!!

  WATANZANIA WATAJUTIA KUIRUDISHA CCM MADARAKANI...!!!

  NEC ni ya CCM 100%... UKAWA, wangetakiwa wakomae kabisa kabisa... wapate TUME HURU YA UCHAGUZI...!!!

  HAPA NI WIZI WA KURA TU...!!!

  NEC ni ya CCM...!!! So, UPINZANI sasa wakatae NEC na wakiingia tu BUNGENI... WATAKE TUME HURU YA UCHAGUZI...!!!

  BILA TUME HURU YA UCHAGUZI NI BUREEEEEEEEEE....!!!
   
 18. WILE

  WILE JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2015
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,609
  Trophy Points: 280
  **** kampita genius Lowassa..!!!Maajabu enhe
   
 19. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2015
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,610
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja

  Hapa kazi tu

  Nimechoka dharau za wafanyakazi wengi wa serikali kama vile unachotaka wafanye ni kosa huku ni wajibu wao.

  Na bado watanyooka tu
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2015
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,248
  Likes Received: 1,985
  Trophy Points: 280
  Pasco Imekuwaje?

  Matokeo yameshapikwa? Au kura zisipotosha zitatoshelezwa?

  Tanzania ni maajabu ya 9 ya dunia.

  Unamkabidhi Pombe nyumba zako anazipiga makufuli na bado unampigia kura?

  NEC tu inajaribu kuwachora wadanganyika. Kwa nini NEC haikuanza kutangaza matokeo yanayoonesha kumpa Mamvi ushindi? Unafikiri NEC inafanya hivyo kwa kubahatisha, bahati mbaya au kimkakati?

  Na Wewe Pasco unawasaidia NEC?

  Tz ni zaidi ya uijuavyo. Ni maajabu ya dunia, Ni nchi ya wadanganyika.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...